Tofauti na kugawa fedha moja kwa moja kwa wananchi, njia zipi zitumike kuhakikisha kwamba mafanikio ya Serikali yanawafikia Wananchi?

Tofauti na kugawa fedha moja kwa moja kwa wananchi, njia zipi zitumike kuhakikisha kwamba mafanikio ya Serikali yanawafikia Wananchi?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Wanabodi,

Takwimu mbalimbali zinaonyesha jinsi ambavyo uchumi wa Tanzania umekuwa ukibadilika.

Ingawa njia hii inaweza isielezee kwa uhalisia kinachojiri kwenye nchi tofauti, GDP bado ina angaliwa sana kwenye masuala haya ya uchumi.

Kwa Tanzania, GDP imekuwa ikiongezeka kwa asilimia fulani kila mwaka lakini kwa bahati mbaya mafinikio haya ya serikali hayaja onekana sana kwa wananchi.

Je, kuna njia zipi zinazoweza kutumiwa kuhakikisha kwamba matunda ya kazi nzuri inayofanywa na serikali yanawafikia wananchi?.

Endapo Tanzania ikiweza kuwa nchi ya kipato cha juu, tutegemee kitu kipi cha ziada kinachoweza kumkwamua mwananchi mwenye kipato cha chini mpaka awe na kipato cha juu?

Je, kujikwamua kiuchumi kuna maanisha kutumia nguvu zako mwenyewe?

Je, kugawa fedha moja kwa moja kwa wananchi kunaweza kusababisha madhara yapi?

Labda kuwa wezesha wananchi kujiajiri wenyewe, labda kuboresha kilimo.

Nini maoni yako?
 
Tuwe na bodi ya mikopo itakayowakopesha wahitimu hususani Kilimo,Afya,Ujenzi waweze kujiajiri na baada ya miaka mi3 hivi aanze kurejesha.

Fedha hizi zitoke central Government.
 
Serikali iachane na kujihusisha moja kwa moja kwenye shughuri za miradi ya ujenzi,

Bali iziachie sekta binafsi (private companies) zifanyie kazi hizi by 100%, Serikali ibaki jukumu la kusimamia tu kuhakikisha miradi inajengwa kwa viwango Kama ilivyokuwa hapo awali before awamu ya 5.

Hiyo n njia mojawapo ya kuwezesha pesa kuzunguka kwa wananchi, hivyo uchumi wa individuals kuendana na uchumi wa taifa
 
Punguza Kodi kwenye vifaa vya Ujenzi, hasa cement.

Cement ya Kenya, ni rahisi kuliko Tz

Punguza Tozo kwenye biashara, ili watu wengi wajisajili, na wafanye biashara...na watalipa Kodi kama kawaida. Panua wigo wa Kodi, Kwa kuingiza watu wengi.

Ardhi....Watu wa nje wanapewa ardhi bureee, hasa Wachina. Juzi tu Taarifa ya habari, Wachina wanapewa ardhi Eka 2600 .

Eka 2600 ni ardhi kubwa sana, kiwanda gani kinajengwa kwenye Eka 2600. Hata Kwa upanuzi wa baadae hawatafika huko. Baadae wanakuja kuuza hiyo ardhi Kwa wengine.

Watanzania hasa vijana, nao wapewe ardhi ili wajiajiri. Tunaabudu Wageni.

Mtu akienda Kenya,China au South Africa utapewa ardhi bure?
 
Hapo unapotaja kilimo tu huku mbolea kilo Moja 3500 mpk 4000 hv kweli hapo ni kukwamua wananchi kweli? .

Bora hata nianze na kulalama kwa Jambo liko wazi kabisa kuliko kutoa ushauri ambao hata mfumo uliopo ni wa maamuzi ya mtu mmoja.
 
Punguza Kodi kwenye vifaa vya Ujenzi, hasa cement....

Cement ya Kenya, ni rahisi kuliko Tz..
Nakubaliana nawe kwa asilimia 100 ila pamoja nahayo serikali iwekeze katika miradi mikubwa ya ujenzi wa makazi na kuwakopesha Wananchi kwa Bei na riba ambazo ziko reasonable na kuwekeza ipasavyo katika kuboresha huduma za jamii zimfikie kila mwananchi vinginevyo tutaimba uchumi wa kati na GDP inayokuwa huku umaskini umetamalaki
 
Kufufua viwanda vilivyokufa na kuwalipa wazabuni, suppliers madeni yao.
 
Ili fedha iwe na thamani, lazima iwe hadimu. Ili kundi kubwa la watu liongeze kipato, kuna uwezekano wa kundi lingine la watu kutumia fedha hizo. Nafikiri kuna umuhimu wa kufahamu zaidi kuhusu mzunguko wa fedha na jinsi ya kutatua tatizo la income inequality. Yaani tofauti kubwa iliyopo kati ya walio na kipato kikubwa na walio na kipato kidogo
 
Wanabodi,

Takwimu mbalimbali zinaonyesha jinsi ambavyo uchumi wa Tanzania umekuwa ukibadilika.

Ingawa njia hii inaweza isielezee kwa uhalisia kinachojiri kwenye nchi tofauti, GDP bado ina angaliwa sana kwenye masuala haya ya uchumi.

Kwa Tanzania, GDP imekuwa ikiongezeka kwa asilimia fulani kila mwaka lakini kwa bahati mbaya mafinikio haya ya serikali hayaja onekana sana kwa wananchi.

Je, kuna njia zipi zinazoweza kutumiwa kuhakikisha kwamba matunda ya kazi nzuri inayofanywa na serikali yanawafikia wananchi?.

Endapo Tanzania ikiweza kuwa nchi ya kipato cha juu, tutegemee kitu kipi cha ziada kinachoweza kumkwamua mwananchi mwenye kipato cha chini mpaka awe na kipato cha juu?

Je, kujikwamua kiuchumi kuna maanisha kutumia nguvu zako mwenyewe?

Je, kugawa fedha moja kwa moja kwa wananchi kunaweza kusababisha madhara yapi?

Labda kuwa wezesha wananchi kujiajiri wenyewe, labda kuboresha kilimo.

Nini maoni yako?
Serikali iweke na ihakikishe mazingira Wezeshi na Rafiki kwa wale wanaotaka kuthubutu kujaribu(Entrepreneurs) kwa kuanzisha miradi midogo-midogo (Hata mikubwa) ngazi ya mtu Mmoja, Familia au vikundi.
Hapa nakusudia kusema 1. Serikali iache/isitishe kutoza vijikodi-mshenzi e.g. mama muuza vitumbua eti naye alipe kodi! Bodaboda naye eti lazima alipe EWURA, mchoma mkaa naye alipe TFC, Unatuma ada kwa mwanafunzi bado unatozwa kodi as if unapata chochote kwa kufanya hivyo, n.k. i.e wanaochacharika ngazi ya grassroot level wasibughudhiwe kwa kodi kero.(Hili linawezekana kwani kipindi cha Uchaguzi kodi-kero nyingi ziliondolewa). Serikali kwa kweli ingejifunza kwa waendesha huduma ya vyoo vya kulipia. Ukiingia chooni unatoa fedha na ukimaliza haja yako unamwona mhudumu anakwenda kufanya usafi. Je, wewe Serikali tumeshakupa kodi, basi Sasa wajibika kutoa Huduma na sio tozo ndani ya huduma ambayo tayari ulishalipwa.Ni sawa na yule mwenye huduma ya choo akuambie nunua maji baada ya kumaliza shughuli yako mle ndani.
2. Huduma zitolewazo kwa kutumia kodi zetu zisitozwe tena. Haiingii akilini kwamba kwa mfano; Serikali inanitoza kodi ili iweze kununua madawa ya Hospitali na kulipa mishahara ya wahudumu. Lakini halafu tena Serikali hiyo-hiyo inasema huduma sio bure. Yaani ukihesabu kodi(Tozo) anazolipa mtu mmoja kwa siku moja ni nyingi mno na Serikali inakuwa kama mbabe fulani hv. haisikii wala haijigusi - imekaza shingo tu mbele kwa mbele na Tozo mpaka watoto wanatozwa kodi e.g. mtoto akiweka vocha ya 500/= (wenyewe wanaita Jero) kwenye simu anatozwa kodi.
3. Serikali iache kukumbatia utoaji wa huduma ambazo zingeweza kutolewa na Sekta binafsi. e.g. Huduma za maji, Usafi mijini n.k. kwa kifupi Serikali iwajibike kwa mambo muhimu zaidi kama Ulinzi/Majeshi n.k.
Asante .. Ni maoni au mtazamo wangu tu.
 
Serikali iachane na kujihusisha moja kwa moja kwenye shughuri za miradi ya ujenzi,

Bali iziachie sekta binafsi (private companies) zifanyie kazi hizi by 100%, Serikali ibaki jukumu la kusimamia tu kuhakikisha miradi inajengwa kwa viwango Kama ilivyokuwa hapo awali before awamu ya 5.

Hiyo n njia mojawapo ya kuwezesha pesa kuzunguka kwa wananchi, hivyo uchumi wa individuals kuendana na uchumi wa taifa
Kwa muundo huo una maanisha kwamba kampuni hizi binafsi zilipwe na serikali baada ya kukamilisha shughuli zake za ujenzi. Sidhani kama mabadiliko haya yanaweza kuwagusa watanzania walio wengi hata kama mzunguko wa fedha unaweza kuongezeka. Labda kuna sababu za msingi zinazo ilazimu serikali kuhakikisha kwamba shughuli hizi za ujenzi zinafanywa na serikali yenyewe
 
Uchumi ni swala zito sana,,, linapaswa kuangaliwa kwa jicho kubwa sana...

Namna ya kuongeza na kupunguza mzunguko wa fedha tunafeli sana hapo.... Jinsi tunavotumia hela za mikopo na jinsi serikali inavoendesha taasisi zake kwa hasara na bado wanazichekeachekea...

Nadhani taasisi za serikali zingeanza kujiendesha zenyewe,, mf TTCL, ATCL na zingine zote zinazohusika na uzalishaji... Na walipe serikalini kama kawaida chini ya usimamizi....
 
Sherikali

Hii nchi haina ubunifu wa miundombinu

Serikali haitengenezi fursa kwa wananchi wake "utasikia hatuwezi kuajiri kila mwaka"

Hii yote inasababishwa ukosefu wa miundombinu kuajiri skilled na unskilled

Serikali itengeneze miundombinu sio propaganda ili watu waajiriwe na kujiajiri
 
Kwa muundo huo una maanisha kwamba kampuni hizi binafsi zilipwe na serikali baada ya kukamilisha shughuli zake za ujenzi. Sidhani kama mabadiliko haya yanaweza kuwagusa watanzania walio wengi hata kama mzunguko wa fedha unaweza kuongezeka. Labda kuna sababu za msingi zinazo ilazimu serikali kuhakikisha kwamba shughuli hizi za ujenzi zinafanywa na serikali yenyewe
Serikali haina uwezo kutoa ajira kwa watu wake, Private zikipewa kazi za miradi ya ujenzi Ina maana zitakuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa watu wa kada mbalimbali hivyo kuwapa kipato. Kwa maana hiyo mzunguko wa fedha itakuwa umekamilika maana hata hao wafanyakazi wa makampuni binafsi wataweza kununua bidhaa kutoka kwa wajasiliamali wenye Biashara zao ndogondogo. Nadhani Sasa umenielewa.
 
Back
Top Bottom