Mshana siku za nyuma nikiwa nimelala usiku niliota mtu mwanaume ananiamsha usingizini akitaka nimfate nimsindikize mahali yaani ni kama hiyo sehemu anayoenda kuna jambo lake anataka akafanye basi kweli tukatoka lakin kimuujiiza nikashangaa tumeshafika Eneo la tukio lakini hilo eneo tuliofika muhusika alikua ni sheikh maana alikua akiishi Kando ya msikiti nakumbuka huu msikiti niliuona wakati nimesimama pembeni ya nyumba huku huyo alionitoa nimsindikize akiwa ameshika moto mkubwa mkononi akiwa anaizunguka ile nyumba ya yule sheikh akiwa anamwaga dawa na kunuia vitu.
Ghafla pale niliposimama nikamuona yule sheikh ameamka anakuja ile upande tuliopo Kwa kasi akiuliza nyie ni wa kina nani? Nikaanza kupiga kelele natetemeka naogopa ghafla yule baba niliekua nae akapotea nikabaki mwenyewe eneo la tukio nilivyoona yule sheikh ametaka kunikaribia akili ikanituma kimbia utaambiwa mchawi kweli nikaanza kukimbia lakin speed ya sheikh ilikua kubwa nikajikuta naomba Mungu huku nimesimama nimempa yule sheikh mgongo alipofika akanishika bega nikageuka ghafla sura yangu ikabadilika ikawa Ngumu kama jiwe yule sheikh akaniangalia usoni akashindwa kunitambua akaniachia nikaondoka niliondoka na ile sura ngumu kama jiwe.
Asubuh nashtuka naamka najiona tofauti naiona sura yangu inabadilika kutoka hali ya ugumu ya usiku kuja kwenye sura yangu ya kibinadamu ya kawaida.
Hii ilikua ni ndoto ama tukio halisi na ilikua na maana gani