Mimi huwa nikiota jambo linatokea baada ya muda au mfano wake.
Nilipokuwa mdogo darasa la 3 niliota mtu wangu wa Karibu sana amefariki na hata rangi ya shuka niliyoiota ndiyo hiyo hiyo aliyofunikwa siku yake ya mwisho (Mwaka mmoja baadae).
Pia nilipokuwa mdogo sana miezi michache kabla ya bibi yangu kufariki (Ni mtu mwingine tofauti na wajuu) aliniita akaniiomba nimuandikie Wosia wake, Bibi yangu alikuwa anawajukuu wengine na watoto wakubwa sana ila alisafiri ili mimi tu ndio nimsaidie. (Siku ya Msiba wazee walinipa Heshima sijawahi kupewa).
Kuna ndugu yangu aliniibia Kisimu changu(Kibovu) wakati niko mdogo, siku hiyo nilikasirika sana sana, ila baada ya hapo huyu mtu hajawahi kufanikiwa hata akifanikiwa ataaishia kuiba na kufukuzwa kazi hadi leo hii.
Ndoto yangu ninayoikumbuka vyema kabisa kuliko zote (Niliota darasa la pili) ni harusi niliyoota na binti mzuri sana Mwuepe mwenye kupendeza
😀😀
Naomba kuuliza swali,
Ndugu
Mshana Jr je mtu unaweza ukawa unaweza kufanya ndoto zako kuwa kweli bila wewe kujua au kwa kujua