Uchaguzi 2020 Tofauti ya Edward Lowassa wa 2015 na Tundu Lissu wa 2020

Uchaguzi 2020 Tofauti ya Edward Lowassa wa 2015 na Tundu Lissu wa 2020

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Lissu na Lowassa ki utendaji, ki maadili, ki makuzi na ki umri ni watu wawili tofauti kabisa, Lowassa ana uwezo wa ukwasi Lissu ana uwezo wa akili 'genius'.

Lissu ni mwongeaji sio muoga, hana ukwasi lkn hana bei, anajiamini hasa eneo lake la kujidai la sheria tofauti na Lowassa, hivyo ana nafasi nzuri ya kum challenge na kumhoji mgombea wa CCM rais Magufuli kuliko Lowassa.

Lowassa ni mpole, mtu mzima, siyo mwongeaji kama Lissu yuko compromised, wakati wa kampeni alikuwa hawezi kusimama na kujieleza hata kwa dakika 15.

Lissu wakati anajieleza mbele ya wajumbe wa Chadema, alisema, yeye si yule wa kusema "Tunamwachia Mungu", aliongeza kusema akiibiwa kura yuko tayari kuwaingiza wananchi barabarani. Lowassa alikuwa muoga hata kutamka neno la kumuuzi mpinzani wake wala kumjibu msajili wa vyama.

Baada tu ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA, kasema kitendo cha rais kupewa jogoo na kutoa laki moja kwa mpiga kura ni rushwa hivyo ataweka pingamizi kwa mgombea wa CCM. Hii ndiyo sura halisi ya yule anayekwenda kupambana mgombea wa CCM ambaye vyombo vyote vya dola viko chini yake.

Mwisho kabisa Lissu ana damu ya uanaharakati upinzani wa kuzaliwa tofauti na Lowassa aliyeingia upinzani baada ya kukosa alichotaka ndani ya CCM.

Kuna wakati Kikwete alinukuliwa akisema kuwa, "Ni bora Dr Slaa kuwa raisi kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge".

Tutegemee kampeni ya 'vijembe' hasa ukizingatia wagombea wote rais Magufuli na Lissu kwao neno kushindwa haliko kwenye vocabulary yao.
 
Pia Lissu ni mtu aliyefufuliwa na Mungu kutoka katika wafu ili aje aikomboe Tanzania , baada ya kushambuliwa na watu waoga walioshindwa siasa za hoja

Tundu Lissu atarejea Tanzania - Kupitia uwanja wa ndege wa Dar siku ya Jumatatu  ( 800 X 640 ).jpg
 
Ngoja nisubiri analysis za baada ya uchaguzi maana ndo huwa real,hizi za kabla huwa mzuka na mahaba zaidi.
HAPO UMENENA!
 
Kabla ya uchaguzi tayari Tundu Lisu ana 50% ya kura za Watanzania waliojiandikisha. Kimsingi Tundu Lissu ni Rais Mteule anayesubiri kuapishwa. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayempa kura Magufuli. Ameua uchumi na ameua binadamu
 
Kabla ya uchaguzi tayari Tundu Lisu ana 50% ya kura za Watanzania waliojiandikisha. Kimsingi Tundu Lissu ni Rais Mteule anayesubiri kuapishwa. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayempa kura Magufuli. Ameua uchumi na ameua binadamu
Uko sahihi kabla ya 2015 watu walikuwa hawayajui makucha ya Magufuli sasa wanayajua si wafanyakazi si wafanyabiashara si wakulima si wanafunzi.
 
Wananchi wa Tanzania hawawapendi wanaharakati. Watu wanaoongea huku mishipa yao ya shingo ikiwa imekakamaa.
Hao waliompa kura 405 kwenye kamati kuu ya Chadema na wale maelfu waliojitokeza kumlaki pale airport ni wananchi wa nchi gani mama?
 
..Lissu angekuwa ni bondia basi style yake ingekuwa ni " switch hitter ."

..Yaani ni bondia anayeweza kupigana kwa mtindo wa "orthordox" na mtindo wa "southpaw."

..Orthordox ni bondia anayepigana kwa kutanguliza mkono wa kulia, na southpaw ni kushoto.

..kwa kawaida mabondia huwa ni orthodox au southpaw, ni nadra bondia kuweza kupigana kwa staili mchanganyiko.

..Lissu anaweza siasa za hoja, na ni mzuri pia ktk siasa za vijembe.
 
Acha uongo mchana kweupe ... Watanzania hao hao unaowazungumzia hapa sindio hao hao walio kwenda kumpokea lissu AIRPORT alipokuwa anarudi toka Belgium !??
Hamna hiyo mi misukule ya CHADEMA
 
Back
Top Bottom