Uchaguzi 2020 Tofauti ya Edward Lowassa wa 2015 na Tundu Lissu wa 2020

Ngoja nisubiri analysis za baada ya uchaguzi maana ndo huwa real,hizi za kabla huwa mzuka na mahaba zaidi.
HAPO UMENENA!

Uko sawa kabisa, lakini upo uwezekano na hata ukisema leo, walio amini hawawezi kukubali maneno mazuri utakayo toa.
 
Acha uongo mchana kweupe ... Watanzania hao hao unaowazungumzia hapa sindio hao hao walio kwenda kumpokea lissu AIRPORT alipokuwa anarudi toka Belgium !??
Waliokwenda airport walikuwa wahuni na mateja bila kusahau walevi wa gongo na konyagi. Watanzania wazalendo tulikuwa msibani.
 
Waliokwenda airport walikuwa wahuni na mateja bila kusahau walevi wa gongo na konyagi. Watanzania wazalendo tulikuwa msibani.
Hahaa ukiishiwa hoja bwana lazima uongee viroja ... Kwa hiyo katiba ya nchi inasema kuwa mateja na walevi wagongo sio watanzania !??
 
Lisu ni muongo muongo sana kama walivyo viongozi wengine wa Chadema, ktk ile list ya mafisadi waliyokuwa wanasimama nayo majukwaani lakini akalamba matapishi yake kumpokea mmoja wa " mafisadi" wale na kuanza kumnadi kwenye majukwaa ya kampeni 2015. Mleta mada nae ni mmoja ya waliodeki barabara kipindi kile leo anamtoa kasoro Yule Mzee punguzeni kigegeu na muwe na akiba ya maneno.
 
Okay nimekuelewa ila totauti kubwa Kati ya Lowassa vs Lisu....ni kwamba Lowassa aliwapatia wabunge wengi....je Lisu ataweza au vijembe zaidi ndyo tuvitegemeee,

Vipi Dr slaa vs Lisu...who was/is potential
 
Mtanzania pekee aliyeweza kuiamsha Tanzania kutoka kwenye nusu-kaputi ya kisiasa!
Sikutegemea kuona siasa ya Tanzania inaweza kuchangamka ndani ya usiku mmoja tu.
Mchukie au Mpende lazima ukubali kwamba Tundu Lissu ana kitu cha pekee.
+1
sikutegemea kabisa kama ningekuja shabikia siasa tena , upinzani ulionekana kama umekufa ,
then ghafla bin vuu,tupo alive tena!!!
 
kwa tulipofikia hata kama hana sera za maendeleo wenye busara watamchagua , tunahitaji zaidi democracy kuliko maendeleo yenye ukakasi
 
+1
sikutegemea kabisa kama ningekuja shabikia siasa tena , upinzani ulionekana kama umekufa ,
then ghafla bin vuu,tupo alive tena!!!
Mkuu unamaanisha nini unaposema kushabikia siasa ???
Hili ni suala la uhai wa taifa, tusilifanye dogo kabisa.
Lazima kila mzalendo ajitoe kunusuru taifa letu.
 
Mkuu unamaanisha nini unaposema kushabikia siasa ???
Hili ni suala la uhai wa taifa, tusilifanye dogo kabisa.
Lazima kila mzalendo ajitoe kunusuru taifa letu.
Ninakukubali sana ML
 
Mkuu unamaanisha nini unaposema kushabikia siasa ???
Hili ni suala la uhai wa taifa, tusilifanye dogo kabisa.
Lazima kila mzalendo ajitoe kunusuru taifa letu.
haha nimetumia kiswahili cha mtaa naelewa siasa ndo kila kitu , ila nilishakata tamaa kuifatilia, hasa kipindi kile cha wimbi la kuunga juhudi kwa madiwani na wabunge ,
, On serious note, wajumbe nao wamenifurahisha walivowatema waunga juhudi
 
Lissu kumshindanisha na jpm kwenye mdahalo in kutomtakia mema jpm, lissu ni motoooo
 
Bahati mbaya mko wengi humu JF tu
 
Lissu Ni moto wa gesi haupoi hapa ni chakula kiive au kiungu mpishi lazima kuwa makini akisinzi amekwisha
 
Suala la jaribio hilo linalozungumziwa kwa mtazamo wangu ni gumu sana kutokea Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…