Ramsy Dalai Lama
Senior Member
- Apr 5, 2021
- 156
- 554
Unajua nini!, bado pesa ipo nyingi katika nchi yetu hata kama imekuwa ngumu kiasi gani lakin ukweli ipo. Pesa ipo kila sehemu, Serikali ina pesa, benki zina pesa, makampuni yana pesa,migahawa na mpaka mama ntilie wana pesa hata kama ni ndogo, wauza biashara ndogo ndogo mpaka wenye biashara kubwa wana pesa
Wewe una pesa hata kama ni shilling 50, marafiki zako wana pesa! Matajiri wana pesa, masikini wana pesa! asikudanganye mtu kwamba pesa hakuna kabisa, ipo na kila wakati inazunguka masaa 24 kwa siku - kila siku 365 kwa mwaka! Lakin Je! Unawezaje kuzipata hizo pesa? hata kwa yule mwenye buku tu au hata shilling 50 yake.
Nikuambie kitu?, tofauti ya watu wa hali ya chini na matajiri ni katika JINSI 'wanavyoingiza' pesa. Watu maskini wanafanya kazi kwa bidii kwa huwekeza muda kwa kufanya kazi sehemu ili walipwe pesa au kufanya biashara ndogo yoyote ili tu wapate pesa.
Wakati watu matajiri, wanaofanya kazi kwa bidii waliwekeza katika kujenga na kuikuza biashara ambayo "itaingiza" pesa kwao kwa wingi na kwa muda mrefu. Labda nitoe mfano rahisi, buibui hawawezi kufanya kazi ngumu kufukuza wadudu wanaoruka kupata chakula Badala yake, atafanya kazi ngumu kujenga wavu wa buibui (SPIDERWEB) ambao utawapatia wadudu wengi wanaoruka hivyo watapata chakula chenye uhakika kwa muda mrefu pasipo kufanya kazi ya kukimbizana na wadudu (Pesa) kila siku.
Hiyo inaitwa uwekezaji katika kujenga biashara itakayo kuingizia pesa ambayo Inafanya kazi masaa 24 ama 12 kwa siku, siku 7 kwa wiki, kukamata "pesa" ya kuruka - hata wakati buibui umelala. Hiyo ndiyo siri. Shule hazitakuambia hivi.
Watakufundisha kufuata pesa, ambayo inasababisha fomula ya malipo: (Shahada ya Chuo) x (Muda) halafu mshahara Onyo: Huo ni mtego wa kutumia nguvu! Kuna suluhisho moja tu: Ujasiriamali.
Please Acha kutoa visingizio na anza kujenga "SPIDERWEB" yako leo!