The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Kabla jua halijazama utaitwa motivational speaker!
Amini amini nakwambia...
Hapo hajaongelea buibui anajenga hiyo wavu wake wapi? Anawezajenga amekaribia kumaliza unakuja upepo, watu wanafanya usafi, amepita mnyama/ binadam kwa bahati mbaya mtego ukavurugika.
Anaweza kukamilisha mtego akapita hapo mdudu mkubwa akaondoka na wavu/ mtego.
Pia huo mtego utanasa wale wadudu watakaopita kwenye hilo eneo pekee, akiweka mtego sehem isiyorafiki atafanya kazi ngumu ya kuweka mtego na atalala njaa kila siku.
Kuna mambo mengi sana ya kuangalia hapo. Kimsingi kila mmoja wetu kama sio wote tunatamani au tunaitafuta pesa. Wanaopatia kanuni zake ndio hao wanatupiga gap, awe amesoma au hajasoma ila atatoboa tu srma juhudi zinatofautiana.
Yote kwa yote, ujumbe umefika na kila mmoja ataondoka na idea ya mtazamo mpya wa ulimbo mujarab kuinasa pesa.