Tofauti ya kuingiza pesa kati ya tajiri na masikini

Tofauti ya kuingiza pesa kati ya tajiri na masikini

Kabla jua halijazama utaitwa motivational speaker!

Amini amini nakwambia...
Hapo hajaongelea buibui anajenga hiyo wavu wake wapi? Anawezajenga amekaribia kumaliza unakuja upepo, watu wanafanya usafi, amepita mnyama/ binadam kwa bahati mbaya mtego ukavurugika.

Anaweza kukamilisha mtego akapita hapo mdudu mkubwa akaondoka na wavu/ mtego.

Pia huo mtego utanasa wale wadudu watakaopita kwenye hilo eneo pekee, akiweka mtego sehem isiyorafiki atafanya kazi ngumu ya kuweka mtego na atalala njaa kila siku.

Kuna mambo mengi sana ya kuangalia hapo. Kimsingi kila mmoja wetu kama sio wote tunatamani au tunaitafuta pesa. Wanaopatia kanuni zake ndio hao wanatupiga gap, awe amesoma au hajasoma ila atatoboa tu srma juhudi zinatofautiana.

Yote kwa yote, ujumbe umefika na kila mmoja ataondoka na idea ya mtazamo mpya wa ulimbo mujarab kuinasa pesa.
 
Pia ifike mahala kuingiza milioni 1 kwa siku ionekane ni kitu cha kawaida, iruhusu akili yako ikubali kwamba hilo linawezekana bila ukakasi, huwa nashangaa nikiwaambia watu kuwa mil.1 ni pesa ya kuingiza kwa siku huwa wanashtuka mno, nadhani ni tatizo la kisaikolojia zaidi
Mkuu wewe una biashara gani inayokuingizia M1 kwa siku? Na hayo ni mauzo au ndo faida? Na hiyo ni faida baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji? Je umeajiri au unafanya mwenyewe?
 
Huyo wa milioni moja kwa siku unajua anatakiwa awe na mtaji kiasi gani...
Mtaji usio chini ya 5m ...ndio aipate hyo profit
 
Kwenye mzunguko pesa ipo... Ila hakikisha na wewe unakua sehemu ya hio system pesa inako pitia

Akili inayohitajika ndio hapo kwenye "...hakikisha na wewe unakua sehemu ya hiyo system..."

Ukishaliweza hilo, haijalishi umesoma, umetokea familia masikini, au hali yako ikoje, lazima unufaike na mtiririko wa pesa.
 
Mkuu wewe una biashara gani inayokuingizia M1 kwa siku? Na hayo ni mauzo au ndo faida? Na hiyo ni faida baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji? Je umeajiri au unafanya mwenyewe?
Hahahah, vipi kwani 🤣🤣🤣🤣
 
Spider web unaijengaje bila pesa kwa mfano!!!??

Uwekezaji unahitaji mtaji. Ninani asiyetaka kuwa kuwa na spider web!!....
Tuanzie hapo.
Use what you have to get what you want! Simple like that, spider wed = sound mind.
 
Spider web unaijengaje bila pesa kwa mfano!!!??

Uwekezaji unahitaji mtaji. Ninani asiyetaka kuwa kuwa na spider web!!....
Tuanzie hapo.
Sikia kiongozi, inawezekana kabisa sio kila biashara kuanzisha inahitaji mtaji. Zipo unaweza aanzisha pasipo mtaji au inahitaji mtaji mdogo sana. Lakini pili kama inahitaji mtaji na huna basi unaweza kuajiliwa kwanza Kisha kusanya mtaji Kisha anzisha biashara yako
 
Gitaa umecharaza vizuri sasa solo bado hajaweka maneno. Umesema vyema tu ila hujaweka utekelezaji (execution) ambayo hiyo ndiyo kila kitu. Maana wapo wenye taarifa sahihi, wapo waliofanya maamuzi, lakini hapo kwenye utekelezaji ndio kila kitu.
 
Mkuu hakuna suluhisho moja tu kwa kila kitu. Kuna watu kazi inawafaa zaidi, wengine huduma, wengine biashara, wengine udalali , hakuna kinachomfaa kila mtu na hakuna suluhisho moja tu kwa kila mtu.
 
Back
Top Bottom