Tofauti ya kuingiza pesa kati ya tajiri na masikini

Unajua nini!, bado pesa ipo nyingi katika nchi yetu hata kama imekua ngumu kiasi gani lakin ukweli ipo. Pesa ipo kila sehemu, Serikali ina pesa, benki zina pesa, makampuni yana pesa,migahawa na mpaka mama ntilie wana pesa hata kama ni ndogo, wauza biashara ndogo ndogo mpaka wenye biashara kubwa wana pesa…Wewe una pesa hata kama ni shilling 50, marafiki zako wana pesa! Matajiri wana pesa, masikini wana pesa! asikudanganye mtu kwamba pesa hakuna kabisa, ipo na kila wakati inazunguka masaa 24 kwa siku - kila siku 365 kwa mwaka! Lakin Je! Unawezaje kuzipata hizo pesa? hata kwa yule mwenye buku tu au hata shilling 50 yake.
Nikuambie kitu?, tofauti ya watu wa hali ya chini na matajiri ni katika JINSI 'wanavyoingiza' pesa. Watu maskini wanafanya kazi kwa bidii kwa huwekeza muda kwa kufanya kazi sehemu ili walipwe pesa au kufanya biashara ndogo yoyote ili tu wapate pesa. Wakati watu matajiri, wanaofanya kazi kwa bidii waliwekeza katika kujenga na kuikuza biashara ambayo "itaingiza" pesa kwao kwa wingi na kwa muda mrefu. Labda nitoe mfano rahisi, buibui hawawezi kufanya kazi ngumu kufukuza wadudu wanaoruka kupata chakula Badala yake, atafanya kazi ngumu kujenga wavu wa buibui (SPIDERWEB) ambao utawapatia wadudu wengi wanaoruka hivyo watapata chakula chenye uhakika kwa muda mrefu pasipo kufanya kazi ya kukimbizana na wadudu (Pesa) kila siku. Hiyo inaitwa uwekezaji katika kujenga biashara itakayo kuingizia pesa ambayo Inafanya kazi masaa 24 ama 12 kwa siku, siku 7 kwa wiki, kukamata "pesa" ya kuruka - hata wakati buibui umelala. Hiyo ndiyo siri. Shule hazitakuambia hivi. Watakufundisha kufuata pesa, ambayo inasababisha fomula ya malipo: (Shahada ya Chuo) x (Muda) halafu mshahara Onyo: Huo ni mtego wa kutumia nguvu! Kuna suluhisho moja tu: Ujasiriamali.. Please Acha kutoa visingizio na anza kujenga "SPIDERWEB" yako leo!
Huu ni uzi bora kwa mwaka 2021.
 
Pia ifike mahala kuingiza milioni 1 kwa siku ionekane ni kitu cha kawaida, iruhusu akili yako ikubali kwamba hilo linawezekana bila ukakasi, huwa nashangaa nikiwaambia watu kuwa mil.1 ni pesa ya kuingiza kwa siku huwa wanashtuka mno, nadhani ni tatizo la kisaikolojia zaidi
 
Spider web unaijengaje bila pesa kwa mfano!!!??

Uwekezaji unahitaji mtaji. Ninani asiyetaka kuwa kuwa na spider web!!....
Tuanzie hapo.
Mtaji wako ni ubongo wako, usidanganyike na kingine chochote, labda uwe taahira ndio tutasema huna mtaji. Au kama unataka kuwa masikini ndio tutasema mtaji wako ni nguvu zako mwenyewe. Ila nikupe hint ya mafiga matatu ya utajiri katika kizazi hiki cha sasa. 1.) IG 2.) FB 3.) WSAP
 
FACT jenga kwanza mitego yako wala hutahangaika na CV mkononi kutafuta kuajiriwa serikalini ambako tija yake haipo, walioshtuka wamejiajiri na wanapiga mishe zao kama kawaida bila bugudha, wanaosubiri kuajiriwa na teuzi ndio wabishiiii, hata wakipewa madini ya namna gani hawakubali kwakua akili zao zimeganda, huwezi kuishi kwa kutegemea ajira ambazo hazipo na hata kama zipo Niambie Mfanyakazi wa Serikali ambaye ni Bilionea yuko wapi hata kama alikua mwiziiiiiii
 
Pia ifike mahala kuingiza milioni 1 kwa siku ionekane ni kitu cha kawaida, iruhusu akili yako ikubali kwamba hilo linawezekana bila ukakasi, huwa nashangaa nikiwaambia watu kuwa mil.1 ni pesa ya kuingiza kwa siku huwa wanashtuka mno, nadhani ni tatizo la kisaikolojia zaidi
Forex sio
 
FACT jenga kwanza mitego yako wala hutahangaika na CV mkononi kutafuta kuajiriwa serikalini ambako tija yake haipo, walioshtuka wamejiajiri na wanapiga mishe zao kama kawaida bila bugudha, wanaosubiri kuajiriwa na teuzi ndio wabishiiii, hata wakipewa madini ya namna gani hawakubali kwakua akili zao zimeganda, huwezi kuishi kwa kutegemea ajira ambazo hazipo na hata kama zipo Niambie Mfanyakazi wa Serikali ambaye ni Bilionea yuko wapi hata kama alikua mwiziiiiiii
Kila mtu akijiajiri nani atanunua bidhaa au huduma kwa mwenziwe!?
 
Ndiyo yeye!! Muambie akuonyeshe spider web yake kama hajazama uvunguni,hata hivyo ana vimaneno vitamu,atakuwa alifuzu vizuri ile kozi wanayopewaga ya kusaundisha malofa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] we jamaa shenzi sana.
 
Kutengeneza mfumo wa kupata pesa ni ngumu,ni njia inayohitaji uvumilivu sana,ni njia ambayo haileti majibu leo,au kesho..inaleta majibu baadae sana lakini iki'tick' ni njia ya uhakika sana na yenye kuhakikisha ukuaji wa mifumo yetu kwa asilimia kubwa.

Wengi tutapinga kwa kuwa tunapenda kuyafanya yale tuliyoshindwa kuwa uhalisia wa kila mtu, labda ili tujifariji na kuepuka maumivu ya kufikiri wapi na namna gani tulikosea tusirudie yale tuliyokosea.Maumivu yatokanayo na kutofikiwa kwa mategemeo makubwa sana tunayotengeneza vichwani mwetu tunapoanza biashara zetu,tukisahau kuwa tunayotegemea na uhalisia ni vitu viwili tofauti au labda mategemeo yangehitaji muda zaidi na juhudi nyingi,ubunifu mwingi au nidhamu kubwa ili kuyafikia.

Lakini haitoweza kupingika kuwa vitu vingi au watu wengi waliofanikiwa wana mifumo imara nyuma yao..iwe kibiashara,kimahusiano,kifamilia au kivyovyote vile.

Tunaposhindwa kufanikisha jambo,kuna wngine wanafikiwa kulifanya vizur.

Au labda nami ni 'motivesheni speaker '..hahaha.
"..Wengi tutapinga kwakuwa tunapenda kuyafanya yale tuliyoshindwa kuwa uhalisia wa kila mtu.." kesho asbuhi mapema sana niko Benk na hii sentence kuchukua mkopo.
 
Back
Top Bottom