Pre GE2025 Tofauti ya Lissu na Magufuli ni moja: Magufuli hakupenda Vitu vya Msaada (bure), Lissu apunguze kuomba omba kuelekea 2025!

Pre GE2025 Tofauti ya Lissu na Magufuli ni moja: Magufuli hakupenda Vitu vya Msaada (bure), Lissu apunguze kuomba omba kuelekea 2025!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba Tundu Lisu na Shujaa Magufuli wanafanana katika mambo mengi ikiwemo Ujasiri, Kujiamini, Ubabe, Upendo na One Man Show

Tofauti yao ya Msingi ni Moja tu Kwamba Lisu anapendelea mambo ya kusaidiwa saidiwa hata kwenye kupeleka gari binafsi Gereji lakini Shujaa Magufuli alipenda kujitegemea kwa kila kitu hata Bombardier zilipakwa rangi hapa hapa Nchini

Ili apate kura za kuridhisha 2025 Tundu Lisu aachane na mambo ya kupitisha bakuli

Samahani kwa wale mliokwazika 🐼

Ahsanteni Sana 😂
Kwa hiyo, kwa kusema hivyo unamaanisha kipimo cha Tundu Lissu ni Magufuli?
 
Hoja mfu. Kwani uchapakazi wa Magufuli ulianza baada ya kuwa rais? Kupiga kazi na kupiga porojo ni vitu viwili tofauti.
Kama unasubiri lisu awe rais basi utasubiri sana!
Mkuu, heshima kwako! Huwezi kukamata Meli za uvuvi na mwisho wake unashitakiwa na kusababisha sintofahamu.
 
Mkuu, heshima kwako! Huwezi kukamata Meli za uvuvi na mwisho wake unashitakiwa na kusababisha sintofahamu.
Mkuu, mimi nikikukamata kwa kufanya kosa fulani, nikakupeleka kwa wanaopaswa kukuchukulia hatua, ukawapa cha juu, ukaachiwa na kesi ikaishia hapo; mwenye makosa ni nani? Ni mimi mkamataji, walioachia mwenye makosa aende zake?
Kukamata na kuchukua hatua ni mambo mawili tofauti!
 
Mkuu nani hao waliopewa cha juu? Ulikamata na vielelezo? Au unataka kutuambia kuwa Mahakama zetu hazitendi haki?
 
Mkuu nani hao waliopewa cha juu? Ulikamata na vielelezo? Au unataka kutuambia kuwa Mahakama zetu hazitendi haki?
Unachosema hapa ni kwamba hakuna wanaopiga cha juu hapa nchini?
Unaongea ukiwa umejigicha wapi?
 
Back
Top Bottom