Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Kiongozi lazima uwe honest.Hii ndo tofauti kwa Makocha pamoja na mashabiki wa Simba SC na Yanga SC katika kupokea matokeo uwanjani.
••Simba SC ikifungwa mashabiki wa Simba, wanaona ni hali ya mchezo wanakubali na kwamba mchezo wa mpira una matokeo matatu hivyo wanasonga mbele kwenye mapambano huku wakijipa moyo kuwa mechi ijayo watafanya vizuri kuweza kushinda.
••Yanga SC ikifungwa mashabiki wao wanaanza kuijia juu TFF kuwa inawahujumu na wala hawana muda wa kuwapa moyo wachezaji wao.
••Simba SC ikifungwa, Kocha Patrick Aussems anatoa sababu za kiufundi kwanini wamepoteza mchezo huo na kuahidi kufanyia kazi makosa.
••Yanga SC ikifungwa Kocha wao Mwinyi Zahera anaijia juu TFF, Simba na Waamuzi kuwa wanamhujumu asiwe bingwa wa TPL na hana muda wa kueleza matatizo ya timu yake kiujumla.
••Simba SC hata ifungwe, mashabiki wao wanaenda uwanjani kuipa support klabu, kwa maana wanajua Soka linataka nini na wanajua mpira pia.
••Yanga SC ikifungwa hawaendi uwanjani wanajazana kwenye vijiwe vya Kahawa huku wakisema TFF wale ni Simba na kudanganyana kila siku.
••Simba SC ikishinda wanasema Kahonga, mara TFF, mara magoli ya Penati na kulia lia kila wakati yaani full Malalamiko.
••Yanga SC ikishinda wanafurahi mno huku wakisema hakuna kama Yanga ilhali walipewa ubingwa mara tatu lakini hata Robo Fainali Hawakufika.
Mashabiki wengi wa Yanga hawana uelewa na masuala ya mpira ni vile wapo tu na wao waonekane..Lipi ambalo litainusuru hii klabu ya Yanga na Kocha wao kwa sasa..!View attachment 1077422
Inakopita Yanga sasa hivi, ndiko ilikopitia Simba wakati Manji akiwika Yanga. Hilo unalijua kabisa.
Umesahau malalamiko ya Haji hadi kuweka Video clips kwa wandishi wa habari?