Tofauti ya Smart Tv na Android TV ni ipi?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza. Nahitaji wataalam wanisaidie please. Kwa sasa nina Smart Tv hii ipo Sebuleni.

Nahitaji kununua Tv nyingine kwa ajili ya Chumbani. Angalau nipate 60" plus. But the question is je ninunue tena Smart Tv au sasa ninunue Android TV.

Je ipi ni bora katika hizo na kwa sababu zipi? Nashukuruni. Wahenga walisema wewe ukijua ya Nyuma wenzako wanajua ya mbele.
 
Android ni Smart Tv, ila Smart TV haina Android

Andoid kama ilivo kwenye simu, unaweza kuupdate mambo mbalimbali kwenye tv, kwa Smart Tv ni ngumu kuupgrade.

Android unapata apps nyingi sana kwenye smart hazipo nyingi.

Asante
 
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza. Nahitaji wataalam wanisaidie please. Kwa sasa nina Smart Tv hii ipo Sebuleni.

Nahitaji kununua Tv nyingine kwa ajili ya Chumbani. Angalau nipate 60" plus. But the question is je ninunue tena Smart Tv au sasa ninunue Android TV.

Je ipi ni bora katika hizo na kwa sababu zipi? Nashukuruni. Wahenga walisema wewe ukijua ya Nyuma wenzako wanajua ya mbele.
Kwnye kununua hapo zingatia ukubwa wa chumba na ukubwa wa tv...Ili kuepusha athari kwenye macho
 
Raia wa jf bhana eti inch 60 plus kwaajili ya chumban sa sebulen umeweka inch ngp? Humu kila mtu anazo, ana gari nk ukute uyu jamaa hana mbele wa nyuma amepata kahela ka kununulia tv ya arboder au sundar 32 inch analeta sfa humu.
😅😅😅
 
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza. Nahitaji wataalam wanisaidie please. Kwa sasa nina Smart Tv hii ipo Sebuleni.

Nahitaji kununua Tv nyingine kwa ajili ya Chumbani. Angalau nipate 60" plus. But the question is je ninunue tena Smart Tv au sasa ninunue Android TV.

Je ipi ni bora katika hizo na kwa sababu zipi? Nashukuruni. Wahenga walisema wewe ukijua ya Nyuma wenzako wanajua ya mbele.
smart tv ni tv janja zenye uwezo wa kuongeza features kama apps na peripheral nyengine, kuna operating system nyingi za smart tv kama vile android tv, tizen, web os, roku, fire tv, etc.

kama unalipia apps zako kama dstv, netflix, amazon prime basi os yoyote ile ni sawa tu angalia features nyengine, ila kama unatumia apps za kuchakachua basi android tv ina make sense zaidi.
 
choose the right size TV for your living room
 
Attachments

  • images (9).jpeg
    images (9).jpeg
    25 KB · Views: 40
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza. Nahitaji wataalam wanisaidie please. Kwa sasa nina Smart Tv hii ipo Sebuleni.

Nahitaji kununua Tv nyingine kwa ajili ya Chumbani. Angalau nipate 60" plus. But the question is je ninunue tena Smart Tv au sasa ninunue Android TV.

Je ipi ni bora katika hizo na kwa sababu zipi? Nashukuruni. Wahenga walisema wewe ukijua ya Nyuma wenzako wanajua ya mbele.
Smart TV ni jina la jumla, Android TV ni aina moja ya Smart TV yenye operating system ya Android/Google (Gari vs Toyota) .
Cha muhimu ujiulize ni feature gani za hiyo TV unazihitaji na zitakufaa wewe, wengine wanang'ang'ania smart tv wakati hata internet hawana.
 
Raia wa jf bhana eti inch 60 plus kwaajili ya chumban sa sebulen umeweka inch ngp? Humu kila mtu anazo, ana gari nk ukute uyu jamaa hana mbele wa nyuma amepata kahela ka kununulia tv ya arboder au sundar 32 inch analeta sfa humu.
huwa nawachora tu matajiri wa jf
 
Raia wa jf bhana eti inch 60 plus kwaajili ya chumban sa sebulen umeweka inch ngp? Humu kila mtu anazo, ana gari nk ukute uyu jamaa hana mbele wa nyuma amepata kahela ka kununulia tv ya arboder au sundar 32 inch analeta sfa humu.

UTAPATA UGONJWA WA MOYO BURE TU. ROHO YA KIMASKINI INATESA SANA KWA ALIYE NAYO. WEWE ISHI MAISHA YAKO NA ACHA WENGINE WAISHI MAISHA YAO. UNATESEKA UKIWA WAPI?
 
Raia wa jf bhana eti inch 60 plus kwaajili ya chumban sa sebulen umeweka inch ngp? Humu kila mtu anazo, ana gari nk ukute uyu jamaa hana mbele wa nyuma amepata kahela ka kununulia tv ya arboder au sundar 32 inch analeta sfa humu.
Sijaona kosa lake kwa kueleza kile anachoamini au kupenda
Binafsi chumbani kwangu nimekupa kipaumbele kuliko sebuleni, chumban kuna double the size and quality ya vitu nilivyoweka sebulen, na vingine vipo chumbani tu sebulen havipo.
Maisha yenyewe mafupi haya naipenda nafsi yangu kwanza.
 
Smart TV ni jina la jumla, Android TV ni aina moja ya Smart TV yenye operating system ya Android/Google (Gari vs Toyota) .
Cha muhimu ujiulize ni feature gani za hiyo TV unazihitaji na zitakufaa wewe, wengine wanang'ang'ania smart tv wakati hata internet hawana.
Smart Tv mwenzie internet, tena sio capped bundles, inataka unlimited internet yenye speed ya kutosha ku stream 4k videos.
 
Back
Top Bottom