mkuu hiyo hapana bora nichukuehapa hapa ndani maana yapo ya bei hata hiyo tena hata chini sema ni ufume then unakuja fanya service then unapga kazi hilo ni dogo labda kwa mtu wa tela, pia mpaka lifike na ulitoe hapo bandarini bei yake itakuwa si chini ya M 10ndio mzee unachukua hio unajipiga piga nalo ukipata ela kidog unaongeza anaagiza jipya
mkuu hiyo hapana bora nichukuehapa hapa ndani maana yapo ya bei hata hiyo tena hata chini sema ni ufume then unakuja fanya service then unapga kazi hilo ni dogo labda kwa mtu wa tela, pia mpaka lifike na ulitoe hapo bandarini bei yake itakuwa si chini ya M 10
usemalo ni kweli ila hako kadogo sana ka unalenga kazi bora bovu ambalo unalisambaratisha unalivika vifaa vingine vizuri then unazama shamba, tractor huai haifi mkuu ile ni mashine,mchawi ni service kubwa kunajamaa alinunua MF165 kwa M6 amelifufua na hela ambayo si zaidi ya M5tatizo ya hapa nyumban yanakua ni mabovu mkuu
bora hayo ya nje linaweza kua na hali nzul kidogo
Tatizo ni alibaba unaweza kuta ni toyHiyo bei inatosha kununulia jembe la kawaida ila jembe zuri wala hata haiwezi nunua, itakuwa kachanganya mambo tuu
Valmet pia naikumbuka. Tractor za zamani zilikuwa vyuma kweli kweli, siyo za sasahivi batiValmet nzovwe Mbeya kuna mangi mmoja alikua analitembeza km ferarri vile.
Full mikwaju ukiunga vumbi basi mzuka akianza kutafuna gia hapo anaelekea swaya kuchukua mzigo wa mahindi.
Utamnunulia mirinda mwenyeewe
Inabidi uhakikishe unachonunua ndio ulichoagiza kwani dunia ya sasa watu wana akili za ziada hahahaha[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] kwahyo alibaba sio seem salama??
Boramm bhn mambo ya online cyawezii
habar wadau , habari za sikunyingii
hatimae JF yetu imerudiii [emoji28][emoji28][emoji28]
twende kwenye mada wakuu.
binafsi nimekua nina interest kubwa ya kumiliki trector walau 2 tu while nikifanya mishe mishe zangu town naamini ntafika ninapo pata kwa haraka zaid sas shida ni kuusu hizi trector za kichina hivi zina tatizo gan mana ni cheap sana.. unakuta trector ina uzwa us dolla 3500 na trector ni mpya yaan 0 kilometer 4wd hp 85 hapo hapo ukija upande wa pili huku kwa kina john deere trector 4wd hp 85 bei yake hugusii yan ni pesa ndefu ambayo kwa usawa huu wa magu kijana kama mimi kupata hio pesa inakua ni mazoeziii
ombii kwa wataalam tofaut hasa ni ipiii
kwan hizi trector za kichina haina uwezo kwa kulima walau eka 15 per day??
mana izo massey zipo naziona mtandaon had dollar 3500 sas shida ni kweli zinauzwa bei hio mana USA ni mbali na actually siamini hizi mitandaoView attachment 800264View attachment 800265View attachment 800266
izi massey ni bei yke kwel au fixx binafs nilifikilia nikanunue tu trector za kichina mana ni cheap sanaaa
naomben ushauli kabla cjapotea wadau...
Tsh milioni 9 na laki 3tractor mpya pamoja na trailer lake, disc plough na hallow yake(complete) ni being gani
mkuu sina shaka na yote uloandika, unajua pasipo kubahatisha,nimependa uelewa wako mkuu keep it goingMimi nina uzoefu wa matrekta kwa miaka minne sasa. Watanzania wengi ukiwauliza matrekta watakuambia massey ferguson(mf), john deere, ford, fiat na new holland maana ndizo walizozoea kuziona barabarani karibia kila siku.
Trekta karibia zote huwa zinafanya kazi ngumu sikushauri ununue iliyotumika hata kama bado inavutia kwa sura labda tu kama huna uwezo wa kununua mpya. Na kama unanua iliyotumika, ikague sana maana matatizo mengi ya trekta hayapo kwenye matairi au body yake, yapo kwenye mfumo wa hydraulic, fuel pump hasa mambo ya ndani ambayo si rahisi kuyaona kwa kuangalia hadi utakapoanza kutumia shamba ndo utaona tatizo.
Mf ni trekta ambazo zimekuwepo Tz kwa muda mrefu hivyo upatikanaji wa vipuri ni rahisi sana kuliko trekta zote na ni trekta imara pia.
Sasa tuangalie hayo matrekta mengine, tuanze na john deere (jd). Jd ni trekta ambalo ni gharama sana kwenye matunzo na matumizi ulaji wake wa mafuta ni juu kidogo maana unalimia gia namba 1 tu. Hata hayo yanayotokea India ni hivyo hivyo tu japo si imara sana.
Farmtrack (ft). Nimeshamiliki na bado namiliki hili tena toleo la kisasa kabisa (heritage series lenye horse power 75 lenye mfumo wa umeme kwa karibia kila kitu). Matatizo yake makubwa kwa muda wote ni fuse kuungua labda na hydrauliv pipe kupasuka ambavyo ni vitu vinapatikana kwa urahisi sana.
Ford. Hili kumiliki jipya ni gharama sana na kulitunza ni gharama pia na vipuri ni adimu kuvipata.
New holland. Bei nafuu, spare nyingi. Rahisi kulitunza pia.
Fiat na kubota. Haya yote ni gharama kweli kweli kwenye kila kitu.
Swaraja. Ni bei nafuu kila kitu, ila hayana nguvu. Labda kama shamba lako lina asili ya mchanga basi swaraj litakufaa.
Lovol(la kichina hili). Fuel pump ni mtihani mkubwa sana kwa hili na linakula mafuta sana. Lita 20 unapiga eka 1 ujiandae sana kama utanunua hili au lolote la kichina. Mawazo yanaweza kukua hapa.
Tafe. Hili halina tofauti na massey ferguson hata vipuri vinaingiliana kwa kiasi kikubwa sana.
Kama unanua trekta nakushauri nunua jipya lenye horsepower kuanzia 60 kwenda juu. Na kwa ushauri wangu massey ferguson (japo jipya la horse power 60, 2wd ni kama 45ml). New holland na farmtrack yanafaa hayo. Mimi namiliki hayo hayo matatu. Trekta ni kama gari tu usipozingatia service utaliweka juu ya tofali au utauza kama chuma chakavu. Na kazi ya kulima ni ngumu mno kwani mashamba mengi ya watanzania ni machafu yamejaa mawe na visiki vya kila namna kwahiyo trekta kuharibika ni jambo la kawaida sana labda kama unalimia shamba lako tu ndo utafaidi. Vile vile dereva mzuri anaejali chombo atakusaidia pia kufanya trekta lidumu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwel Hivi viJohn deer vinakimbia kama VW GolfIndia labda Swaraj tu ina afadhali, ila Farm Truck au John Deer new model ni kichefu chefu. Hii John Deer ya India spea zinapatikana India. hapa Tz hamna. Pia mkono wake wa jembe ni mwembamba sana kukatika n rahisi hauna nguvu.
Watu wanakimbilia hiz John Deer maana kiukweli zina shape nzuri na njian zinakimbia lakin shamban kimeo.
Pia hazidumu, mwaka tu ubabadilisha spea.
Kwel Hivi viJohn deer vinakimbia kama VW Golf