Togo yafungua Milango kwa raia wa nchi za Afrika kuingia bila Visa

Togo yafungua Milango kwa raia wa nchi za Afrika kuingia bila Visa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Togo imekuwa nchi ya sita barani Afrika kuruhusu raia wote wenye pasipoti za nchi za Afrika kuingia nchini humo bila visa, kuanzia Mei 18, 2026.

Kwa hatua hii, Togo inaungana na nchi nyingine kama Rwanda, Ghana, Benin, Gambia, na Shelisheli (Seychelles), ambazo tayari zimeshafungua milango yao kwa kutoa fursa kama hiyo ya kusafiri bila visa kwa Waafrika wenzao. Lengo kubwa la mabadiliko haya ni kuchochea mtangamano wa kiuchumi barani Afrika, kukuza biashara, utalii, na kuifanya Togo kuwa kitovu kikuu cha usafiri na biashara katika ukanda huo.

Hata hivyo, wasafiri bado watatakiwa kujaza fomu maalum ya taarifa zao mtandaoni kabla ya kuwasili, pamoja na kukidhi vigezo vyote vya sasa vya uhamiaji, afya, na usalama.

Taarifa hiyo ilitolewa na Wizara ya Usalama ya Togo kupitia waraka uliosainiwa na Waziri wa Usalama, Calixte Batossie Madjoulba, na limeanza kufanya kazi rasmi tangu Mei 18, 2026.

Chini ya utaratibu huu, raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wenye pasipoti halali za kitaifa wataruhusiwa kuingia na kukaa Togo bila visa kwa muda usiozidi siku 30.

Soma pia Burkina Faso kutoa visa bure kwa raia wa Afrika

Source: Business Insider Africa
 
Back
Top Bottom