Toka aliponitenda nimekosa imani kabisa na wanawake

Toka aliponitenda nimekosa imani kabisa na wanawake

Inaendelea……..

Baada ya kumwambia jamaa ampe mwenye simu ili niongee nae jamaa akaanza kunioji huku akifoka wewe ni nani? Nikaona isiwe tabu nikakata simu.

Kesho yake asubuhi sana simu inaingia namba ileile nikapokea, hapo nimefura hatari nikamwambia (happy) shida yako nini oooh,, nilikuambia usipige ile namba unaona sasa umemsababishia rafiki yangu matatizo? Yule mwanaume aliyepokea jana ni mume wake.

Baada ya kutoelewana mimi na yeye akampa rafiki yake aliyedadai ni mke wa jamaa, dah, rafiki yake akaanza kunilaumu kwani nimemsababishia matatizo makubwa kwenye ndoa yake basi kidume nikajirudi na kuomba msamaha. Nyie hawa wanawake walinichezea mchezo wa hatari.

Siku zikasonga baadae happy akarudi bongo, basi bwana siku hiyo tulipoza kiporo haswa.

Baada ya kukaa kama siku mbili akanipa taarifa nyingine kuwa anatakiwa kusafiri kuelekea Dodoma kwani kuna dada yake mkubwa amejifungua hivyo hana mtu wa kumwangalia.

Dada yake amemwambia anatakiwa kusafiri haraka, dah nikajisemea yaani umekuja juzi tu kesho unasafiri ndio nini sasa?

Sikuwa na jinsi siyo mke wangu siwezi kumzuia ikabidi niwe mpole, akasafiri baada ya ya safari mawasiliano yakawa shida tena simu yake haipatikani, kila nikipiga hola siku zikapita, baada ya muda akanitafuta kwa namba nyingine.

Shida nini mama mbona haupatikani? Akadai huko alipo ni kijijini sana mawasiliano ni shida, kidume nikaelewa siku zikasonga baada ya kukaa huko dodoma kama week mbili hivi, kuna siku akaniomba kama 20k hivi ila akadai nisimtumie kwenye namba yake kwani namba za siri hazikumbuki.

Hivyo atakwenda kwa wakala nimtumie moja kwa moja basi bwana kidume nikatuma.

Baada ya kutuma 20k ikakaa kama week hivi hajanitafuta kabisa, nakumbuka ile namba ya wakala message sikufuta hivyo nikasema nitatumia nii namba kujua ukweli upi huyu demu kweli dodoma au laa.

Nikaipiga ile namba ya wakala baada ya kupokea nikajifanya kama namwambia mimi nipo hapa Temeke hospital wewe umefika wapi? Basi yule wakala akaniambia utakuwa umekosea namba.

Nikamwambia hapana mbona hii namba sijakosea kwani wewe upo wapi wakala akaniambia nipo Morogoro, dah nilishikwa na butwaa kumwe huyu manzi yupo moro alafu ananiongopea yupo dodoma kwa dada yake.

Bahati nzuri siku inayofuata happy akapiga simu hi.. baby nikamuuliza habari za moro alikata simu. Baada ya kama dakika kumi akapiga simu samahani baby nitakuja nikwambie ukweli wote. Kesho naanza safari kuja dar.

Nakumbuka ilikuwa alhamisi kesho yake ijumaaa akaja dar, sasa ikabidi aanze kufunguka. Hapa ndio nikajua kuwa yule dada siyo dada yake wa tumbo moja bali ni majirani tu waliotoka kijiji kimoja.

Na yeye hapa dar alikuwa akifanya kazi za ndani (house girl) doooh,, nilichoka, aisee yule manzi alikuwa bomba yaani huwezi mdhania kuwa anaweza kuwa house girl.

Demu ananiomba msamaha machozi yanamtoka, kidume kweli nilipenda siyo kwa kumvumilia huku, ebwana nikamsamehe tena.

Sasa nikamuuliza huko moro unafanya nini? Akanijibu anafanya kazi za ndani kwa mama mmoja. Hivyo ameeomba ruhusa ya siku mbili tu atarudi moro. Nyie hawa viumbe wakikukamata haupindui.

Baada ya siku kadhaa akarudi moro, siku zikasonga, nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili 2016 tarehe 20akanijuza kuwa atakuja dar tusherehekee wote. Kidume poa.

Kweli bwana tarehe 24 akaja magheto, kesho yake tukaenda kariakoo kufanya shopping ya sikukuu (Christmas) bi dada akachagua viwalo tukamaliza kukaanza safari ya kurudi home.

Wakati tuaenda niliacha viatu vyangu shoe shine, kwa hiyo baada ya kurudi nikakuta bado shoe shine bado hajavisafisha ikabidi nimwambie mama tangulia nyumbani ngoja mimi nisubiri viatu. Dah kumbe ndio nimejiloga, wakati nikiwa pale machale yakanicheza hivi huyu nitamkuta kweli?

Dah,, kumbe nilichokiwaza kweli bwana nikachukua bodaboda fasta kwani nilimkuta 😂😂 kasepa kabeba nguo zake tu hajaiba chochote nilichoka.

Nikaona hata aibu kuwauliza majirani, hapa sasa nikasema basi inatosha huyu siyo mwanamke hanifai. Aseeh hawa wanawake wana roho ngumu licha ya kufanya matukio yote hayo bado aliendelea kunitafuta.

Hapo ndio ulikuwa mwisho wa kuonana nae. Japo aliendelea kunitafuta ila ndio hivyo tena moyoni mwangu alishatoka.
 
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,
Nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi ooh, ooh na
Dharau tele
Ungenieleza ukweli solemba,
Kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi ooh ambayo si ya
Kweli.
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele solemba.
Nilichomwa na jua toka asubuhi,
Mpaka saa nane Solemba sababu ya
Kukungoja wewe
Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani
Nimeshituka Solemba,
Nimeshituka Solemba
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele solemba.
Sikutaki tenaaa, sina haja nawe, nimeshapata
Mwingine atakaye nipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha
Kama mimi
Huna huruma Solemba... Aloi I love you
Baby
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
Ila dharau uliweka mbele solemba.
 
Shida wanaume wengi hawajui kama wadada wapo kwenye mahusiano Kwa faida. Akiona kwako hakuna faida anasepa. Mwanaume unatakiwa kuelewa this generation hakuna mapenzi. Tafuta Hela uenjoy tu.
Ukishalitambua hili na ukawa huogopi vimizinga vya hapa na pale mbona kile leo unaonja mbususu mupya alafu wala hawana shida wee kuwapanga. Tuwagegede tuu hawa warembo. Ni watamu sana.
 
Back
Top Bottom