Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Hali ya usalama jijini Dar bado ni ya mashaka.

Ninaomba vyombo vya dola vifuatilie maeneo ya BULULA,GOLANI na MATOSA katika kata ya Saranga.

Maeneo hayo yanasemekana kuhifadhi wahuni wanaokimbia operesheni kali za jeshi la Polisi katika maeneo mengine ya mji haswa Manzese ambapo inasemekana wengi wa wahuni hao ni mabaki ya makundi ya MBWA MWITU na PANYA ROAD.

Hivi karibuni kumeanza kuibuka uhalifu wa kupora watu,watu kushambuliwa na vikundi vya wahalifu na kukatwa mapanga huko Matosa, Bulula na Golani.

Sasa hivi kuna taarifa kwamba wahalifu hao hasa kutoka Bulula na Golani wanakwenda hadi Kimara Suka na Kimara stop over nyakati za usiku na kufanya uhalifu kwa kushirikiana na makundi ya wahuni wa Suka,Stop over na Matosa.

Taarifa zinafika Polisi Kimara na Mbezi lakini zinapitishwa defender mbili tatu kwa siku moja au mbili bila ya kukamata wahusika halafu kimyaaa, wahuni wanazidi kuvimba vichwa na kuzidisha uhalifu mitaani.

Naomba mamlaka za juu za kiserikali na vyombo vya usalama kutokupuuzia suala hili,haswa makundi yanayojiunda upya huko Bulula na Golani.

Msikurupuke,fanyeni uchunguzi wa kina kujua nini kinaendelea,tumeni watu toka mbali kwani hawa askari wenu wanaohusika na maeneo hayo (Mbezi) wako compromised.

Pia suala hili limulike Dar yote,wahuni wana syndicate zao siku hizi.

Wana mitandao ya kimaeneo jijini na wanasimamiwa na tycoons wenye pesa,maarifa,mikakati na masoko kwa ajili ya biashara zao haramu.

Wana mitandao hadi kwenye bodaboda na madereva taxi.

Pale Ubungo kulikuwa na wizi lakini tangu kituo kihamie mawasiliano na wizi nao umehamia huko na maeneo ya zile njia za pembeni kuelekea Mlimani city.

Mmeshawahi kwenda kuchunguza nini kinaendelea chini ya yale madaraja ya Ubungo?

Nasikia mali nyingi zinazoibwa eneo la Ubungo zinapatikana chini ya madaraja yale. Fuatilieni.

Haya makundi msiyape nafasi,maana watu wenye pesa na exposure kubwa ya maisha wameanza kuyageuza dili na kuyatumia,hivyo kuwapa mbinu zilizoenda shule.

Msipojipanga na mkipuuza jiji halitakalika hili huko mbele.

Halafu vita ya vijiwe vya madawa na bange inawashinda nini jamani? Watoto wanaharibika. Vijiwe vya wahuni ndio center za kuuza bidhaa hizo na niwaambie jambo moja msilolijua akina Makonda na wenzio, HOMOSEXUALITY IS VERY COMMON THERE.

Wahuni wengi wanaotumia madawa na bange wanafanyiana huu ushenzi,saaana tu, ni siri zao. Msikurupuke, fanyeni uchunguzi, mtajua meengi sana, halafu anzisheni operesheni zenye malengo,mkiwa na uhakika where to hit and how and when.

Mwisho ninawaasa wazazi wenzangu wenye watoto wenu boarding schools. Hawa wahuni na vijiwe vyao wana wateja wengi wa bangi huko boarding schools wanawapelekea. Sijui walimu na walinzi wa hizo shule wanakuwa wapi. Sasa bangi ya leo sio ile mliyokuwa mkivuta nyinyi enzi zenu. Bangi zao wanachanganya na unga humo humo. Wakikosa kabisa huchukua valium,bangi na gundi ya viatu wanachanganya humo. Huyu mvutaji wa hiyo kitu ukikutana naye usiku akikunyanyulia panga akate sikio, harudishi mkono bila sikio lako.

Kama mnajali jamii yenu basi fanyieni kazi taarifa mnazopata.
 
Kero kuu na kubwa kwa kundi la watu wengi ni AJIRA, mimi ninachoamini ni kwamba, ajira zipo lakini jinsi ya utoaji wa ajira hizo ndo kero inapoibuka.

Kwa mashirika ya binafsi, wengi hutumia watu wao hasa kutoka nje, hawawathamini wazawa, wenyewe pengine wanaamini wakiwa na utofauti wa rangi ofsini kwao ,basi maendeleo ndo yanakuwepo.

Kwa serikali, kujuana kunakuwa kwingi, hata vyombo vilivyopewa dhamana ya kusimamia hili, bado havijakidhi vigezo.

Tunaomba Rais wetu, usimamie haya na mengine mengi, sio lazima kuajiliwa , tutaridhika hata tukiwekewa mazingira ya kujiajiri.

ASANTE.
 
Inakera sana unaponunua kitu ukiomba risiti unaambiwa bado tunafuatilia EFD TRA. Nyie TRA kwani inachukua miaka mingapi kumpatia mtu hiyo machine. Mapato bado yanavuja sana wafanyabiashara wengi hawana hizo machine, wapeni bwana tutengeneze Tanzania.
 
Inakera sana unaponunua kitu ukiomba risiti unaambiwa bado tunafuatilia EFD TRA. Nyie TRA kwani inachukua miaka mingapi kumpatia mtu hiyo machine. Mapato bado yanavuja sana wafanyabiashara wengi hawana hizo machine, wapeni bwana tutengeneze Tanzania.
TRA kila mtu ni BOSS hata mtu wa mapokezi ni BOSS....juzi kati nmeenda TRA ilala nmekuta watu wengi wanahitaji kulipa na maofisa wengi hawapo...sijui ndio hewa zenyewe
 
Takribani wiki tatu zilizopita niliandika kuhusu kusua sua kwa uletwaji wa umeme katika kijiji cha IHOWANZA kilichopo kata ya IHOWANZA na tarafa ya Malangali, mkoa wa Iringa.

KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAOMBA NITUMIE FURSA HII KUMSHUKURU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KWA KUIONA KERO YANGU NA KUIFANYIA KAZI.

KWA SASA UMEME UMEWASHWA NA SISI WANANCHI TUNAENDELEA KUNUFAIKA. PONGEZI KWENU.
 
BUREAU DE CHANGE ZOTE ZIFUNGWE ZINAHATARISHA UCHUMI WA NCHI.

1. zinachangia kutorosha fedha nje ya nchi
2. zinasababisha ukwepaji kodi kwa sababu waagizaji wa mizigo wanatumia kufanya miamala ya T/T,.
3. Million saba kwa dakika zilifichwa huko. zinasababisha money laundering itokanayo na madawa ya kulevya,
4. wamiliki wengi ni BOT worker.
5. zimevunja sheria za nchi zilizowekwa na watanzania.
6. Hazikaguliwi na kusimamiwa ipasavyo.
7. Pato lake halitokani na biashara halisi
8. Zinasababisha shilingi ya Tanzania kukosa thamani.
9. Zinasababisha kupanda kwa dola na kusababisha ugumu wa maisha kwa watanzania.
10. zinasababisha Rushwa kukidhiri kwenye huduma ya mabenki.
11. Hazichangii maendeleo ya jamii kama ilivyo kwenye mabenki. Mheshimiwa Rais mimi kama mtafiti na mtaalam wa mambo ya fedha napendekeza zifungwe na shughuli yake ifanywena mabenki tu. Kwa hiyo hili ni jipu kubwa sana.

MHESHIMIWA RAIS NAPENDEKEZA TAFAKARI,FANYA UTAFITI THEN TUMBUA KABISA HILI JIPU'
Katika baadhi ya masuluhisho ya kero hizi ni:
  • Kuweka dawati la BOT katika kila Bureau de Change ili kusimamia na kutoa risiti za BOT baada ya mauzo na manunuzi ya mteja( Idadi ya Bureau kama 222 -kwa mujibu wa mwaka 2012). - suluhisho la muda mfupi/wa kati.
  • Kuweka utaratibu wa kutumia ATM maalum kuuza na kununua fedha za kigeni katika Bureau na mabenki.- Suluhisho la muda mrefu.
  • Kufunga Bureaux zenye utata wa mahesabu na zisizofanya kazi.
 
Mkuu waachie Nchi yao maana wao wamezoeya kuishi kwa unafiki kuliko ukweli,wape nafasi waibe wawezavyo. Waache wapige deal ndio maisha yao.

Nchi ilitaka kumfia Kikwete mwaka jana akakwepa hivyo usikubali ikufie wewe Magufuli. Wamezoea uongo na magumashi hutawaweza hao maana wamekugeuka wote umebaki peke yako.
 
Mkuu waachie Nchi yao maana wao wamezoeya kuishi kwa unafiki kuliko ukweli,wape nafasi waibe wawezavyo. Waache wapige deal ndio maisha yao. Nchi ilitaka kumfia jk mwaka jana akakwepa hivyo usikubali ikufie wewe Magu. Wamezoea uongo na magumashi hutawaweza hao maana wamekugeuka wote umebaki peke yako.
Hakuna, siyo kweli. Tatizo la mkuu ni vitu vichache vinavyowafanya walio wengi kuona afadhali ya ufisadi kuliko yanayoendelea.
1. Matumizi ya hela za serikali bila kibali cha bunge- splurge
2. Kuua democrasia
3. Kukanyaga sheria na Katiba
4. Condemning suspects unheard- violation of one of the cardinal principle of natural justice
5. etc, etc, etc, etc, etc

Otherwise kukabiliana na mafisadi ni jambo jema tu!
 
Kwanza naomba kumpongeza mheshimiwa rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ili kuwaletea watanzania maendeleo ya kweli.

Pia naomba kumshauri mheshimiwa Rais Magufuli kwamba:-

(1) Asitishike na wanaojifanya wanataka kufanya maandamano ya nchi nzima, hawa ni watu wasioitakia mema nchi yetu. Sisi watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu tupo nyuma yake na tunathamini kazi nzuri anazozifanya rais wetu.

(2) Mheshimiwa rais Magufuli ajue kuwa, huu ni wakati wa yeye kuonesha kuwa yeye ndiyo pekee rais wa nchi mpaka sasa, hivyo achukue hatua kali zaidi kwa yeyote atakayeshiriki kwenye maandamano yanayopangwa kufanyika. Nchi haiwezi kuwa na marais kila kona. Kila mtu anatoa tamko lake kana kwamba na yeye ni rais. Watu hawa watatucheleweshea maendeleo yetu. Zaidi sana madai yao hayana kichwa wala miguu zaidi ya kuwalisha wananchi kasumba mbovu kwa maslahi yao binafsi. Kwa hakika watashindwa wao tena vibaya mno.

MUNGU WA IBRAHIM, MUNGU WA ISAKA NA MUNGU WA YAKOBO AINYOOSHE FIMBO YA NGUVU ZAKE KUTOKA MBINGUNI ILI RAIS MAGUFULI AWE NA ENZI KATI YA MAADUI ZAKE WOTE, NA AWAWEKE MAADUI ZAKE CHINI YA MIGUU YAKE.

AMINA.
 
Pongezi kwako na serikali yako baba yetu mheshimiwa rais Magufuli.

Kazi nzuri unazozifanya ili kuleta maendeleo sisi watanzania tunaona na tunathamini.

Mungu mwenyezi akulinde, akubariki na awateketeze maadui zako kwa moto mkali ushukao kutoka juu.

Amina.
 
Inakera sana unaponunua kitu ukiomba risiti unaambiwa bado tunafuatilia EFD TRA. Nyie TRA kwani inachukua miaka mingapi kumpatia mtu hiyo machine. Mapato bado yanavuja sana wafanyabiashara wengi hawana hizo machine, wapeni bwana tutengeneze Tanzania.
TRA naona bado hawajajipanga. Kuna maduka mengi pamoja na petrol stations hazina EFD. Wanatakiwa wajipange vyema kukusanya mapato vinginevyo watamuangusha Rais.
 
Vibaka jiji la Dar es Salaam ni kero, yaani wanaathiri hadi shughuli za kawaida.

Kuna baadhi ya maeneo hata kutoka asubuh ya saa 12 huwezi
 
BUREAU DE CHANGE ZOTE ZIFUNGWE ZINAHATARISHA UCHUMI WA NCHI.

1. zinachangia kutorosha fedha nje ya nchi
2. zinasababisha ukwepaji kodi kwa sababu waagizaji wa mizigo wanatumia kufanya miamala ya T/T,.
3. Million saba kwa dakika zilifichwa huko. zinasababisha money laundering itokanayo na madawa ya kulevya,
4. wamiliki wengi ni BOT worker.
5. zimevunja sheria za nchi zilizowekwa na watanzania.
6. Hazikaguliwi na kusimamiwa ipasavyo.
7. Pato lake halitokani na biashara halisi
8. Zinasababisha shilingi ya Tanzania kukosa thamani.
9. Zinasababisha kupanda kwa dola na kusababisha ugumu wa maisha kwa watanzania.
10. zinasababisha Rushwa kukidhiri kwenye huduma ya mabenki.
11. Hazichangii maendeleo ya jamii kama ilivyo kwenye mabenki. Mheshimiwa Rais mimi kama mtafiti na mtaalam wa mambo ya fedha napendekeza zifungwe na shughuli yake ifanywena mabenki tu. Kwa hiyo hili ni jipu kubwa sana.

MHESHIMIWA RAIS NAPENDEKEZA TAFAKARI,FANYA UTAFITI THEN TUMBUA KABISA HILI JIPU'

Mabanda, "ndugu yangu usilaumu wakunga uzazi ukalipo". Hebu tutafute tatizo liko wapi. Mwenye kufanya "fiscal policy" ya nchi sio bureau de change. Hebu soma tena sheria zilizo wekwa kwenye ubadilishaji wa fedha.

Hivyo, ukirudi miaka 30 nyuma na kuangalia hali ya uchumi wa Tanzania ulivyo, utajua matatizo yapo wapi. Pengine manahodha wamechoka wapumzishwe.
 
Majohe kwa Ngozoma, rada, shule kuna utapeli unafanyika!!

Viongozi wa serikali za mtaa wametangaza kiasi cha wananchi kuchangishwa kulipia pesa za ukusanyaji wa takataka lakini ukitulia na kufanya calculation utagundua pesa zinazopatikana ni nyingi sana!!

Kampeni hii waliianzisha tangu miaka ya nyuma lkn siku zote huishiwa njiani na pesa huliwa in such away that hata wale wanaobeba taka mishahara yao hawapewi ....je pesa hizo huwa zinaenda wapi?
 
Utaratibu wa kutoa malalamiko uko wazi - kama una tatizo kila halmashauri na mkoa kuna dawati la malalamiko hivyo iwapo kuna shida waone taasisi hizo.
Je, unadhani kila mwananchi anajua mahali hapo sahihi kufikisha malalamiko yake?

Nadhani elimu zaidi inatakiwa kutolewa ili wananchi wajue mahali gani katika wilaya yao au mkoa, wanaweze kupeleka malalamiko yao.

Najua hii serikali ndiyo ingechukua sera/kauli mbiu ya ukweli na uwazi, kwani iko vizuri katika kuhudumia wananchi katika uwazi na ukweli.

Mungu msaidi maisha marefu raisi wetu afanye kazi uliyomtuma hapa dunia(Tanzania)
 
Mheshimiwa waziri wa NISHATI na MADINI, kwanza nikushukuru na kukupongeza kwa kazi nzuri unazozifanya, sisi watanzania tunazitambua juhudi zako. TUNAOMBA utusaidie mchakato wa upelekwaji UMEME katika mitaa iliyopo jirani kabisa na mji wa Makambako(MKOA WA NJOMBE)
 
Aende afatilie mkuu wa wilaya ya sumbawanga Dr khalfan haule, alikula pesa ya uchaguzi, pia ni mtuhumiwa TAKUKURU ana kesi nyingi mno
 
Je, unadhani kila mwananchi anajua mahali hapo sahihi kufikisha malalamiko yake?

Nadhani elimu zaidi inatakiwa kutolewa ili wananchi wajue mahali gani katika wilaya yao au mkoa, wanaweze kupeleka malalamiko yao.

Najua hii serikali ndiyo ingechukua sera/kauli mbiu ya ukweli na uwazi, kwani iko vizuri katika kuhudumia wananchi katika uwazi na ukweli.

Mungu msaidi maisha marefu raisi wetu afanye kazi uliyomtuma hapa dunia(Tanzania)
Hata hivyo mimi siamini dawati sijui sanduku la malalamiko.

Kwakuwa wanaotunza hayo masanduku na "kuyagubua" kuchukua kusoma hayo malalamiko,saazingine ni haohao waliolalamikiwa.

Utegemee kesi ya nyani kula mahindi, ishughulikiwe na tumbiri,kutatua kero za kula mahindi kwenye mashamba ya watu?

Me naona jukwaa salama la kutolea malalamiko ni humu JF. Unapaka mtu hadi anajiheshimu na kujirekebisha.
 
Back
Top Bottom