Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
Akosema anaachia ngazi
 
Hilo linasaidia vipi mamilioni ya watu waliopo vijijini Kwa mfano. Na je una uhakika Hilo tu kitakufanya uamini kweli magufuli ni rais wa wanyonge.. Jukumu Hilo umeliona ni gumu Sana na ni muhimu Sana kutekelezwa??? Upo serious
Hilo ndo litabeba impact nzima ya zana yake ya kutetea wanyonge maana wapo walofoji vyeti na walikua watumishi wametimuliwa saivi wapo vijijini, sasa wanapoona wengine hawachukuliwi hatua yeyote hata kama angegawa pesa kila siku kwa raia wa Tanzania hakuna atakae mwelewa
 
Shushu bnh mmetumwaa eeeh kichinjiioo kipo nakitunza kuliko mboni yng
 
Hakuna moja, kuna elfu moja na moja.

Magufuli hataki mjadala, ana hulka ya udikteta, anajiona anajua kila kitu, kasema watu watalimia meno. Kasema wasio na nauli watapiga mbizi.

Anafuga mtu aliyeiba mpaka jina na kufoji vyeti, huku akijinadi anapiga vita waliofoji vyeti.

Hana muelekeo wa kisiasa unaoleweka. Leo anaweza kuvunjia nyumba watu mabondeni bila simile (si mtetezi wa wanyonge) kesho akaachia Wamachinga wafanye biashara bila mipango (anatetea wanyonge bila mpango endelevu).

Magufuli haheshimu uhuru wa bunge, kalipangia bunge jinsi ya kutumia fedha za tafrija bila hata makubaliano na Spika.

Magufuli haheshimu uhuru wa bunge. Kaapisha wabunge wa kuteuliwa wawe mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge.

Magufuli haheshimu uhuru wa mahakama. Kahutubia mahakama na kuzielekeza jinsi ya kufanya kazi wakati mahakama ni mhimili unaojitegemea.

Magufuli hathamini utenganifu wa serikali na kanisa. Anahutubia habari za kisiasa makanisani. Hili linaweza kuleta mtafaruku na mpasuko wa nchi kidini. Nyerere alikuwa anasali St. Peters kila siku akiwa Dar. Mwinyi aliswali sana Msikiti wa Tambaza. Mkapa alisali sana kanisa la St. Immaculata. Kikwete naye pia motto wa Bagamoyo msikiti anaujua. lakini wote hawa hawakuwahi kuhutubia siasa kwenye madhabahu ya dini to my knowledge, ukiondoa maneno machache tu ya shukurani labda.

Huyu Magufuli anatoa hotuba ya siasa kabisa, kanisani!

Magufuli hatahamini utawala wa sharia. Kawaambia Polisi wakiona gari la kawaida linaenda kwenye lane ya mwendokasi, walichukue, walipeleke polisi, watoe matairi, mwenyewe akija kuulizia matairi wamwambie lilikuja hivyo hivyo bila matairi.

Magufuli hana heshima hata kwa mawaziri wake. Anawaruka bila hata uchunguzi. Mke wa Waziri wake wa karibu kaonewa/ wamepishana maneno kidogo na trafiki, jibaba kaingilia issue na kuvunja utaratibu wa mtu kupandishwa cheo polisi.

Magufuli hataki hata kusoma hotuba anazoandikiwa, matokeo yake anasema madudu.

Magufuli anapenda maamuzi ya ghafla na jazba ambayo hayajachekechwa vizuri na mara nyingine yana athari kwa taifa.

Magufuli ana kauli za kijinga kama motto anayebalehe, ona alivyomdhalilisha Mama Kikwet, mke wa bosi wake wa zamani, kwa kumwambia maneno yasiyo staha hadharani.

Magufuli hawezi mijadala ya kisiasa. Ndiyo maana kapiga marufuku mikutano ya siasa ya wapinzani kinyume na katiba.

I could go on and on and on. kwa nini unataka niseme moja tu?

Msingi mkubwa ni kwamba Mgufuli hana uwezo wa kuwa rais.

Mtu kama huyu hafai kuwa kiongozi.
Dah umemaliza kila kitu respect [emoji109]
 
Hilo linasaidia vipi mamilioni ya watu waliopo vijijini Kwa mfano. Na je una uhakika Hilo tu kitakufanya uamini kweli magufuli ni rais wa wanyonge.. Jukumu Hilo umeliona ni gumu Sana na ni muhimu Sana kutekelezwa??? Upo serious
We s umeuliza? Na yeye kakujbu amtimue bashite ziro
 
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
 
Hilo linasaidia vipi mamilioni ya watu waliopo vijijini Kwa mfano. Na je una uhakika Hilo tu kitakufanya uamini kweli magufuli ni rais wa wanyonge.. Jukumu Hilo umeliona ni gumu Sana na ni muhimu Sana kutekelezwa??? Upo serious
Itaonesha tu amri ya mkuu haina exception.
 
Mimi ningempenda na kumtambua ni mtu wa wanyonge kama angefungia kiuno shida ya maji nchi nzima. Hili ni tatizo kubwa na ni ngumu sana kufanikisha.
 
Kwanza aziamuru wizara zake zote zitoke katika majengo ya vyuo maana. Katika usanifu majengo hutegemea Sana matumizi sasa yale majengo hayakusanifiwa Kwa ajili ya ofisi bali n Kwa ajili ya vyuo
 
Linagusa vipi maisha ya watanzania? Je una uhakika gani kuwa siyo rumors? Au umesahahu ya Mwamunyange 2015?

Wewe huoni kuwa imani kwa muongoza imepata msukosuko. Au mna amini kuwa wote wanaolipigia kelele hili suala hapa ni wauza unga, wavivu, wenye wivu, husuda, wapinzani and the like? Kama hapo awali ufafanuzi ulitolewa kwa hoteli meneja kuhusu jina na vyeti vyake, kwa nini sasa iwe shida? Ni ugumu gani umetokea kipindi hiki? Je mmepima demage ya serikali katika kulizibia masikio na kulifumbia macho hili hasa huko mbeleni?

Na washawasha!
 
Mkuu jambo unalolisema ni kweli kabisa kuwa lazima RC aondoe utata kuhusu vyeti vyake au awajibike kwa endapo itabainika ameghushi vyeti. Binafsi sifurahishwi na huu u-double standard ila hoja inabaki pale kuwa, je, hili swala la vyeti linagusa vipi changamoto za kimaisha za watanzania wanyonge?
 
Aachane na kukimbizana na wapinzani na visasi visivyo na maana.....
 
Back
Top Bottom