Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Kuna watumishi wengi wa umma ambao tuhuma zao za kijinai zimesafishwa na mahakama na jamhuri imeridhika pasipo kukata rufaa lakini waajiri hawataki kuwapangia majukumu huku wakilipwa mishahara kila mwezi bila kufanya kazi kinyume kabisa na kauli mbiu ya mh Rais yahapa kazi tu.
 
Kuna wafanyakazi wa TANROADS wanakuwa na gari Hardbody Ya Tanroads nyeupe inasimama njia ya Msata - Bagamoyo mida ya usiku, wanakula rushwa kwa kila fuso za mizigo zinazopita njia ile.

Kwa siku wafanyakazi hao huenda nyumbani na sh3m.

Tuanze na jipu hilo kwanza maana huo mchezo ulikuwepo tangu yeye akiwa waziri wa ujenzi.

utaifakwanza
ww kinachokuuma n nn?
 
Kuna watumishi wengi wa umma ambao tuhuma zao za kijinai zimesafishwa na mahakama na jamhuri imeridhika pasipo kukata rufaa lakini waajiri hawataki kuwapangia majukumu huku wakilipwa mishahara kila mwezi bila kufanya kazi kinyume kabisa na kauli mbiu ya mh Rais yahapa kazi tu.
Peleka taarifa ikulu
 
....sijui kama hili wazo linafaa?

....tujadili kama linafaa tumsaidie magufuli afanye informed decision.

...nimesema kwenye moja ya topic,

...serikali iwe na tume ya nje ya watu kutoka mataifa mbali mbali ambao ni exparties kwenye different fields kama fedha,elimu ,afya etc,ambao watafanya kazi kushirikiana na wafanyakazi wa ndani,kuleta utaalamu wao,

..serikali inaweza kutumia hela nyingi kuwalipa ila in the long run tutafaidika.....

..karibuni
 
Sisi wafanyabiashara kariakoo tunapatavshida mno tunashumbuliwa na polisi kwa ajili ya rist za efd mkuu rushwa inanuka..
 
Nawapongeza mnaomiliki JF. Mmetupatia uwanja mahsusi wa kutolea pongezi, maoni na kero zetu.
Binafsi nashukuru sana kwa sababu niliwahi kuleta kero zetu na baada ya kipindi kifupi kero zile zilishughulikiwa kikamilifu.
Kero zile(ile ) ilihusu masuala ya umeme wa REA kule kijijini kwetu.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
TCU VIPI LEO?
 
Meneja Tanesco Mbezi ni funga mwaka. Umeme anakata kuanzia saa kumi na mbili alfajiri mpaka saa kumi na mbili jioni. Hi ni kwa maeneo ya Mbezi na Kibamba; na hata sasa Katanya hivyo. Prof Muhongo ile ahadi yako ya kutowavumilia mameja wasio kuwa na maslahi kwa Shirika na taifa inastahili kabisa kumuangukia huyo Meneja wa TANESCO Mbezi.
Anza na huyo maaana anawanyanyasa wanachi wa chini wa Mh Rais, kina mama Lishe na juice zao zinakosa ubaridi, vipi wenye vijiwe vya kufyatua matofali; na wale wenye mabucha ya Nyama na samaki; wapo wenye maduka nk nk. Pili, analikosesha shirika mapato ambayo yangetokana na utumiaji wa units za Luku.
 
Wanasiasa wamekuwa karibu saana na wananchi wanapoomba kura, ila kiutekelezaji ni zero..hasa hawa wabunge, madiwani nk.

Jamani barabara za wilaya nyingi hazitamaniki...Wananchi wengi wanakufa kabla ya kufika hospitali katika hospitali zao za wilaya..
Mfano barabara ya Halmashauri ya wilaya Rufiji kuelekea Hospitali ya Utete haipitiki kabisa kipindi hiki cha mvua, si kwa gari, si kwa pikipiki, si kwa miguu...Mbunge, Diwani, Viongozi wetu mko wapi...?

Mkuranga leo namsikia Bonge akiongelea watu wamepanga madumu wanavuka katika mto..hakuna daraja...jamani tunatia aibuuu...

Mbunge wa haya maeneo vipi? Unasinzia bungeni au.....maendeleo yanakupiga chenga....unatia aibu...
 
NAOMBA KUTOA MAONI YANGU KWA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
Kwanza napongeza kazi zote zinazofanywa na wizara hii.
Maoni yangu ni kwamba, mpaka sasa kuna utaratibu wa kila mwezi WALIMU WAKUU na WARATIBU ELIMU KATA kupata fedha kutoka serikalini zinazoitwa POSHO YA MADARAKA. Katika fedha hizo kila mwalimu mkuu hupata shilingi laki mbili (200,000/=) na kila Mratibu Elimu Kata hupata shilingi laki mbili na nusu (250,000/=) kila mwezi.
Jambo lenyewe siyo baya, lakini ubaya wake unakuja pale ambapo fedha hizo zinamlenga mwalimu mkuu pekee yake bila kumgusa mwalimu mwingine zaidi yake.
Fedha hizi zisingekuwa na ubaya kabisa kama angalau nusu yake ingewagusa walimu wengine.
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mwalimu mkuu anayeweza kufanya kazi kwa mafanikio akiwa pekee yake bila kushirikiana na walimu wengine.
Ikumbukwe kuwa walimu wakuu wana vikao vingi hivyo shughuli nyingi za shule hufanywa na walimu wakuu wasaidizi pamoja na walimu wa Taaluma wakishirikiana na walimu wengine, hivyo fedha hizo kumlenga mwalimu mkuu pekee yake kwa maoni yangu si vizuri sana.
Hata hivyo kuna WALIMU WAKUU wenye busara na waliojaliwa kuwa na kipato kizuri. Walimu wakuu hawa hutoa nusu ya fedha hizi na kuwanunulia walimu angalau hata soda.
NINI MATOKEO YAKE?
Matokeo yake ni kwamba÷
(1)Kumekuwa kukitokea migogoro mingi shuleni hasa kati ya walimu na mwalimu mkuu.
(2)Walimu wengi wamekuwa wakimgomea mwalimu mkuu kufanya baadhi ya kazi hasa zile zenye harufu ya majitoleo kwa kumtaka mwalimu mkuu kufanya kazi zote za ziada kwani ndiye anayepata fedha za ziada.
NINI KIFANYIKE?
Ama ÷
(1)Waziri mwenye dhamana aandike barua inayowataka walimu wakuu kutumia kiasi fulani cha fedha hizi na kiasi kingine kigawiwe kwa walimu wengine.
(2)Serikari ilete fedha zingine kila mwezi kwa ajili ya kila mwalimu kama POSHO.
(3)Au serikali ifutilie mbali hizi posho za WALIMU WAKUU kwani kwa asilimia kubwa zinaleta mitafaruku mingi kwa walimu wengi badala ya kuleta neema.
AHSANTE, NAWASILISHA.
 
Magufuli ana nia njema sana, ninajivunia kwamba kura yangu haikupotea, bahati mbaya siwezi kumfikia nimpe mkono wa pongezi lakini vita hii ni ngumu ili aishinde anapashwa kuharakisha sana uundwaji wa katiba itakayo weka misingi ya uwajibikaji na uadilifu, hii iliyopo sasa imechakachuliwa sana haiwezi kushindana na mbinu za waliyoiweka na waliyoichakachua. KATIBA MPYA SI AGENDA YA WAPINZANI NI AGENDA YA WATANZANIA WOTE.
 
rais aendelee kufumua na kuboresha mifumo ya utendaji serikalini ambayo ilikuwa corrupt na weak
 
Mimi ninashida ambayo mtatuzi wake ni waziri wa ulinzi na usalama maana hawa waliopewa dhamana ya kutulinda sisi na mali zetu wameshindwa kunitatulia tatizo langu .ninaomba mwenye mawasiliano ya waziri mheshimiwa Mushemba anipe
 
Back
Top Bottom