1. Ondoa wakurugenzi waliowekwa kiukada, hawana msaada wowote wa kuendesha mambo kiueledi zaidi ya siasa
2.Mchezo wa kupotezana, kutkana, kuumizana ni ushamba na dalili za kushindwa kujibu hoja kwa hoja
3. Achana na kuteua watu KIDINI, kuteua watu kwa mrengo wa udini ni kujibania pool ya talent za kusaidia maendeleo kwa upofu wa "hawa ni wenzangu" na "wale si wenzangu", wakati kumbe ni taifa la watu walewale tu, jahzilikizama tunazama wote!
4. Ondoa white elephants projects, Uza ndege hizo pesa tuingize kwenye umeme wa gesi
5. Kuua private sector ni kuturudisha kwenye siasa za uchumi zilizofeli za Julius Nyerere, ni aina ya uchumi muflisi
6. Nchi lazima iwe na mipango endelevu, siyo kila anyekuja anakuja na ishu zake, anavunjavunja zile alizoshiriki kuzipitisha
7. Lazima sheria za nchi, uhuru wa watu, Demokrasia na Utaalam viheshimiwe
8. Rudisha Trilion zetu 2.4
9. Hakikisha unaenda mahakamani kudai Trilion zetu 424 tulizoibiwa na ACACIA, Mtu akisamehe hizo ni mhaini, huwezi kusamehe pesa inayolingana na bajeti ya nchi ya miaka 15 halafu usiwe msaliti!
10. Elimu bora na siyo bora elimu, lazima Elimu ya vitendo itiliwe mkazo, siyo matheory ambayo ukishapiga NECTA unatupa kule hayakusaidi choochote, lete elimu ya ujasirimali, ufundi kama vile ujenzi, umeme, vyombo vya moto, electronics, computer, mabomba, ufugaji, ususi, ushonaji etc. Hiyo ndo elimu ya maana, Siyo habari za Historia ya Ulaya kwenye middle ages, itanisaidia nini mimi?