Shalom shalom
Kama ukapata fursa ya kwenda kufanya kazi ulaya, uarabuni au Amerika nenda haraka sana hata kama ni kazi ya beki 3 au kubeba box, mlinzi au store keeper, kusafisha vibibi nk, acha kazi yako ya halmshaur nenda.
Beki 3 Saudi Arabia, Jordan, Oman, Dubai, Qatar UAE anamafanikio na maendeleo kuliko mfanyakazi wa halmashauri bongo na tamisemi na hao walinda watu na Mali zao ambao hawana access yoyote ya kuibia wananchi au mali za umma
Hakuna mfanyakazi wa bongo wa halmashauri au tamisemi hata madokta anaeweza kujenga nyumba nzuri 3 Kwa miaka 5 kama sio mwizi au mla rushwa na mikopo kausha damu, lakn beki 3 na wabeba box katika hzo nchi wanajenga bila shida na aibi wala hakopi.
Usisuburi fursa bali itafute fursa, kama umeajiriwa huko ndo unanafasi kubwa ya kupanga mipango ya kuondoka kirahis zaidi na hata kutafuta kazi nzuri zaidi huko, usikubali kufia TANZANIA kajaribu duniani huko huyo sio ww unastahili zaidi ya hapo.
Nyie wabishi bakini hapahapa na mishahara yenu ya Laki 5 Hadi 1.5milion ambayo mbeba box anaipata Kwa siku 4 hadi 5 tu.
Watanzania wengi tunawajua sio wapambanaji hamna uthubutu na hamuwezi kuchukua maamuzi magumu na kwenda kupambana huko mbele mkishapata uhakika wa kula, gari la mkopo used, na kulala kwenye mapagala , kupeleka mtoto EMS mnajiona maboss na mshamaliza kila kitu hapa duniani.
Kwahy nategemea mtakuja na kejeli za kila aina lakn ukweli utabaki palepale ukipata nafas ya kukimbia utumwani kimbia acha uzito
Nawasilisha