Toka nje ya kundi: Wewe ndiye wa kujipatia ukitakacho

Toka nje ya kundi: Wewe ndiye wa kujipatia ukitakacho

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Siyo Serikali, Dini, Elimu au Jamii vitakavyoweza kukupa kile unachotaka haswaa. Toka nje ya kundi, wewe ndiye wa kujipa kile unachokitaka.

Toka nje ya halaiki, jitafute na ujipe kilicho chako. Hakuna njia rahisi zaidi ya kutoka katika kundi licha ya ukweli kuwa mizizi ya makundi imejiimarisha sana.

Wewe siyo Jamii licha ya kuwa sehemu ya Jamii. Hakuna wa kukupa ukitakacho zaidi yako. Mifumo imekazwa kuhakikisha watu tunafanana na kuishi kwa namna ileile. Hakuna wa kumtoa mwezake kundini kwa sababu ukubwa wa kundi ndiyo faraja ya kundi na wanaijua mchezo.

Unatoka mwenyewe, na unapotoka kubali kuonekana wa tofauti kwa sababu siyo kawaida kwa wengi wetu kutoka nje ya kundi. Nje ya kundi Kuna namna nyingine tofauti ya kuona tofauti na kuona ukiwa ndani ya kundi.

Kundi lina joto na faraja, ila upekee unaondoa pumbazo na kuibua nidhamu ya uwajibikaji. Wajibika kwa maisha yako kama asili inavyotufunza. Kwa mfano, Mama anapomnyonyesha Mtoto hamsaidii Mtoto huyo moja kwa moja kukua, miwili wa mtoto wenyewe hujijenga na kukua.

Jamii, Dini, Elimu ni kama mfano wa Mama anayenyonyesha lakini suala la ukuaji wa mtoto lipo ndani ya Mtoto mwenyewe. Ni hakika inawezekana kutoka nje ya kundi na kulitazama kundi kipekee huku ukiubeba wajibu wote wa uwepo wako.

Kumbuka unayeishi ni wewe na ukiondolewa kila ulichojifunza au kuaminishwa utabaki wewe. Wewe(Mimi) ndiyo wenye jukumu kuu la uwepo wetu.
 
Back
Top Bottom