Tokea afe Horace Kolimba cheo cha Katibu mkuu wa CCM kimekuwa kama hakina Baraka

Tokea afe Horace Kolimba cheo cha Katibu mkuu wa CCM kimekuwa kama hakina Baraka

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jaribu kuwafuatilia Makatibu Wakuu wa CCM walioteuliwa baada ya Horace Kolimba kukutwa na yaliyomkuta utawaona ni kama wamevurugwa kwa namna fulani.

Yaani shukrani ya chama kwao huwaga kama ni " mateke"

Niwakumbuka akina mzee Gama R.I.P baadae Nchimbi akamvuruga, kuna huyu mzee wetu Mangula alirudi Ilembula kuuza nyanya, kuna yule Makamba sr haijulikani yuko Madale kwa Diamond au Bumbuli, yupo pia Dkt. Wilson Mkama nadhani ni mjasiamali kwa sasa, tunaye mzee wetu maarufu Komredi Kinana ambaye nusura atimuliwe chamani baada ya kurekodiwa na mwisho yupo Komredi Bashiru ambaye yuko bungeni kwa sasa.

Kiufupi safari ya Katibu Mkuu wa CCM huwa ngumu na iliyojaa mashaka kama ya Katibu mkuu wa Yanga.

Mungu Ibariki CCM

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Watakapoacha makundi au kumchagua mtu ambaye ni neutral hicho cheo bado kitayumba tu sana.
 
Nilisikia Kolimba...... ngoja niache tu nimezee tu bado natakiwa kuwa President
 
Mtoa mada ni shabiki wa simba ndiyo maana mwisho wa uzi wake kaipondea yanga kiaina.

Wana jangwani mnasemaje juu ya hili?
 
Lakini aliyepata kizaazaa kikubwa kuliko wote ni aliyekuwa katibu wa kipindi cha mwendazake...

Anguko alilolipata ni kama tembo kujirusha na kudondoka toka kwenye ghorofa ya 30.

Hivi sasa yuko kapu moja na Halima Mdee.
 
Huyu ndio walau kafaidika maana atakula pensheni ya Katibu mkuu Kiongozi hadi atakapokufa!
 
Lakini aliyepata kizaazaa kikubwa kuliko wote ni aliyekuwa katibu wa kipindi cha mwendazake...

Anguko alilolipata ni kama tembo kujirusha na kudondoka toka kwenye ghorofa ya 30.

Hivi sasa yuko kapu moja na Halima Mdee.
Kwa hiyo Bashiru na mzee Mdee wote wapo kwenye kapu moja?
Yaani wote ni wabunge wa viti vya dezo vya hisani ya mtawala na watakuwa wanagonga meza tu!
 
Back
Top Bottom