Tokyo, Japan: Alphonce Simbu ashinda Medali ya Dhahabu ya kwanza nchini kwa kushinda mbio za Dunia za Marathoni

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mtanzania Alphonce Felix Simbu ameshika nafasi ya kwanza na kushinda Medali ya Dhahabu katika mbio za Marathoni Kilometa 42.195 upande wa Wanaume katika mashindano ya Dunia ya World Athletics Championships 2025 akimshinda Mjerumani Amanal Petros.

Simbu ametumia Saa 2:09:48 akipishana na Petros kwa sekunde 3 ambapo Mjerujumani huyo amepewa Medali ya Fedha. Walioshika nafasi zilizofuata ni Iliass Aouani wa Italia (2:09.53) na Tim Vincent wa Australia (2:20.12).

Medali ya Simbu ni ya kwanza kwa Mtanzania kushinda katika michezo hiyo ya World Athletics Championships.

Your browser is not able to display this video.

​
 
Write your reply...hongera sana mwanayanga mwenzetu ambae pia ni kada nguli wa ccm
 
Hongera nyingi kwake! Ila nimeshangaa siwaoni akina Kipchoge!!
 
Hao jamaa walikua mguu kwa mguu, wamepishana chini ya sekunde 3.
 
Wazungu Kwa wivu utasikia kapimwa mkojo umeoneka anatunisha misuli

Hongera zake
 
Safi sana.

Kaiheshimisha nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…