Tokyo, Japan: Alphonce Simbu ashinda Medali ya Dhahabu ya kwanza nchini kwa kushinda mbio za Dunia za Marathoni

Mkuu umekosea hapo kwenye sekunde tatu, nadhani hizo ni nanoseconds, maana ukiangalia walikuwa karibukaribu kabisa
 
Ndio maana tunawaambia CCM imefanya mengi mazuri na hamkubali.

Kidumu chama Cha Mapinduzi
 
Nachukua fursa hii kumpongeza Mama samia kwa Simbu kushinda mbio
 
Hongera kwa Simbu, ila hizo sio sekunde tatu, ni 0.03 seconds
 
Watu wanaoshindaa hivi hukuti makelele makelele ya siasa yaan ikiingia tu makelele makelele ya siasa unarogwa hushindi hata stars hili kombe la juzi wangeenda kimya kimya wangechukua ila dah hongera kwake Simbu
..na hasa ukiambatana/fungamana na viongozi wa hiki chama chakavu..wana LAANA
 
Historia imeandikwa huko Tokyo. Kwa muda wa masaa 2:09:47 huko Tokyo, Japan mtanzania Alphonce Felix kaipeperusha vyema bendera na kujipatia medali ya dhahabu. NI BINGWA WA DUNIA WA MARATHON KWA SASA. Hili ni jambo kubwa na heshima kwa nchi ya Tanzania.

Pamoja na kuiletea nchi heshima ila pia kwa sasa thamani ya Alphonce imeongezeka. Mkataba wake na Adidas huenda ukaboreshwa zaidi na pia kusaini mikataba mingine mipya na kampuni zingine. Na kwa sababu ni staa atazidi kulipwa pesa ndefu za appearance fees kwa mbio atakazoshiriki. Kama kawaida huko jeshini nako watamwandalia kazawadi. Amiri jeshi mkuu Dr Samia naye lazima atampa zawadi.

Achana na kina Diamond, Harmonize, Mwijaku... huyu Alphonce ndo supastaa wa ukweli wa kimataifa tuliye naye. Kwa leo tayari CNN, BBC, Supersport, Fox News, Reuters na vyombo vingine vikubwa vya habari duniani vimeshapost suala lake.
 

Attachments

  • 17579282711210.mp4
    6.7 MB
  • VID_20250915_022019_455.mp4
    28 MB
  • IMG-20250915-WA0095.jpg
    72.6 KB · Views: 23
  • IMG-20250915-WA0096.jpg
    61.4 KB · Views: 21
  • IMG-20250915-WA0094.jpg
    71.8 KB · Views: 21
  • IMG-20250915-WA0093.jpg
    106.3 KB · Views: 23
  • VID_20250915_022019_455.mp4
    28 MB
  • 17579282711210.mp4
    6.7 MB
..na hasa ukiambatana/fungamana na viongozi wa hiki chama chakavu..wana LAANA
Mwakinyo aliposhinda kipindi kile kule Uingereza km sijakosea alienda kimya kimya hakuna aliejua mpaka aliposhinda ndio sasa watu wakajua na siasa zikaanza kuingia hapo, yaan hata Olympic mashindo yale watu wakienda bila siasa siasa ushindi huu hapa sema siasa zikiwekwa mbele wanasiasa wanataka wasifiwe wao wakati watu wanachafuka majasho kupambania ushindi wao wanaleta siasa zao za kiduanzi duanzi, weka fungu wape fungu waende kimya kimya siasa zikae pembeni watu lazima washinde ila makelele makelele ya siasa yakiwa mengi watu wanarogwa hawashindi ng'o
 
Natuma nafasi hii kumpongeza Mama Samia kwa simbu kushinda mbio
Umeona huu ungese huu ndio maana watu wanazila wanaamua bora wasishinde tu, kupambana apambane Simbu pongezi apewe mwingine WTF is this?
 
Umeona huu ungese huu ndio maana watu wanazila wanaamua bora wasishinde tu, kupambana apambane Simbu pongezi apewe mwingine WTF is this?
Hata wewe sahivi tukikuona umetuwakilisha vizuri kimataifa tutampongeza Mama samia utake usitake hata kama hatujui umefikaje huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…