Hivi karibuni, kampuni kubwa ya mawasiliano na teknolojia ya China, Huawei, ilifanya mauzo ya awali ya simu yake mpya ya kisasa (smartphone) aina ya Huawei Mate 60 Pro, hatua iliyozusha mjadala mkubwa katika jamii ya Wachina, ikiwa ni tofauti na hali inavyokuwa wakati wa kuzindua bidhaa mpya.
Ikiwa ni kampuni ya China iliyoathiriwa zaidi na vizuizi vya Marekani, Huawei, baada ya kuvumilia kipindi kigumu, inakabiliwa na changaoto mpya ya kutatua kiini cha matatizo ya kukosa chip zinazoweza kuendana na teknolojia ya 5G. Suala hili linachukuliwa zaidi kama ishara muhimu ya shinikizo la uwezo wa kampuni za teknolojia za China katika eneo hilo ambalo lina ushindani mkali na ukandamizaji unaofanywa na Marekani.
Wakati Huawei imeendelea kufanya mambo yake kimya kimya na haijaweka wazi mambo yaliyomo katika teknolojia ya Huawei Mate 60 Pro, matarajio na matamanio makubwa ya jamii ya Wachina kuhusu ‘kurejea kwa Kirin’ kunaonyesha hamu kubwa na uaminifu katika sekta ya utafiti wa teknolojia na maendeleo nchini China.
Watu wengi wamgundua “kulingana,” ambako ni muda wa kutolewa kwa toleo jipya la bidhaa ya Huawei ambao umeendana na ziara ya Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raiomondo nchini China. Hapa inafaa kuzingatia kuwa, vizuizi vingi vya Marekani dhidi ya China katika sekta ya teknolojia ya juu vinatekelezwa kupitia Wizara ya Biashara, na mpaka sasa, bado kuna mamia ya kampuni za China katika orodha yao ya viwanda. Bila ya kujali dhamira ya Huawei, kuzindua simu hiyo ya Mate60 Pro kumechukuliwa na Wachina wengi kuwa na maana ya kina Zaidi ya ‘kuibuka kutoka chini ya shinikizo la Marekani.’ Haifahamiki kama Bi. Raimondo alifuatilia sauti hizi wakati wa ziara yake hapa China, lakini inaaminika kuwa sauti hizi zinapaswa kusikiwa naye na Wamarekani wengi Zaidi, na kuwa na athari katika msimamo wa Marekani!
Kwanza, tangu kuanzisha vita ya kibiashara na China mpaka vita inayoendelea ya kiteknolojia, Marekani, licha ya kubadili mwelekeo wake, inatumia njia za kimwamba kuikandamiza China. Sasa, kadri vitendo vya nchi hiyo vinavyokuwa havina mantiki, ndivyo vinavyovhovhea Zaidi ustahamilivu wa jamii ya Wachina, kusimama pamoja na kukabiliana na matatizo. Vita ya kibiashara, bila shaka imeshindwa kidhahiri, na sasa, wakati vita ya kiteknolojia ikiendelea na Marekani ikidumisha nafasi yake katika sekta ya teknolojia ya juu, kasi ya ari ya Wachina kusonga mbele licha ya shinikizo, na nguvu kubwa ya kimaadili, ni vitu ambavyo Marekani haiwezi kukabiliana navyo.
Pili, ni wazi kwamba kampuni za China zitapenya vizuizi hivyo na kusonga mbele, na haya ni matokeo ya maendleo ya jumla ya China na maingiliano ya karibu na maskahi ya kimataifa. Katika zama hizi za utandawazi, wazo la kuziondoa kampuni za China kwenye mnyororo wa uzalishaji litakabiliwa na upinzani mkali kwa kuwa linakwenda kinyume na sheria ya maendeleo. Kuibuka tena kwa simu za kisasa za Huawei baada ya miaka mitatu ya kulazimishwa kuwa kimya kunatosha kabisa kuthibitisha kuwa ukandamizaji mkubwa wa Marekani, umeshindwa.
Tatu, ‘vita’ kati ya China na Marekani inawezekana kabisa kuepukwa. Maendeleo na ukuaji wa kampuni za China na soko la China vinaweza kuwafanya baadhi ya Wamarekani kuwa na hofu, lakini wakati huohuo, hatua hii inaweza kutoa fursa nyingi Zaidi. Moja ya lengo kuu la ziara ya Bi. Raimondo ni kulinda maslahi ya kampuni za Marekani, lakini hata hivyo, wafanya maamuzi wa Marekani wanapaswa kufikiria upya kama wanataka kujiumiza katika mvutano wa ‘maisha ama kifo’ au kutafuta nafasi Zaidi katika ushirika wa kunufaishana wa mgao wa kazi duniani na kupata faida kubwa Zaidi.
Zaidi sana, Wachina hawana tena matarajio yoyote ya mabadiliko makubwa kutoka upande wa Marekani, lakini kama Marekani itaacha udhibiti wake uliokithiri na ushindani usiofaa dhidi ya China, jambo hilo litakaribishwa sana na China.