mkuu inaongeza gharama kwa nani raha ya maana ya kitu hufurahiwa na wahusika sio watu wengine. kwa waafrika ina maana kwa wengine inaweza kuwa ujinga. kwani john walker tukilitafsiri kikwetu litakuwa zuri? bush je? waache watu wajinafasi kwa mila na desturi zao.
kwa waliosoma symblolic interactionism wataelewa sana kuwa kila kitu kina maana kwa watu fulani na kwa watu wengine inaweza ikawa ujinga mtupu. ndio maana tunajifunza kuchukuliana na kuheshimiana kwa kile ambacho wengine wanakiamini kuwa kizuri kwao. ili mradi tu isivunje miiko ya ujumla ya kidunia.