Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Watanzania wamekuwa wakidanganywa sana na Wanasiasa wakiwemo Chadema, Mwendazake nk kwamba Nchi yetu ni tajiri sana hapa Afrika ingawa kiuhalisia sio Kweli.. Mbona kweli list hapa ya utajiri haipo?

Kwa mujibu wa jarida la economist intelligence Nchi 10 Zenye Utajiri wa Madini hapa Afrika ni zifuatazo

1.South Africa
2.Nigeria,
3.Algeria,
4.Angola,
5.Libya,
6.Egypt,
7.Ghana,
8.DR Congo,
9.Gabon,
10.Zimbabwe.

Sasa kama Tanzania hatumo kwenye hiyo list utajiri ambao huimbwa na Wanasiasa ni upi?
Maana hata kama ni Ardhi nzuri ya Kilimo hatuwezi ifikia South Sudan, Angola, Zambia, DR Congo nk.

Hivi utajiri wa Tanzania hasa ni upi? Au tafsiri ya Utajiri inayosungumzwa ni ipi hasa?

Lete ya kwako
Wataalamu wanasema mpaka muda huu Tanzania imeshachima asilima 10% tu ya madini yote, na karibia nchi nzima ina mali kiasi kwamba ukitaka uchimbe kila kitu itabidi uwahamishe watu baadhi ya maeneo. Pale Mwadui zilipo nyumba za mgodi, inasemekena pale kuna mali imetulia
 
Kama Madini yapi unayoyajua wewe Yako Tanzania? Acha porojo ingekuwa hivyo settlers wa kizungu wangeshakuwepo miaka Mingi sana kama South Africa, Zimbabwe, Angola, Nigeria, Algeria nk..

Tanzania hakuna Madini yeyote ya maana ni ubangaizaji tuu.

Hizo Nchi kwenye list hapo Zina Madini sio mchezo,Zambia haipo ni Kwa vile Ina aina mbili za Madini tuu zinazopatikana Kwa wingi japo sio wingi wa kama Congo na Zimbabwe.
 
Source ya list tajwa kwanza. Siikatai list, ila nakataa Tanzania kuwa si miongoni mwa hiyo list. Wabongo fake sana. Tuseme kwa mfano, Tanzanite ipo kwenye nchi gani nyingine?
Tanzania haipo kwenye list, hakuna Madini ya maana hapa Tzn..

Ni sawa na tumafuta twa Uganda ambato Tunaenda kuisha baada ya miaka 20.
 
Tanzania haipo kwenye list,hakuna Madini ya maana hapa Tzn..

Ni sawa na tumafuta twa Uganda ambato Tunaenda kuisha baada ya miaka 20.
Muanzisha thread amekosea possibly alimaanisha rasilimali zilizo kwenye ardhi ikiwa ni pampja na mafuta. Ebu labda ujaribu kunipa facts za madini kwa nchi za Egypt na Libya
 
Kama na congo imeponea chupuchupu kuwepo kwenye list alaf bado uniambie niiamini hyo data
Congo Ina Madini ila sio kuzizidi hizo Nchi tajwa..

Algeria ndio Ina gas asilia nyingi kushinda Nchi zote hapa Afrika na inafanya utaratibu wa kulisha Ulaya, yaani Iko top 10 ya Dunia.

Sasa Congo itaisidi nini Nigeria? Copper na Cobalt au?
 
Muanzisha thread amekosea possibly alimaanisha rasilimali zilizo kwenye ardhi ikiwa ni pampja na mafuta. Ebu labda ujaribu kunipa facts za madini kwa nchi za Egypt na Libya
Mafuta sio Madini? Ukiacha mafuta Kuna gas na aina zingine za Madini..

Kama una mashaka na List Anza ku google Nchi Moja Moja..

Kwa taarifa Yako Nchi za kijasusi zilishafanya utafiti kitambo sana Kwa hiyo Wana taarifa za kutosha.
 
Back
Top Bottom