Top 10 ya nchi zenye utajiri wa madini Afrika, Tanzania haipo

Acha hadithi wewe,Madini ya kubangaiza na wachimba sululu wakitorosha ni sawa..

Tanzania ina Madini ya kubangaiza bangaoza ndio maana inabembeleza investors ila tungekuwa nayo wangejileta wenyewe kama hizo Nchi zingine.
Hujui ila unajikuta unajua, uliza tulopitia kazi ya madini!! Nyie ndiyo mnaifelisha nchi kwa ujuaji wakijinga sasa kaa na ujinga wako
 
Kuna Utofauti baina ya "Mineral producing" na "Mineral reserve"

Inawezekana nchi ikawa na madini machache ila ina technology kubwa ikachimba mengi kwa haraka

Ukiangalia Hio list nchi nyingi za Juu Zina Mafuta ama Technology.

Tanzania Kuna madini hata hayachimbwi mfano mchuchuma, na ni Nchi ya 4 Africa kwa Dhahabu, pia Nchi pekee Duniani Yenye Tanzanite, Nchi pekee Africa Yenye Maziwa yote Makubwa, Kuna Almasi, Shaba na Rasilimali nyengine kibao.
 
Hebu muelewe ni kwamba hizo nchi wazungu au walitoa hizo takwimu wamepata nafasi za kuchunguza ila kwetu ardhi kubwa haijafanyiwa uchunguzi.

Pia wanavigezo lbd kuangalia mauzo ya nchi lkn huku zinapeperushwa nchi nyenginezo na sifa wanapata wao.
 
Kumbe mambo ya kusemekana. Tanzania ina madini ya kawaida sana, hata haina mafuta ya kutisha na kwenye gesi vilevile haipo top 5 ya nchi zenye reserve kubwa ya gesi.
Mambo ya unaambiwa, inasemekana hayajawahi kuwa facts
 
Nadhani umeshindwa kujua hiyo orodha ya nchi inahusu nini hasa!

Ni kwamba hukusoma vizuri kichwa cha habari ukakielewa kinahusu nini:

Kinasema "Mineral Producing Countries"

Pamoja na kwamba tayari nasi tunatoa madini, lakini kiwango chake hakijafika kwenye kiwango kinachaangaliwa na hiyo wanayoiangalia hao waliyoleta hao waliyoileta hiyo taarifa.

Sisi bado hatujachimbua gesi na kufaidika nayo.

Nchi kama Msumbiji, wakiweza kutumia gesi ile vizuri na kuingiza pato, huwezi kuona wakiwa nje ya orodha hiyo

Lakini utajiri wa nchi hautokani na madini pekee. Nchi kama Korea Kusini hawana madini, lakini ni matajiri.
Sisi hapa kutegemea madini kujigamba kwa utajiri ni kukosa akili kichwani. Tunayo fursa kubwa sana kuwa matajiri kwa kutumia ardhi yetu vizuri, lakini viongozi wetu hawalioni hilo.
Wanachokiona wao zaidi ya chochote, ni kutembea duniani tukiwalilia watu toka huko nje waje hapa kutuletea maendeleo!
Hii ni akili ya ajabu sana.
 
Ndio Zenye Madini hizo nyie wengine ni wababgaizaji..

Pale Zimbabwe Mchina Katia Mgodi wa Til.4 wa Lithium,Tanzania una Mgodi upi wa thamani hiyo Kwa mfano?
Unasema kweli hayo ya Zimbabwe na hiyo Tr4?

Hii inaweza kuwa sababu kwa nini hao wengine wamekazana na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi!
 
Kwani hiyo orodha unajua nani katengeneza? Unajua tofauti ya kutoa/kuzalisha madini kwa wingi na kua na madini kwa wingi?
Sasa cheki orodha ya nchi zenye madini kwa wingi utaona tanzania kwenye namba 8. Ikiipita botswana kwenye namba 9. Pia tanzanite ikitajwa kupatikana tanzania peke yake.
 
Kumbe mambo ya kusemekana. Tanzania ina madini ya kawaida sana, hata haina mafuta ya kutisha na kwenye gesi vilevile haipo top 5 ya nchi zenye reserve kubwa ya gesi.
Mambo ya unaambiwa, inasemekana hayajawahi kuwa facts
Wataalam wanaokuzidi wewe utaalamu ndiyo walwahi KUNIAMBIA hivyo, NDIYO MAANA nikatumia NENO inasemekana kwa sababu mwenye proof siyo mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…