Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,414
- 2,181
TAMWA wanatafsiri Ukatili wa kijinsia kuwa ni kitendo anachofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono na kiuchumi. Hata hivyo tafiti nyingi zimeonyesha kwamba wanawake ndiyo wahanga wakuu wa ukatili wa kijinsia.
Tukimjadili mwanamke zaidi na mtoto, makundi 5 yameibuka kidedea wa kumnyanyasa mwanamke na mtoto, huku picha ya wazi wakionekana kumtetea.
Moja: Wana kampeni ya mahusiano ya jinsia moja (LGBT)
Anza na swali rahisi tu kwa wana kampeni, wazazi wao wasingechanganya jinsia, wao wangekuwepo? Swali hili nawauliza wasichana wanaoniomba ushauri kwamba wanaplan wawe single mother, namuhoji umekuzwa na wazazi wako wote wawili au walezi wawili wa kike na kiume. Anasema ndiyo.
Namuuliza tena, rafiki zako walokuzwa na mzazi au mlezi wa jinsi moja pekee wanasemaje? Anajibu huwa hawana furaha. Hapo nammalizia swali la mwisho, kwa hiyo unataka mwanao akose furaha maisha yote kwa starehe yako ya miezi michache?
Hahiitaji tafiti kujua sense ya kila nchi imeonesha wanawake wakiwazidi wanaume kiidadi, hapo hapo kuna kundi linapambana kunyofoa hao wanaume wachache kuwageuza dume jike, hapo mwanamke anaongezewa ugumu mara mbili wa kumpata mwanamke wa kumuoa ma kulea pamoja watoto.
Hivyo mwanamke na mtoto watanyanyasika mnoo kadri kampeni hii chafu inavyopata muitikio.
Mbili:Watunga sheria na wasimamizi (law enforcers)
Madhara ya kumpeleka mtu mahakamani kabla ya upelelezi kukamilika ni pamoja na kumuumiza kwa kumharibia heshima yake na kuifanya familia yake kuishi kwa wasiwasi wakati wote hasa mwanamke na mtoto wa Yule alotuhumiwa kwani ni tofauti na msiba ambapo ndugu hukaa kujadili, kwenye kesi hufkiri atarudi mara moja kama walivyomwambia wakati wanamfuata mtuhumiwa.
Na pale ambapo ushaidi unapatikana, mara moja muhalifu akamatwe ,na hasa zama hizi za teknolojia. Kwa mfano Zanzibar wamefunga karibu mji mzima CCTV kamera, ina maana kama kuna kosa la jinai linafanyika, serikali inakwenda kwenye CCTV itakupata tu kwa urahisi badala ya kutumia mfumo wa zamani wa kumtafuta mtu.
Tatu: Wasimamia usaili na mitihani (Interviewers and lecturers)
Mwaka 2020, TAKUKURU walifanya tafiti suala la ruswa ya ngono pale UDSM na UDOM , walikuja na sababu kadhaaa ikiwemo ukosefu wa maadili na ushawishi wa mtu mwenye madaraka.
Hali hiyo pia pia iko makazini.
NINI MATOKEO
Anaachwa mwanamke mwenye uwezo wa kuzalisha zaidi (productive) kazini na nafasi kupewa mwanamke mwenye uwezo hafifu ila mwepesi kutii tamaa za bosi asiyejiheshimu.
Kwa hiyo wanawake wenye uwezo darasani na makazini watawaambia mabinti zao pia, wasitarajie uwezo pekee kuwapa nafasi.
Kiuchumi mwanzo atayumba, japo ana nafasi ya kujiajiri na kuonesha uwezo wake.Kisaikolojia mwanamke atajiona ni chombo cha starehe zaidi kuliko kiumbe mwenye hisia.
Nne: Waganga na Manabii feki(Witch doctors )
Kundi hili hukuza tatizo kwenye akili ya mgonjwa hasa wa kike. Humuweka clinic ya kwenda na kurudi, akipangiwa tarehe kama hospitali ya rufaa.
Kibaya huhusisha uzinzi kama sehemu ya masharti mwanamke kupona. Atakayekataa kwa hiyari, wapo waganga na manabii walowalewesha kwa madawa ya kulevya wateja wao na kuwaingilia kasha wakizinduka husingia nguvu za uponyaji zimemwingia.
Ukiona mke hakauki kwa kundi hili ,jua uko hatarini kuambukizwa maradhi mabaya mabaya.
Ni hivi karibuni kampeni ya kuwafichua imeanza kueleweka, ndipo hupata kesi ya kubaka na kunajisi.
Tano: Wasanii
Japo liko mwisho kimpangilio ,ila ndilo kundi linaloongoza kudhalilisha wanawake.
Tangu utotoni tukikua aina za video ni zile zile huku zikiongezwa udhalili zaidi ambapo nyingi ya video zao ,wanawake wapo karibu na uchi , na wanaume wao Wana suti).
Ni rahisi msanii kutafuta kiki ya kupanda chati kwa kujitangaza wanawake walotembea nao Kwa maneno au kuvujisha video.
Kuelekea kumtetea mwanamke kiuchumi, kimwili na kisaikolojia , jamii iyatazame makundi haya kwa jicho la tahadhari.