Top CCM leader secretly funding opposition party

Top CCM leader secretly funding opposition party

Tina,
Hivi anayekaa hotelini ni Prof. Lipumba nini?
Kama ni huyo, basi nabadili URAIA na UKABILA. Au itabidi nianze kutafuta kithibitisho kuwa Lipumba SI MNYAMWEZI. Kama Mirambo akifufuka leo, basi huyu Lipumba atachukuliwa ISELAMAGAZI na Walugaluga, na akifika huko basi watapiga hadi mifupa ionekane.

LIPUMBA UNATUTIA AIBU KAKA YETU. Kama mambo magumu, nenda tu UDSM ukafundishe na uachane na haya MATAPISHI. SHAME ON YOU.

BURN: Huyu kaka yetu, vijana wa CCM Tabora, CCM Tabora, kwa kweli itatufanya milele tubaki na umasikini wetu, Wanyamwezi siye. Sijui tumelaaniwa nini?

"LIPUMBA veve, lekaga ikuluye kulya vya vantu, vilakufumile mu-nyindo."

Sikonge, ninavyojua mimi si Lipumba, ila yeye anabariki na ananufaika kwa kiwango cha juu. Hiyo si siri na wengi pale CUF wanajua. Mtu anayekaa hotelini ni kutoka Zanzibar, na ni mtu anayeheshimika sana. Sijui nchi imeingiwa na mdudu gani jamani. Hii inatisha sana. Labda Tina ana zaidi ya hivi
 
Nikiwaambia watu vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanzaga hivi huwa wanapuuzia eti kwa kuwa mmakonde kolewa na mhaya.

Haya!
 
Last edited:
Haya ndo maneno ya Mhe. Lwakatare ndani ya CUF

Mhe. Mwenyekiti na waheshimiwa Wajumbe. Mimi Wilfred Muganyizi Lwakatare ni binadamu kama binadamu wengine, bila shaka nina mapungufu yangu kama binadamu wengine walivyo.

Najua wako viongozi, wanachama na watu wengine niliowakwaza, kuwaudhi, kuwakera, kuwakasirisha, kutowaridhisha, n.k. kipindi nilichokuwa Naibu Katibu Mkuu. Kwa unyenyekevu mkubwa naomba hao wote wanisamehe kwa moyo mkunjufu. Hayo niliyoyafanya na yakawa hayakuwafurahisha sikuyafanya kwa kudhamiria. Wakati mwingine ni uwajibikaji wa kazi.

Mhe. Mwenyekiti jana na leo, nilipokuwa nikichangia na kuhoji ndani ya baraza hili kama mjumbe na hasa suala la fedha za mkutano mkuu ambazo hazikupatikana toka kwa mfanyabiashara mmoja tuliyewekeza naye, suala la kutoendelea na utaratibu wa kuifanya SIRI ya viongozi wa juu tu mikataba ya uwekezaji tunayoifanya na baadhi ya wafanyabiashara na hatari iliyopo kwa utaratibu huo, na pia suala la kutoridhishwa na namna Chama kisivyo na utaratibu mzuri wa "Kuwaenzi na kuwaheshimu" viongozi wanaomaliza kipindi cha kukitumikia Chama (hususani kama nilivyotendewa mimi) mmoja wa Wajumbe niliokuwa nimekaa nao karibu aliniomba na kunisihi nipunguze kidogo "ukanyagaji mafuta" Mhe. Mwenyekiti, Kwa wajumbe wanaonijua vyema tangu huko nyuma nilipokuwa Mwenyekiti wa CUF mkoa wa Kagera, Mjumbe wa Kamati Kuu
ya Chama Mwenyekiti wa kamati mbalimbali za chama za kushughulikia majukumu mbalimbali n.k. hawawezi kushtushwa na namna au "Style" yangu ya ujengaji na uwasilishaji hoja. Kabla sijawekwa hapo mbele meza kuu kama Naibu Katibu Mkuu ndivyo nilvyokuwa. Sipendi masihala katika kazi ya watu.
 
Vyama ambako RA ni mwekezaji ni NCCR Mageuzi, CUF na TLP, lakini alipo na nguvu nyingi ni CUF.

Hivi kweli nani alimuua CHACHA Wangwe? Halafu ni nani alitumwa Tarime kusambaza sumu kuwa Mengi na Mbowe ndio wauaji? (JIWE LA KISOGO). Isitoshe alikwenda Tarime kutumikia deni la shilingi ngapi? km vile milioni 3 au? Ha haha nimekumbuka mzee wa Magabachori aka, mzee wa suspender au ukipenda Mchungaji.....
 
Ah! huu ni ugomvi wa Bw. Mengi tu usioisha. Nani asiyefadhiliwa katika dunia ya leo. Tuwe makini jamani. Tusijeingia kwenye vita vya panzi!
 
Ah! huu ni ugomvi wa Bw. Mengi tu usioisha. Nani asiyefadhiliwa katika dunia ya leo. Tuwe makini jamani. Tusijeingia kwenye vita vya panzi!

Msianze kumparula Mengi bure, kwani hotelini hamna mtu? kwani pesa hawajachukua?

Mimi nilivo soma maoni ya Lipumba kuhusu Dowans, na saga la mafisadi papa, na nikakumbuka Lipumba alivo kuwa moto wa kuotea mbali enzi za ndege ya raisi na rada, I smelt something fishy!
 
Hii ikmwagika hadharani ni kashfa kubwa ya kisiasa hapa nchini na itakuwa pigo kubwa sana -- siyo kwa CCM -- bali kwa upinzani hususan CUF. sasa hivi jawabu la mbili ongeza mbili linakuja vizuri kuhusu Profesa wetu kumbwatukia mzalendo wetu Mengi -- kumbe ni asali anayolambishwa na RA.

Mchongo bila shaka ulikuwa kwa kupitia kwa Jussa.

Na ndiyo maana Profesa aling'ang'ania sana kuendelea na uenyekiti ambapo tulitegemea angesema sasa basi, na wengine waje wenye mbinu mpya za kuing'oa CCM -- achilia mbali kuupata ule "muafaka" ambao sasa ni wa hadithini.

Amekubaliana na usemi kwamba "usipoweza kuwashinda, basi ni bora ujiunge nao." Lakini asingepaswa kuwa yeye kusalimu amri hivyo -- kama alishindwa, basi angewaachia wengine.

Ni aibu kubwa hii kwake, na siyo kwa RA na au CCM kama nilivyotaja kwani mbele ya CCM atajitetea kuwa lengo lake ni kuidhoofisha CUF. Upo hapo Profesa?
 
Vyama ambako RA ni mwekezaji ni NCCR Mageuzi, CUF na TLP, lakini alipo na nguvu nyingi ni CUF.

Hivi kweli nani alimuua CHACHA Wangwe? Halafu ni nani alitumwa Tarime kusambaza sumu kuwa Mengi na Mbowe ndio wauaji? (JIWE LA KISOGO). Isitoshe alikwenda Tarime kutumikia deni la shilingi ngapi? km vile milioni 3 au? Ha haha nimekumbuka mzee wa Magabachori aka, mzee wa suspender au ukipenda Mchungaji.....

Ni hapo sasa.....mambo hadharani... Hata Chadema fisadi Rostam alimnawisha mtu.... ... Zitoooo..... Zitoooo..... Zitoooo.....Zitoooo..... Zitoooo..... Zitoooo.....Zitoooo..... Zitoooo..... Zitoooo.....Mtetezi wa.... Mtetezi wa....Mtetezi wa....Dowans... Dowans.....Dowans... Dowans.....Dowans... Dowans.....
 
Wakuu wa JF heshima mbele,

Nimepitia michango ya wanachama na post zote zilizowekwa hapa, nitangulie kwa kusema michango yote ni mizuri na ninaiheshimu sana, lakini baada ya kusema hayo ningependa kuuliza maswali macheche,

Jee hii haiwezi ikawa ni strategy ya kuwachanganya wananchi juu ya chama gani bora kwa sasa, kwa kuwa tunajua chama kikuu kimepoteza umaarafu na wananchi wengi hawana imani nacho, labda hii ni strategy ya kuwarudishia imani wananchi kuwa japo kuwa chama kikuu kinafanya mambo mengi ya ajabu ajabu lakini hata vyama vya upinzani havina afadhari hata kidogo,
Jee hii haiwezi ikawa ni strategy ya kuhamisha attention ya wananchi ili wasahau mapambano ya mafisadi papa na sasa waanze utafuta mchawi...??

Nijuavyo mimi JF ni jukwaa ambalo shilingi huwa inapande zaidi ya mbili.

MJ
 
"LIPUMBA veve, lekaga ikuluye kulya vya vantu, vilakufumile mu-nyindo."

Hii ni External Service ya Radio Sikonge, Tabora. Kwa wale ambao hawakuelewa, kijana anamuasa Lipumba aache kula vya watu, maana vitakuja kumtokea puani.

OFF TOPIC
Mkuu nimekukubali kwamba wewe ni wa Sikonge original!
 
Wakuu wa JF heshima mbele,

Nimepitia michango ya wanachama na post zote zilizowekwa hapa, nitangulie kwa kusema michango yote ni mizuri na ninaiheshimu sana, lakini baada ya kusema hayo ningependa kuuliza maswali macheche,

Jee hii haiwezi ikawa ni strategy ya kuwachanganya wananchi juu ya chama gani bora kwa sasa, kwa kuwa tunajua chama kikuu kimepoteza umaarafu na wananchi wengi hawana imani nacho, labda hii ni strategy ya kuwarudishia imani wananchi kuwa japo kuwa chama kikuu kinafanya mambo mengi ya ajabu ajabu lakini hata vyama vya upinzani havina afadhari hata kidogo,
Jee hii haiwezi ikawa ni strategy ya kuhamisha attention ya wananchi ili wasahau mapambano ya mafisadi papa na sasa waanze utafuta mchawi...??

Nijuavyo mimi JF ni jukwaa ambalo shilingi huwa inapande zaidi ya mbili.

MJ

fafanua zaidi nani anayofanya hayo?

Suala la CUF kufadhiliwa kisiri na ktk hali ya hatari limesemwa pia na Lwakatare ndani ya kikao cha kamati kuu ya CUF. So, kama ni mtego ni hapo ... kwenye kupokea fedha za Rostam. Si amini kwamba Thisday na Kulikoni wanacheza mchezo wa kutahamisha target. We are still focusing the target. Kama suala hili litaangusha upinzani ni vema tu ili liwefundisho kwa hapo baadae, na ili tupate wapinzani wa kweli.
 
Ni hapo sasa.....mambo hadharani... Hata Chadema fisadi Rostam alimnawisha mtu.... ... Zitoooo..... Zitoooo..... Zitoooo.....Zitoooo..... Zitoooo..... Zitoooo.....Zitoooo..... Zitoooo..... Zitoooo.....Mtetezi wa.... Mtetezi wa....Mtetezi wa....Dowans... Dowans.....Dowans... Dowans.....Dowans... Dowans.....
Mkuu humtendei haki mpiganaji wetu.Yeye Zitto na mimi nikiwemo tuliogopa athari za nchi kuingia gizani na jisi mustakabari wa uchumi wa nchi utakavyoathirika.Mimi ni mwenyeji wa kyela na mwanachama wa CHADEMA,nilikuwa shuhuda kukatika kwa umeme kule Mbeya kwa mda wa miezi miwili.Athari yake ikwa mbaya kwa wajasirimali wadogo.Hawa ni kama vile waziba pancha za magari,wachomeleaji,waendesha saloon n.k.Katika tukio lile sitasahau wajasirimali walivyosumbuliwa na Micro-credit Lenders wengi wao walinyang'anywa vitendea kazi walivyopata kutoka asasi hizo.
Uzalishaji uliathirika na kazi ndogondogo za kuajiri vijana wabangaizaji zikasitishwa,sikilizia nondo zilivyoanza kutembea kuanzia saa 2 usiku.Usalama kwa wakazi wa Mbeya ukawa umetoweka na mpaka ninapoandika ujumbe huu kwenu hali ya matembezi usiku jiji la Mbeya si nzuri.
Kwa hiyo ndugu usikimbilie kutoa hukumu kwa wenzako bila kufanya utafiti.Kamanda Zitto anajiamini na yuko tayari kusimamia hoja zake sio hao mashujaa wako wa CCM wanapigania maslahi ya makundi yao na chuki binafsi.Huu wizi wa EPA hawakuuona mpaka pale Zitto alipopokelewa kwa vifijo na matumaini na watanzania baada ya kusimamishwa ubunge kutokana na sakata la Buzwagi.Kuona hivyo,hao mashujaa wenu kwa kutaka kupotosha ndio wakaanza kujitokeza na hisia za kizalendo feki.Ila sisi wenye kufikirisha vichwa vyetu tulijua hiyo trick yao.Kamanda Zitto kaza buti nenda kanoe bongo yako maana ujumbe wako umeongeza akina Zitto wengi hata ndani ya CCM maelfu kwa maelfu.Kamanda Zitto Moto ulioanzisha hautazimwa kwa njia yeyote na wadandia hoja.Hivi punde nimepata taarifa kuwa Mh.Lyatonga kahutubia watu 20 kwenye uzinduzi wake wa kampeni!Aibu kubwa!
 
Mkuu... nimekupata lakini bado sijaridhishwa na maelezo yako kuwa generators za dowans pekee ndio zingetuondolea hiyo kadhia! Why it was dowans only and not else? Halafu Zito alitumia juhudi za ziada kupigania wazo lake!!!
 
Ni mwenda wazimu pekee yake anayeweza kukubali kuwa na mfadhili moja katika kambi mbili za upinzani bila ya kuhoji kulikoni?. Huwezi kufadhili Yanga na Simba kwa wakati moja kwa mapenzi halisi ya klabu hizo zaidi ya nia na lengo la kujinufaisha mwenyewe.

Kama hali ni hiyo katika Tanzania basi bila shaka tumefika mahali pabaya na pa hatari sana na tusione haya kutafuta ukweli katika hili kabla umauti haujatufika ndani ya Tanzania.

Mfadhili huyo anaweza kabisa akagawa silaha pande zote mbili kwa lengo la kuleta machafuko katika nchi ili aendelee kuneemeka zaidi. Ni wakati muafaka wa kumuanika mfadhili huyu ili aache kula kulia na kushoto.
 
Mambo Jambo,

Sina hakika kama mkakati huo una baraka za CCM kama Chama, bali ni mkakati personal wa mhusika mkuu.

Wachangiajie wengi hapa wamesema ni RA, na sijaona watu waliopinga hilo jina. Sisi sote tunafahamu kwamba iwapo Bunge likiwaka moto RA hatapona maana dili kubwa kubwa ambazo ni chafu nyingi zina mikono ya RA na zikianza kuchunguzwa na Bunge anaweza kujikuta anaenda Segerea.

Kinachoangaliwa kwa sasa ni kipindi cha 2010 - 2015 ambacho haijulikani kitakuwaje. Kwanza JK (kama atachaguliwa kuendelea) atakuwa anatumikia kipindi chake cha mwisho na hakuna anaejua atakuja na nini. Maana hapo atakuwa hana haja ya kubembeleza urafiki na baadhi ya watu kwa kuwa hatawahitaji tena. Kwa sasa nina hakika JK anafanya kazi ya ziada kuzima mambo mengi sana ambayo yanamgusa RA na huwezi kujua ataendelea kumlinda mpaka lini.

Kisiasa kwa upande wa Bunge, joto liko juu sana maana hakuna Mbunge ambaye ana uhakika wa kurudi Bungeni awe ni wa upinzani ama wa CCM. Chaguzi ndogo za Kiteto, Mbeya, Tarime na Busanda zimeonyesha kuongezeka kwa ushindani kwa kiwango cha juu, sasa hivi CCM haichukulii for granted kwamba ukiteuliwa kuwa mgombea kupitia CCM basi umeshinda Ubunge, NO.

Tumeona jinsi mawaziri na vigogo wa CCM wanavyohangaika kwenye chaguzi ndogo ili kushinda na wakajikuta wanashinda lakini kwa jasho na kuzomewa juu. Mwakani wakati wa uchaguzi kila mgombea atakuwa jimboni kwake peke yake, hakuna Waziri ambaye ataenda kumpigia debe ama hakuna Tingatinga kwenda kusafisha njia, bali ni juhudi binafsi za mgombea. Kwa hiyo hilo nalo linapunguza possibility ya CCM kuendelea kuwa na numbers Bungeni.

Siku zote siasa ni mchezo wa namba. RA alishaona kwamba CUF already wana numbers Bungeni (viti vyote vya Pemba + viti maalum). Sidhani kama kuna dalili za kwamba CCM itashinda kiti hata kimoja kule Pemba, na hivyo RA is banking on the numbers of MPs from CUF ili kuzima hoja zote zinazomhusu yeye. Lipumba akishasema kwamba Dowans ni safi unategemea Hamad Rashid na wenzake huko Bungeni waseme nini? Watafuata msimamo wa chama na kubariki uchafu.

RA hana hakika kama wale wabunge wote wanao-side na mafisadi wataweza kurudi Bungeni kwa kuwa agenda inayowaumiza CCM sasa hivi ni ufisadi na ukiongea kuhusu ufisadi lazima unafika mahali unamgusa RA. Je, wapambe wake Bungeni wataweza kujenga hoja za kujitetea kwenye kura za maoni na kwenye uchaguzi wenyewe na hatimaye waweze kurudi mjengoni?

Ili RA aendelee kuwa na support kubwa Bungeni, njia pekee kwake ni kuanza kuweka watu wake iwe ni kupitia CCM ama upinzani. Msije mkashangaa iwapo RA ataamua kuwatosa baadhi ya wapambe wake ambao anaona kwamba hawabebeki tena na hivyo kuendelea kuwafadhili ni sawa na kupoteza hela bure. Subirini nominations za CCM zifanyike mtaona jinsi watu wanavyohama vyama na kwenda upinzani na watapewa ufadhili na hao hao mafisadi ili waingie Bungeni kwenda kutetea maslahi ya mafisadi.

Ninashawishika kuamini kwamba kinachofanyika ni personal effort za RA ili apate support na kinga ndani ya Bunge ili asije akasulubiwa iwapo JK atafika mahali akashindwa kumbeba na kuamua kuliachia Bunge. Madudu ya RA tunayoyafahamu yanaweza kuwa machache sana, lakini yakianza kufumka hapa hata JK atafika mahali aseme sasa nimeshindwa, liwalo na liwe. Acha RA ajitetee mwenyewe maana ukibeba mtoto mwenye kinyesi nawe unaweza kujikuta unanukia perfume ya kinyesi mbele za watu na hakuna mtu mwenye ujasiri huo. Akina Mkapa hawapendi kuitwa mafisadi na ndo maana wanajificha hata kwenye functions fulani fulani hawajitokezi maana wamejawa na aibu. Sidhani kama JK anataka kujitengenezea mazingira kama hayo mara baada ya kumaliza ngwe yake ya pili.
 
Ah! huu ni ugomvi wa Bw. Mengi tu usioisha. Nani asiyefadhiliwa katika dunia ya leo. Tuwe makini jamani. Tusijeingia kwenye vita vya panzi!

Usije ukachukulia kila kitu ugomvi, hebu kwanza anza kujiuliza mwenyewe..

  1. Ilikuwaje CUF hawako mstari wa Mbele katika Vita ya Ufisadi unaolitafuna taifa
  2. Ilikuwaje Mh Lwakatare akataja uwekezaji wa mfanyabiashara mkubwa ndani ya CUF?
  3. Kwa nini Lipumba aling'aka sana pale Mh. Mengi alipotaja mafisadi papa?
Wapo wengi wanaofadhiliwa hata TZ enzi za Nyerere ilifadhiliwa...Lakini..
  1. Ufadhili unatoka wapi?
  2. Mfadhili ana malengo gani nyuma ya pazia?
Si kila kitu cha kupokea,

Habari hii ni muhimu, ukifuatilia uchaguzi wa Busanda utapata Jambo ndani ya CCM. Kambi yote ya Rostam, Makamba, Edward Lowassa haikushiriki mchakato wa kampeni.
 
- What a big joke is this, Rostam akifanya ufisadi CCM wote hata rais ni fisadi pia, lakini akisaidia upinzani kwa siri as of this topic ni yeye tu na sio CCM nzima na rais, Ooh mama Tanzania! Mungu akubariki!

- Kuna siku nitaiomba serikali inipe ruhusa nipitishe waya wenye umeme kwenye vichwa vya wananchi wengi, may be wataamuka huu usingizi mzito wa politically naivette waliomo garademuti!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
Kweli fedha ni mwanaharamu, hata Prof. Lipumba ....! kwa njaa zetu hizi vita ni ngumu. Yes, i say again 'Watanzania wengi ni opportunist'
 
Back
Top Bottom