Mkuu humtendei haki mpiganaji wetu.Yeye Zitto na mimi nikiwemo tuliogopa athari za nchi kuingia gizani na jisi mustakabari wa uchumi wa nchi utakavyoathirika.Mimi ni mwenyeji wa kyela na mwanachama wa CHADEMA,nilikuwa shuhuda kukatika kwa umeme kule Mbeya kwa mda wa miezi miwili.Athari yake ikwa mbaya kwa wajasirimali wadogo.Hawa ni kama vile waziba pancha za magari,wachomeleaji,waendesha saloon n.k.Katika tukio lile sitasahau wajasirimali walivyosumbuliwa na Micro-credit Lenders wengi wao walinyang'anywa vitendea kazi walivyopata kutoka asasi hizo.
Uzalishaji uliathirika na kazi ndogondogo za kuajiri vijana wabangaizaji zikasitishwa,sikilizia nondo zilivyoanza kutembea kuanzia saa 2 usiku.Usalama kwa wakazi wa Mbeya ukawa umetoweka na mpaka ninapoandika ujumbe huu kwenu hali ya matembezi usiku jiji la Mbeya si nzuri.
Kwa hiyo ndugu usikimbilie kutoa hukumu kwa wenzako bila kufanya utafiti.Kamanda Zitto anajiamini na yuko tayari kusimamia hoja zake sio hao mashujaa wako wa CCM wanapigania maslahi ya makundi yao na chuki binafsi.Huu wizi wa EPA hawakuuona mpaka pale Zitto alipopokelewa kwa vifijo na matumaini na watanzania baada ya kusimamishwa ubunge kutokana na sakata la Buzwagi.Kuona hivyo,hao mashujaa wenu kwa kutaka kupotosha ndio wakaanza kujitokeza na hisia za kizalendo feki.Ila sisi wenye kufikirisha vichwa vyetu tulijua hiyo trick yao.Kamanda Zitto kaza buti nenda kanoe bongo yako maana ujumbe wako umeongeza akina Zitto wengi hata ndani ya CCM maelfu kwa maelfu.Kamanda Zitto Moto ulioanzisha hautazimwa kwa njia yeyote na wadandia hoja.Hivi punde nimepata taarifa kuwa Mh.Lyatonga kahutubia watu 20 kwenye uzinduzi wake wa kampeni!Aibu kubwa!