Huu ni utafiti(usiokua rasmi) juu ya uwingi wa wazungumzaji wa makabila yaani wale ambao kiasili ni wenyeji wa kabila husika pamoja na wale ambao wamejifunza makabila husika kutokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kimaisha.
1. WASUKUMA
-Idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 10. Ni kabila pekee linalopatikana zaidi ya mikoa 6. Wasukuma (ukijumlisha na matawi yake kama Wanyamwezi, Waikizu n.k) wanapatikana mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Tabora na Kigoma pia.
2. WAGOGO
-Wanapatikana kwa wingi mkoani Dodoma. Pia wanapatikana Morogoro/Gairo(huitwa pia Wakaguru). Mkoani Singida wanapatikana wilayani Manyoni (huitwa Wagogo wa Manyoni). Mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa pia wanapatikana kwa wingi.
3. WANGONI
Ukijumlisha pamoja na Wandendeule na Wamatengo ambao lughazao huendana sana, basi Wangoni wanafanya kuwa kabila la tatu kwa uwingi Tanzania. Wanapatikana Mkoani Ruvuma.
4. WAMASAI
Hawa wanapatikana Mkoani Arusha pamoja na baadhi ya wilaya za mkoa wa Manyara kama Simanjiro na Kiteto.
5. WARANGI
-Ukiwajumlisha pamoja na matawi yake kama Waburunge na Wanguu hawa nao wanapaswa kuingia kwenye top ten.Wanapatikana kwa wingi wilaya ya Kondoa na Chemba. Pia wanapatikana maeneo ya Mpakani mwa mkoa wa Manyara na Dodoma.
List Itaendelea...
NB: NAJUA UTASHANGAA KUTOYAONA MAKABILA YA WANYAKYUSA, WAHAYA NA WACHAGA HAPO JUU, UKWELI NI KUWA KWA KIPIMO CHA UWINGI WANAPWAYA SANA ILA WAMEFANIKIWA KWENYE UMAARUFU NA ELIMU TU.
Karibuni kwa mjadala