Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpendwa usituchanganye, hata Kama ni tax compliant Kama unavyodai, basi bado makampuni yanayolalamikiwa yangejitokeza kuwa ni vinara. Huwezi kuwa tajiri wa kimataifa Kama BAKHRESA and then ukitafutwa kwa walipakodi wakubwa whether by compliant or by amount haupo??.Mkuu Kibanga Ampiga Mkoloni
Kuna tofauti kati ya kuwa tax compliant na kulipa kodi kubwa. Hao waliotajwa kwenye hiyo list ni tax compliant na sio lazima wawe walipa kodi wakubwa.
Unaniangusha yani VODA, TOGO, TTCL na AItel wanzidiw ana Simba Telecom Tanzania Limited (Telecommunication) ?
Haiwezekani kamwe labda kuna kitu hatukijuhi.
Wako wapi TANESCO? SOGAS? IPTL, SYMBION watu wanalipwa over 200 Mil kw asiku ila humu hawaonekani kwa nini?
TRA wamegawa haya makampuni ki sekta, hivyo BAKHRESA alitakiwa kuwa among walipa kodi wakubwa. Usisahau ni Kati ya matajiri wakubwa Africa, ikiwa na maana anazalisha sana pia.
Queen Esther
haya ni maajabu voda,azam etc makampuni makubwa hayapo kwenye walipa kodi wazuri! inabid tra wawachunguze coz wana volume kubwa sana.badala ya kukimbizana na wauza maduka waende huko kujua kunani mbona wanaleta kodi kidogo?mbona wafanyakazi sijackia wanalipa sana PAYE nao wanastail kupongezwa
Hawajajificha, ni kwamba wao wanalipa moja kwa moja kwa "watawala" na "chama tawala" hivyo hesabu zao hazionekani kwenye data base ya TRA! Tafakari!!!
Mpendwa usituchanganye, hata Kama ni tax compliant Kama unavyodai, basi bado makampuni yanayolalamikiwa yangejitokeza kuwa ni vinara. Huwezi kuwa tajiri wa kimataifa Kama BAKHRESA and then ukitafutwa kwa walipakodi wakubwa whether by compliant or by amount haupo??.
Hayo makampuni ya madini yanayoendelea kutuachia mashimo, kodi iko wapi jamani. Kodi anayolipa mfanyakazi ni balaa. Nina ndg yangu amepata redundancy akalipwa tshs. 90 mil , akakatwa kodi 30% ambayo ni 27 mil just imagine. Na bado alipokuwa kazini kila mwezi alikuwa anakatwa kodi. Hayo ni maumivu makubwa, inakuwa Kama double tax.
Halafu kaka Sesame unaleta hadithi wakati maumivu ya mfanyakazi ni makubwa. Ingekuwa wote tunalipa wala isingeuma. Mbaya zaidi waajiri wako buzy kutukata wapate hizo sifa unazosema wakati tunaumia.
Roho imeniuma sana sana na kodi kubwa kwa mfanyakazi, Wakati huko kwenye marasilimali ya nchi hakuna. Mweeeee tunaombaaa tunaombaaaa, usiku na mchana Mungu aiponye nchi yetu, hata hivyo tusikate tamaa, maana kila iitwapo leo tunaona uovu unazidi. Wale wanaoiombea nchi hii ni prayer item, tusikate tamaa, uwazi huu nao ni majibu, tungejuaje?
Mtoa mada ubarikiwe.
Queen Esther
Mjadala bila kujua namna makampuni yanavyofanya kazi itakuwa upotoshaji tu... mfano usitegemee group companies kama IPP, S.S. Bakheresa, SUMARIA to be in top tens..........b'se they have several companies under them and those are the one recognized by TRA.
tatizo ni kutojua makampuni yanavyoendeshwa na aina za kodi na ipi inatolewa wakati gani???yaani nashindwa kuelewa kampuni kama Barrick linalomiliki migodi minne n.Mara,Buzwagi,Bulyanhulu naTulawaka linazidiwa na Resolute kampuni yenye mgodi mmoja tena size ya kati halafu wakala\dealer wa voda Simba telecom anazidi makampuni mama kama vodacom,airtelna Zantel kweli hii ndiyo Tanzania