Tunaomba sana waziri wa kazi na ajira, mkuu wa uhamiaji, na polisi, Wakuu wa mikoa,wilaya, pia muwe wazalendo kazi zote hata za masenior yaani za mameneja ambao watashughulika na ujenzi wa hili bomba la mafuta haswa huko EACOp kazi zitolewe kwa watanzania weusi na wazawa
Sio mkajazanae wafaransa kisa hela ya bomba anatoa mfaransa haya mambo wenzetu hata Botswana hawafanyi hivi. Serikali ni supreme lazima ajira zote kuanzia main contractor and sub contractor wapewe miongozo ya kujaza nafasi kwa wingi na ujumla kwa watanzania asili yaani wazawa.
Sio mlete watu wanatoka Kenya,Uganda,Congo, waliozamia hapa nchini na vibali vyao vya kuhonga. Na Tunamuomba Superstar Freight Forwarding (SSF) kama mmoja wa macontractor naye azingatie upatikanaji wa ajira kwa watanzania kwanza sio mnatuwekea Project manager , sijui Freight manager Mzambia hayo mambo hayana nafasi katika awamu hii ya kuleta ajira kwa wananchi weusi watanzania.sijui Planner mtu katoka Togo sijui Ivorycost hayo mambo lazima yapingwe.
Nawasilisha