Tottenham Hotspurs Thread

Mkuu nakubali. Ila nimegundua hujaangalia performance ya Bale kwenye mechi anazopewa nafasi, tena mchezo ukiwa tayari umekwishadhibitiwa.

Kimsingi performance ya Bale imeanza kuleta matumaini kwenye mechi mbili zilizopita; ile ya Europa na Westham.

Kocha hawezi kumpanga Bale kwa kuwa tu ana jina. Ikumbukwe pia kuwa tatizo la inconsistency ya Bale inachangiwa na kucheza mechi chache sana kwenye misimu miwili iliyopita.

Wewe unajua mpira, mchezaji injury prone anapokosa enough game time ndiyo anazidi kuwa more injury prone na ukijumlisha na umri ndiyo inakuwa soo zaidi. Hii ndiyo situation inamkuta pia namba 10 wetu Lo Celso.

Kimsingi hata benchi letu la ufundi wanatamani Bale acheze kila mechi dk 90 na hata kocha kalisema hilo mara nyingi ikiwemo kwenye press conference ya jana.

All in all. Spurs kama inataka kuwa mshindani wa kweli wa ligi inapaswa kuwekeza uwanjani. Janja janja za ki-Man U au Arsenal za kununua wachezaji mmoja mmoja wa kuziba viraka hapa na pale hazitaifikisha popote.
 
Hahaha mimi kama shabiki wa Arsenal natetea kununua mchezaji mmoja mmoja. Hii husababishwa sana na Financial Fair Play rule, so hata nyinyi naamini mtajikuta na hiyo ishu ya mchezaji mmoja mmoja kwa angalau transfer windows mbili.

Bale anaweza kufungua defense, yaani hata kama asicheze 90 minutes basi amilikishwe 30 minutes za mwisho na aruhusiwe kufanya zile runs na wachezaji wenzake waangalie namna yao ya kudeal na mipira ya Bale.
 
Watu wangu wa Spurs, mkuje tumalizie hiki kiporo leo cha hawa wakulima.

Watu wazima leo wameanzia benchi ili next game na Burnley wawe fresh. Itakuwa vema wakiua mchezo mapema ili Bale acheze walau dk 30-45 zimwongezee confidence. Hii ndiyo run pekee ambapo anatupatia tumaini tangu tumsajili. Huyu ndiye mchezaji pekee mwenye potential katika RW miongoni mwa wote tulionao.

We line up like;
 
Siku hizi sina hata appetite ya kuingia huku. Hii timu inanipa presha
Usikate tamaa mkuu. Mafanikio yatakuja tu taratibu. Hata hizo timu zinazofanya vizuri sasa hivi mwanzoni mwa project zao hakuna makubwa waliyofanya. Liverpool kwa mfano. Miaka mitatu ya Klopp hakuna kitu. Hata sisi tutatoboa ila siyo rahisi.

Jana Mourinho kasema "mafanikio hayaji kwenye sahani ya fedha, ni lazima uyatafute".

#COYS
 
FT: 4 - 0

AGG: 8 - 1

Sasa michuano inaanza rasmi. Tutaanza kukutana na expendables wa Uefa kubwa.

Mazee, Bale is getting back.

#COYS
 
Wapenzi wa Mou,amepewa siku 12 tuu,la sivyo anapigwa chini na kocha wa RB Leipzig anakuja mr Julia
Tatizo la wadau wengi wa soka siku hizi ni kudhani kuwa mafanikio yanakuja kirahisi tu kwenye sahani ya dhahabu. Hivyo wakiona RB Leipzig inacheza mpira mzuri wa kasi dk 90 wanadhani "it's all about the couch". Utasikia "tunamtaka Nagelsman".

Kuna wengine wakiangalia mpira wa Klopp Liverpool inapokuwa on fire wanadhani hata akipewa timu zao itakuwa hivyo kirahisi tu.

Kuna wale wasiojua mchakato uliopelekea Bayern kuwa timu ya dunia kwa misimu hii miwili wanakesha wakitamani timu zao zimsajili Hans Flick akazinoe!

Iko hivi;

Mafanikio au mchezo mzuri wa timu unatengezwa na mambo mengi yakiwekwa pamoja. Sanjari na kocha mzuri panapaswa kuwepo support kubwa ya klabu kwa kocha na benchi lake.

Pia kitahitajika kikosi kilichokamilika na kinachoendana na falsafa na malengo ya kocha na klabu. Kwa tunaojua namna Bayern, Liverpool, City na Leipzig zilivyopitia michakato iliyopelekea wao kuwa na soka walilonalo sasa hatukurupuki tu kudhani makocha wao wataleta kirahisi mafanikio kama hayo mahali pengine.

Leipzig kwa mfano; kocha wao hajawahi kukosa anachotaka. Amepewa kikosi kinachoendana na falsafa zake na zile za klabu na mchezaji anapouzwa tayari kuna replacement.

Sasa tatizo la hizi timu zetu nyingi za Uingereza zinamilikiwa na kuendeshwa na mabepari ambao hutegemea timu ifanye biashara iwape gawio na si wao kutoa pesa mfukoni kuwekeza kwenye timu: Arsenal, United na Spurs kwa mfano.

Hivyo mchakato wa ununuzi wa mchezaji mmoja tu kuziba nafasi flani au kuongezea kitu flani kikosini hugubikwa na "siasa" nyingi na huchukua mlolongo mrefu kiasi cha kupelekea hata unrest kwenye benchi na squad.

Angalia suala la ununuzi wa Partey au Soares pale Arsenal kwa mfano. Tazama pia issue ya replacement ya Jan Vertonghen (LCB) pale Spurs utaelewa namaanisha nini. Angalia pia namna United ilivyoshughulikia issue ya replacement ya Ronaldo na Luis Nani kwenye RW utanielewa kirahisi.

Kuna baadhi ya hizi timu zetu yafaa mashabiki wake wafunguke waache kuota ndoto za mambo yasiyowezekana kwenye klabu zao.
 
Na tutaendelea kuuenzi na kuuheshimu mchango wake kwetu.

He was real a good coach
Mkuu, nakupa kongole nyingi kwa kuwa very honest and thankful. Muungwana ni kitendo. Mentality na ambitions za Abromovic na Jose ndiyo zimetengeneza hii Chelsea ambayo nadhani tangu 2004 ndiyo klabu ya epl yenye vikombe vingi zaidi (nadhani 18). Humo ndani kuna karibu kila aina ya kikombe.

Kudos.
 
Mpaka leo nasubir jibu hapa.
 
Mpaka leo nasubir jibu hapa.
Ha ha haaa. Bro, nakuhakikishia hutolipata kamwe. Ni kwa sababu hakuna kitu kama modern football. Football tactics ni zile zile na zitaendelea kuwa zile zile. Kinachobadilika ni technology inayosapoti kinachofanyika uwanjani. Vitu kama VAR au GoalLine technology.

Asilimia kubwa ya hao wanaokwambia Mourinho and Simeoni are playing the past hawajui ku-analyze mpira wala hata maana ya mpira wenyewe. Kinachowaongoza ni stats na mipira ya kwenye game za Fifa.
 
Team,

Hili kombe letu. Tumepangiwa na wakulima wengine tena. Wako vizuri ndiyo ila siyo level yetu. Tunawatoa asubuhi na mapema. Jana wamemdhalilisha Leicester nyumbani kwake King Power stadium kwa ujinga wa kocha wao. Kachezesha kikosi dhaifu ilhali fixture bado ilikuwa wazi.


#COYS

 
Hapa mou halazi damu. Atapambana kufa na kupona.
 
Kichaka cha kufichia udhaifu wa kocha Mou kimekuwa eti ni wachezaji hawana ubora ,sasa kaz ya kocha si ni kuwafanya wawe bora au
 
Kichaka cha kufichia udhaifu wa kocha Mou kimekuwa eti ni wachezaji hawana ubora ,sasa kaz ya kocha si ni kuwafanya wawe bora au
Mchezaji lazima awe bora kwanza ili mwalimu aongeze vitu vichache +mbinu za kushinda game. Unapoona club zinasajili wachezaji wakubwa, mbona usijiulize ni kwa nini hao makocha wasichukue hawa wachezaji wa mafungu wakawafundisha!? Ile Tot ilimfia Pochettino mikononi, bila kuisuka upya sidhani kama itakuwa rahisi kubeba vikombe.
Mou alipokuwa Man Utd alichukua Europa akiwa na akina Ashly Young, Valencia, Phil Jones, Lingard, Sanchez Marcus Rojo etc. Mou aliwaambia wakitaka kushinda makombe makubwa lazima usajili mkubwa ufanyike na kuanzia iwe ni kusuka upya defense ya timu. Wenye timu wakasema wachezaji waliopo wanaweza kuchukua kombe lolote, mwisho wa wakamtimua.
Ole alipokuja amepita kule kule Mou alikosema kunahitaji kufanyiwa kazi, angalia sajili zilizofuata hapo Man Utd. Pamoja na kupewa wachezaji aliohitaji bado hana dalili za kuchukua kombe lolote.
Nadhani watu wanataka kumtumia Mou kama "hired gun ", yaani ukiwa nae unapaswa kuchukua vikombe vyote bila kujalisha kikosi ulichonacho.
 
Kila shabiki na mpenzi wa soka angekuwa hivi ingekuwa mujarab saana. You know the game bro. Mourinho anafanywa kuwa malaika. Atumie mikuki, mishale na mapanga kushinda vita ambayo washindani wana bunduki, vifaru na mizinga.

Huwa najiuliza ingekuwaje makocha kama Pep na Klopp ndiyo wangekuwa wanainoa hii Spurs ya sasa au ile United ya Mourinho. Zingeshuka mpaka daraja la pili huko nadhani.
 
Hatimaye Bale wetu anaweza kuanza kwenye mechi ya ligi. We are killing people with our attacking. Leo kama ida ni 4 2 3 1 vs Burnley.

#COYS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…