Mbeya City Spurs I
JF-Expert Member
- Jan 6, 2021
- 482
- 1,025
Mkuu nakubali. Ila nimegundua hujaangalia performance ya Bale kwenye mechi anazopewa nafasi, tena mchezo ukiwa tayari umekwishadhibitiwa.Ah sisi tulianza na ushindi na hatujapokea kipigo kikubwa cha kuzidi goli nne.
Kocha hua ana kipaumbele, Mourinho inawezekana kipaumbele chake ni top four au trophies kama EFL hivi kisha kiangazi anaongeza kikosi. Hiki ndiyo tunatarajia akija kocha mpya.
Mimi ningekua kocha kwanza ningebadili formation, ningetumia 4 2 3 1 au 4 3 1 2. Backline hii hii anayoitumia isipokua ningempa sana game time Bale kucheza kama RM kwenye 4 2 3 1 na kucheza kama SS kwenye 4 3 1 2.
Kwenye 4 3 1 2 hii 1 namuweka Son, 2 ST anakua Kane na SS anakua Bale, kwenye 4 2 3 1 hii 1 anakua Kane, hii 3 watasimama Son, Ndombele na Bale. Yaani forward yangu ingemjumuisha Bale, Son na Kane kivyovyote kutokana na wote wana speed hivyo naandaa mazingira ya kaunta na kuwafanya wapinzani wasijisahau hence kupunguza kulisakama lango.
Kimsingi performance ya Bale imeanza kuleta matumaini kwenye mechi mbili zilizopita; ile ya Europa na Westham.
Kocha hawezi kumpanga Bale kwa kuwa tu ana jina. Ikumbukwe pia kuwa tatizo la inconsistency ya Bale inachangiwa na kucheza mechi chache sana kwenye misimu miwili iliyopita.
Wewe unajua mpira, mchezaji injury prone anapokosa enough game time ndiyo anazidi kuwa more injury prone na ukijumlisha na umri ndiyo inakuwa soo zaidi. Hii ndiyo situation inamkuta pia namba 10 wetu Lo Celso.
Kimsingi hata benchi letu la ufundi wanatamani Bale acheze kila mechi dk 90 na hata kocha kalisema hilo mara nyingi ikiwemo kwenye press conference ya jana.
All in all. Spurs kama inataka kuwa mshindani wa kweli wa ligi inapaswa kuwekeza uwanjani. Janja janja za ki-Man U au Arsenal za kununua wachezaji mmoja mmoja wa kuziba viraka hapa na pale hazitaifikisha popote.