Tottenham Hotspurs Thread

Nachojua Ndombele hakusajiliwa na Mourinho. Mourinho hakumleta Ndombele
 
Nachojua Ndombele hakusajiliwa na Mourinho. Mourinho hakumleta Ndombele
Vumilia tu mkuu. Kuna fix nyingi sana. Juzi kati hapo zilizidi mpaka nikajaa gesi. Ki ukweli huwa na-mind sana kuona mtu mwenye zero understanding kuhusu jambo fulani anaandika tu kwa kwa kuwa bando lake. Hata kama hajui anachoandika.

Huyo mkali anakwambia Jose kamsajili Ndombele! Anakwambia pia Jose kasababisha Dele Alli ashuke kiwango na anamchukia ndiyo sababu hampangi.

Noma sana. Huyo bwana hata hajui kuwa Poch ndiye alimsajili Ndombele. Kutojua siyo tatizo, tatizo mtu kujifanya anajua wakati hamna anachojua.
 
Mechi ya leo itakuwa kali sana ila ushindi lazima. Haya ndiyo makombe tunaweza beba. Leo natarajia Jose aweke full squad, yaani hakuna kuremba. Kwanza Ancelotti tunamdai.

Ushindi leo lazima

#COYS
 
Huu mtanange wa leo utakuwa [emoji91][emoji91][emoji91]


Hii kwangu ndiyo fixture ninayoikubali zaidi: Jose vs Carlo
 
HT: 2-3

My take; Timu inacheza vizuri. Tunatengeneza nafasi nyingi ila wafungaji hatuna. Pia defensively hatuko vizuri hivyo kupelekea individual mistakes nyingi. General Maestro Hojbjerg kachomesha mawili peke yake. D Sanchez naye nusu achomeshe.

Mchezo bado upo. Kane aingie tu, maana hakuna namna nyingine.
 
We are out FA cup

120": 5-4

Everton were very clinical with their chances. We had ours but couldn't take them. Good luck Carlo.

Next stop: City jumamosi saa 20:30
 
We jamaa skujua kama ni ndezi kweli, wapi nilisema Mourinho kamsajili Ndombele ?? Issue ya Delle Alli Dunia nzima inajua ni mistrust ya Jose ndo imesababisha dogo kashuka kiwango wakat ni finisher mzur Sana ..... Usijifanye unajua Sana mpira kumbe hujui lolote pimbi wewe , na usinitolee reference tena kama huwez kujadili vyema ,mbna wengine wananiquote Kwa mjadala na maoni mema ....wewe mpak ujifanye unajua na kutoa kejeli ??
 
Mara ya mwisho kuchukua kombe ilikuwa lini?
Aisee, noma. Umenifurahisha sana permanides . Hizi timu tunazipenda ila lazima tuwe tunzijua vema. Kabati letu lina kakombe kamoja tu enzi hizo kanaitwa Carling Cup. Hapo unaambiwa tumeharibiwa timu.

Nadhani tuwe na subira. Project zinazofanikiwa zote huchukua muda. Tena kwa mmiliki bahili kama Levy tusitarajie mafanikio ya mara moja.

Kumlaumu kocha kwa mechi kama ya jana ni kutarajia makubwa sana. Mchezo tulipaswa kuumaliza half time ukiangalia nafasi tulizotengeneza.

Kocha hawezi kuingia miguuni mwa Moura na Lamela akaifanyie renewal. Muda wao uko mwishoni. Mimi nafikiri tuko kwenye mwelekeo mzuri tu.

Tukiimarisha kikosi dirisha lijalo tutarudi msimu ujao tukiwa washindani wa ukweli.

#COYS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…