Tottenham Hotspurs Thread

Jana timu imecheza bhana , nafkr ni mechi Bora kabisa ya FA kwa msimu huu , kuna some defensive error zinaigharimu Timu ....
 
Tuwe realistic kidogo, kombe recently Tottenham ililochukua ni Carling cup nadhani zaidi ya miaka 5 iliyopita. Tottenham imechukua kombe la ligi kwa mara ya mwisho mwaka 1961 mpaka leo haijachukua kikombe cha kueleweka.
Rednkap na Pochetino walikuwa na amsha amsha lakini hakuchukua kikombe chochote.
Ila pia uendeshaji wa mpira umebadilika sana, mwanzano tulizoea kuona academy players wakiendelezwa taratibu na kuwa ndio chimbuko la wachezaji wa senior team. Ila kwa sasa mwenye mkwanja mrefu ndio mwenye uwezekano wa kupata mafanikio kwa haraka.
Mou tokea msimu uliopita alihitaji kuimarisha ulinzi na ushambuliaji ila kila mmoja anaona aina ya wachezaji waliopatikana na umuhimu wa kile mou alichoimanisha.
Ukichukua usajili wote wa Tottenham wa msimu uliopita ni kama sawa na usajili wa Timo Warner. Wachezaji wa Tottenham iliyosajili walikuwa wa kawaida sana ila wa kimkakati tu. Tottenham ikitaka mafanikio ya haraka pia ikubali kupambana na timu pinzani katika usajili, siyo unanunua wachezaji wa buku jero afu unataka kupata mafanikio kwa haraka zaidi ya wale waliowekeza mamilioni.
 
Jana timu imecheza bhana , nafkr ni mechi Bora kabisa ya FA kwa msimu huu , kuna some defensive error zinaigharimu Timu ....
Huu utopolo umetundikwa tano juzi, inafaa nyie mashabiki mrudi kwenye timu zenu za zamani. Hapa najuwa wengi ni Arse8 na manyumbu.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Jiandae kuhama tena timu, Tuchel mepigwa mchana kweupe, ni mzuka tu amekuja nao soon utakata
 
Well said mkuu. Levy anastahili saluti kwa namna alivyoitransform Spurs nje ya uwanja. Amefanya kazi ambayo timu zingine zimeshindwa kufanya pamoja na kuwa na pesa za mafuta na za Wachina au Waasia wengine: City, Wolves, Leicester, PSG, nk.

Ila ajue kabisa bila kununua wachezaji wazuri hii timu itakuwa na wakati mgumu sana kiushindani. Matokeo anayopata Jose na hiki kikosi angekuwa kocha mwingine tungekuwa tushashuka daraja.

Afanye clearance ya deadwood zote walau kikosi cha kwanza. Huwezi kutafuta vikombe ukiwa na Lamela au Moura kwenye namba 10. Huu ni kama utani.

Kama leo hii game na City inayoendelea. Ni bahati kwamba tuko nyuma goli moja tu, ikizingatiwa tofauti ya ubora wa hivi vikosi.

Ngoja tuendelee kucheki hii game.
 
furaha yangu kuona Mourinho anapigwa kila leo ili mjue timu haina kocha,najua wengi wanamtetea kocha kuwa hajapata wachezaji wa maana ndomaana mipango ya ushindi inafeli.hivi kwa mchezaji mmojammoja Leicester anamzidi wapi Spurs...Mou kaishiwa atapigwa kila leo na pira lake bovu hata kuvuka mstari wa kati ni shida.1hlf no shot on target na una washambuliaji wako wote mbele yani kwa timu inavyokaa nyuma itagawa penati kila siku na humu kwenye hili jukwaa la mashabiki mnaojua mpira kuliko wote Tanzania sitoki mpk bwana Jose atimuliwe.
 
Respect mkuu. Mimi naomba nijaribu kujibu swali lako kuhusu Leicester. Nitakutajia nafasi mbili tu. Hizo nyingine ukafuatilie wewe mwenyewe ili usije kusema namtetea sana Jose.

Kwenye RB

Leicester wana Pereira na Timothy Castign. Spurs tuna Matt Doherty na Serge Aurier.
Kama unajua mpira utaona ipi iko vizuri zaidi.

Kwenye namba 10 (CAM)

Sisi tuna Dele Alli na Le Celso (pancha). Leicester wanaye Madisson. Again kama unajua mpira utaona nani ana advantage.

Pia ujue kwamba kuwa na mchanganiko wa nyota kadhaa na magarassa kadhaa kwenye first eleven kama Spurs kunaifanya kuwa na kikosi dhaifu kuliko timu yenye wachezaji average lakini hawana garassa hata moja.

Kama unadhani Lamela au Moura kwenye RW wana ubora kuliko Gray basi ujue nakutakia mafanikio katika maombi yako ya kutaka Jose afukuzwe. Ila ujue Levy ni genius na anajua Mourinho atampa nini.
 
Kuna vitu viwili ambavyo ni muhimu sana kueleweka kuhusu SPURS.
1. Usajili na better scouting.
Naomba tukumbuke, ni lini spurs iliweza kusajili wachezaji wazuri. Wote tutakubaliana nami kwamba ni kipindi kabla Gareth Bale hajauzwa. Maake hela ya Bale pale tulibahatika tu kupata Eriksen wengine wote viwango vya kawaida mno(including Lamela). Miongon mwa wachezaji ambao waliletwa tangu hapo n pamoja na Roberto Soldado, Chiliches, hotberg, David sanchez, (ambao wote walikua ni typical Flopy players) atleast (Lamela, chadli, wanyama, ) wakali ni Son
#Kuna chief scouting nakumbuka alifukuzwa ambaye alikua fundi, na nakumbuka aliletaga watu kama (Dele Ali, Toby, Jan, n.k)#
Ili team ifanye vizur ni muhimu sana kuwa na sajili zenye manufaa, kuna kipindi hapo tumekwama sana kwenye hili

2. Game tactics.
Game tactics ya mourinho ni Defensing,,
KWANINI MBINU HIZO HIZO ZA KUJILINDA ALIFANIKIWA NAZO, CHELSEA NA TEAM ZINGINE HUKO NYUMA LKN SIO MAN U, SPURS NA MADRID??
1, Aina ya wachezaji aliokua nao. Huwezi ukafanikiwa na hii mbinu kama hauna wachezaji wazuri kwenye ulinzi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza. Je, kwa spurs ya sasa anamlinzi gn anayeweza akalinda kweli?? (Kama kipind yuko na akina John Telly, Essein, Obi, na Cole pale chelsea) wakati huo huo ana team yenye washambuliaji makini pia, wakifika golini ni Goli,,.
2. Huwezi ukalinda,, kwa kila muda kukaba tu,, the whole team.
Wachezaji wanatumia nguvu nyingi sana, wanachoka,, huku wasipate matokeo mazuri.
Mpira wa sasa, ili ujilinde ni lazima either uwe unashambulia, au umiliki mpira. Vinginevyo ndo hizo individual errors zisizo koma na sasa technologia tukiwa na VAR.

NINI KIFANYIKE.
Kuna haja kubwa sana ya, kuwa na
1.scouting team nzuri.. sio kuleta wachezaji hata hawana msaada kwenye team,, eti kisa wana uzoefu au ni bei nafuu.
Kumbuka: msimu mwakajuzi tuliofika nusu fainali UEFA hatukisajili lkn team wachezaji wengi walikua wako kwenye peak nzuri. Na angepatikana mmoja tu (Dyabala)kama wataalamu wanavyosema,, labda tungebebaga ile ndoo.
2. Kocha anaye endana na mpira wa sasa.
Mourinho kwa sasa,, kaishiwa mbinu team zishamjua na hanaga mbinu nyingind yeyote ya ziada.
Better tukapata kocho mwingine,, ataye ruhusu team ifanye plessing kama spurs iliyozoeleka machon pa watu.
As currently neither we enjoy playing footbal or Results.
3. Scoud update,,
Team ili ifanye vzr lazima tubadili kikosi mara kw mara.

MAONO YANGU NI HAYO.

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
unasema Mourinho hakufanikiwa na Real Madrid???


Mourinho alifanikiwa kuchukua ubingwa mbele ya timu bora ya karne ( barca ya messi, xavi na iniesta).

Mourinho aliweka rekodi ya kuchukua ubingwa kwa pointi na magoli mengi.

Mourinho ndiye aliyefuta uteja wa Real Madrid kuishia hatua ya Mtoano Uefa.

Mourinho alimmbadilisha Ramos from RB to CB bora duniani.

Real Madrid iliyochukua champions league 2014 na 2016 backbone yake ilisukwa na Mourinho..

Hapa umepuyanga sana.
 
[emoji4] Nakubali mkuu.

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, nimependa sana uchambuzi wako. Ila kwenye issue ya scouting na utaratibu wa kununua mchezaji, Spurs ni miongoni mwa timu zenye structure nzuri zaidi. Mimi nadhani kikwazo ni mwenyekiti mtendaji bwana Levy.

Mchakato wa kununua mchezaji Spurs kwa sasa uko hivi;

Kocha huandaa ripoti za mara kwa mara kwenye kila nafasi na kuikabidhi kwa mkurugenzi wa ufundi (technical director). Kabla ya kuwasilisha ripoti hizo Jose hushauriana na mkuu wa academy kuhusiana na anachotaka kocha kwenye nafasi husika na kile klabu inapaswa kufanya.

Mkurugenzi wa ufundi akipokea ripoti hiyo anajadiliana na Jose kuhusu options walizonazo. Hapa Levy alisisitiza kuwa Jose huwa very specific na profile ya mchezaji anayemtaka.

Wakiishaafikiana kuhusu majina ya wachezaji wanaopendekezwa, anaongezeka mtu mwingine ambaye ni mwanamama mkurugenzi wa fedha. Hapo kwa pamoja wanaifupisha orodha ya wachezaji pendekezwa kwenye nafasi hiyo na hatimaye wanaikabidhi kwa Levy ili afanye maamuzi.

Sasa shida ni hesabu kali za Levy. Kwa mfano, dirisha lililopita Spurs ndiyo timu ya kwanza kumtaka Ruben Diaz ambaye ndiye alikuwa chaguo la kwanza la Jose. Benfica walipotaja bei £m68 Levy kampotezea akaenda City. Option ya pili ilikuwa Milan Skriniar ambaye Inter walitaka €m45 Levy kaona kubwa. Badala yake kaenda Swansea kuchukua chaguo la tatu dogo Joe Rodon ambaye ni mpango wa muda mrefu!

Pia kwenye stricking Jose alimtaka Andrea Bellotti kaletewa Carlos Vinicious.

Vilevile Ikumbukwe kuwa Spurs haina pesa za mafuta. Wamiliki waliinunua timu kwa £m27 na wanategemea gawio kutoka kwenye timu; hawaingizi pesa yao. Hivyo kuna wachezaji ambao ndiyo wanauza zaidi Levy alimwambia Mourinho lazima wabaki.

Eric Dier kwa mfano. Aliapa Spurs sharti ili asaini mkataba mpya. Kwamba lazima acheze CB na si DM alipokuwa akicheza. Mourinho alisema kwenye press conference kuwa Levy alimwambia kuwa anataka Dier abaki. Kwa hiyo Jose akalazimika kumpanga beki ya kati kama bosi anavyotaka!

Hivyo nadhani structure ni nzuri ila tatizo ni hesabu kali za Levy.
 
Nimekuelewa sana mkuu Mbeya City Spurs I [emoji106]

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
dah...mkuu ukiacha hapo kwa Madrid ulipoteleza kibinadamu kiukweli umeandika point tupu na hapo kwa kocha na mbinu zake ndipo mimi ninapopagusia kila leo, inashangaza kuona kuna shabiki wa dunia ya sasa kuridhishwa na mpira wa bwana Jose.kwangu mimi Spurs ilipo sasa nawapa lawama wachezaji kwa 35% na Jose 65% .Spurs hii iliongoza mpaka ligi kipindi fulani akapewa sifa nyingi bwana jOSE leo Spurs matokeo ya kusuasua lawama pia azibebe kama alivyopokea pongezi
 
Ukiangalia hata mechi tulizopoteza, Mou anaingia na approach sahihi ila makosa binafsi ndio yanaicost team. Lakini hata hivyo, Tott karibia kamaliza zile fixtures ngumu zote. Naamini game zijazo timu itatulia na vita ya top four itaanza upya. Ila msimu ujao beki na ushambuliaji ni lazima vifanyiwe kazi ili kupata timu ya mashindano.
 
Hili thread imekuwa tamu sana japo timu haifanyi vizuri. Mijadala inaenda deep. Ni hoja juu ya hoja.

Pongezi kwa wajumbe wote kwa kifikisha post 2000.

Labda sasa mods wataanza kufikiria kutupa heshima tunayostahili watuweke pale juu kwenye sticky threads.

Au watasubiri mpake tuchukue vikombe vyetu tulivyokatia hakimiliki msimu huu: Europa na Karaghabaho!

#COYS
 
Naongezea tu, Mourinho alimfanya Ozil awe king of assists.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…