Tottenham Hotspurs Thread

Tottenham Hotspurs Thread

Karibu sana jamvini mkuu
Asante .......


Ahahahahaha..mambo mengine tunayaacha kama yalivo kama yaliyotokea kwa wenzenu wa london na conte wao ....ila hayatuhusu [emoji1] [emoji1] [emoji1] .. Hugo Lloris huu ulikuwa mchezo wake, mchezo wote ulikuwa kwenye himaya yake, mipira yote iliyopigwa na Real Madrid ilikuwa rafiki wa gloves zake. Madrid walianza kufia kwenye gloves za Hugo Lloris kwanza. Kabla ya blocking, tackling na interception za Toby Alderweireld, Jan Vertonghen na Davison Sanchez kwa Christian Ronaldo, Karimu Benzema na Isco wasimdhuru Lloris.

Erick Dier na Harry Winks hawa walikuwa wanacheza flats katika kujenga ukuta mgumu mbele ya Alderweireld, Vertonghen na Sanchez. Walipishana mara chache sana kwenda kuwapa sapoti Bami Delle Alli na Christian Ericksen katika ile 3:4:3 ambayo ilikuwa 3:4:2:1 katika uchezaji na majukumu ya Pochettino.
Bado Casemiro, Toni Kroosi na Mondric wanahitaji backup ya wanadamu bora sana katika eneo lile. Hapa ndipo palikuwa na njia ya mpitisho ya mipira yote ya Tottenham Hotspur. Tottenham walionekana kuwa Wengi katika kukaba lakini pia walionekana wana nguvu kubwa ya one against one katika kushambulia.

Uwepo wa Nacho Fernandez, Ashraf Hakim katika eneo la Ulinzi wa Real Madrid, pamoja na Casilla golini kuliongeza umakini katika ukabaji kwa upande wa eneo la kiungo cha Madrid na kupunguza ule ubora wa Madrid katika umiliki na kupanga mashambulizi makini katika eneo la Spurs.

Kuna wakati Spurs niliona kama hawapo serious na mipira ya mwisho ambayo walikuwa wanaipata ndani ya box la Real Madrid. Kuna wakati Kane aliamua kuchop na mpira ukawa Zawadi ya Casilla, pia kuna wakati Delle Alli naye kabla ya goli la kwanza, naye aliamua kuchop na ikawa Zawadi ya wazi kwa golikipa yule. Kama Spurs wangekuwa makini na aina ya mipira waliokuwa wanaipata basi Madrid wangeikumbuka Wembley stadium kila kuchwao Msimu huu.

Kinachomtesa Zinedine Zidane ndicho kinachomtajirisha Pochettino. Kuna siku Pochettino anaamua kuanza na Ben Davies kama wing back wa kushoto, na kuna wakati anaamua kuanza na Dani Rose pia katika eneo hilo hilo. Kuna wakati Pochettino anachagua wa kuanza upande wa kulia pia, aanze na Kylien Trippier au aanze na Serge Aurier. Hii ni tofauti sana na mateso ya Zinedine Zidane katika eneo linalofanana na hilo. Madrid ikimkosa Dani Carvajal unaona namna Zidane anateseka, sababu utajiri wa eneo hilo ni mdogo sana. Zidane kuna kipara mzee.

Kuna wakati Dele Alli anabaki juu, alafu Harry Kane na Christian Ericksen wanakuwa nyuma yake, kuna wakati Kane anakuwa juu, alafu Alli na Ericksen wanakuwa nyuma yake na kuna wakati Kane na Alli wanakuwa nyuma ya Ericksen na wanafanya build up kwa ufasaha na kuwatesa walinzi wa Madrid chini ya Sergio Ramos.....
 
Wembley Stadium
d01e373a3936405fe3e55cddb0f025da.jpg
 
Back
Top Bottom