Point yako ya msingi ni nzuri sana mkuu. Kwamba hata kikosi kikiwa cha kawaida kikiwa na spirit kinapata matokeo. Big yes. Ila sharti hicho kikosi cha kawaida kiwe na balance, yaani kusiwe na eneo lenye udhaifu kupita kiasi, hapo kupata matokeo inakuwa ngumu.
Binafsi ninaona sababu kadhaa kwa nini Spurs ilifanya vizuri mwanzoni mwa msimu na sasa haifanyi vizuri. Acha nijadili tatu (3).
Moja.
Mwanzo mwa ligi timu ilikuwa na mshambuliaji mchezeshaji (namba 10) mzuri ila alipoanza tu kupata majeruhi ndipo tukaanza kupoteza matokeo; Giovani Lo Celso. Angalia tulipoanza kupoteza pointi kirahisi ni lini utanielewa.
Mourinho anapokuwa na kikosi cha kawaida au kizuri kisichobalance hapati matokeo bila namba 10 mzuri. Rejea hata ule msimu wa 2017/18 alipoanza vizuri kisha akaanza kupoteza pointi mpaka kumaliza pointi 18 nyuma ya City.
Mikitaryan alipokuwa akicheza vizuri nyuma ya Lukaku ilikuwa mwendo wa 4G. Defense yake mbovu ya akina Smalling na Phil Jones ilipoanza kuwa exposed (kumbuka wapinzani nao wanakusoma siku zinavyoongezeka) kocha akataka namba 10 naye ashiriki ulinzi timu inapokuwa haina mpira! Tatizo. Mikitaryan kaanza kupotea, creation ikapotea na timu nzima ikapotea.
Vivyo hivyo. Gio na Ndombele walikuwa wakicheza vema kwenye CAM na hivyo kuficha udhaifu wa Sissoko/Winks na Bergwijn kucover vema kwenye RW.
Mbili.
Timu nyingi kubwa zilianza ligi vibaya; City, United, Chelsea. Hii iliinufaisha Spurs kwanza kwa kuzifunga timu zenyewe (City 2-0, United 6-1, na nyinyi nadhani) lakini pia ilimaanisha Spurs anashindana na akina Everton, Liverpool, na Aston Villa pekee. Lakini sasa vigogo karibu wote ukiacha Arsenal wanapata matokeo na Everton na Villa hawatetereki. Hivyo sishangazwi na nafasi aliyopo Spurs.
Tatu.
Overdependence kwa wachezaji nyota wa kikosi imewafanya kuchoka na kuanza kupoteza sharpness. Na hili mimi na wewe
Castr tushalijadili sana. Kwamba kwa nini nyota wa Spurs wanacheza kila mechi.
Ukiangalia namna Kane na Son wanavyokosa magoli utaelewa ninachomaanisha. Pia ukiangalia rafu anazocheza Hojbjerg utaona namna uchovu unavyochukua nafasi yake.
Na hapa simlaumu kocha. Kwenye mechi ndogo hasa za makombe, akiwaanzisha nje atalazimika kuwaingiza kuokoa jahazi. Akiwaanzisha wakapata magoli, akina Dier na D Sanchez wanachomesha hivyo analazimika kuwabakiza mpaka dk za mwisho kujihakikishia matokeo.
Swali kwako mtani wangu
Castr . Naomba uniambie ungekuwa wewe ndiye kocha wa Spurs, ungepanga backline ipi ambayo ingepata walau clean sheet tatu tu katika mechi tano?