Mpira tulicheza kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza tulicheza kama Yanga. Poor with the ball, poor without the ball. Kuna wachezaji wetu muhimu ilikuwa kama hawataki kucheza hivi. Binafsi niliona Ndombele akigusa mpira mara mbili tu kipindi cha kwanza kwa mfano.
Ndiyo sababu mliimiliki midfield. Ilimbidi kocha kumtoa sadaka mshambuliaji mmoja (Bale) ili aingie mkabaji (Sissoko). Baada ya kuona bado kuna wavivu ikabidi kumtoa Ndombele aliyekuwa kahamishiwa mbele kama CAM, akaingia Dele Alli.
Hapo ndipo ikawa turning point ya mchezo. Ni ile tu Kane hakuwa na bahati. Miamba kadhaa na kosa kosa nyingine.
Tatizo jingine la kikosi chetu ni kuwa na wachezaji tegemezi wenye low mentalities. Kwa mfano, kwa namna Ndombele alivyocheza juzi ingekuwa kocha kama Ferguson hachezi tena na anauzwa mwisho wa msimu! Kumbuka Barthez alivyozingua kwenye 4-3 ya United vs Madrid. Ila kwa kuwa Mourinho akimbenchi mechi mbili tu zijazo media zitamuua.