Tour Guide kuomba Watalii pesa ni moja ya sababu watalii hawataki kurudi Tanzania?

Tour Guide kuomba Watalii pesa ni moja ya sababu watalii hawataki kurudi Tanzania?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,532
Reaction score
14,164
Ukijaribu kuangalia triend ya Utalii hata Africa utagundua tunazidiwa hata na Botswana, achilia nchi kama South Africa au Moroco inayo Ongoza.

Kuna Mama mmoja wa Kizungu anaishi Arusha na kaolewa na Mbongo mmoja hivi, sasa kuna kazi alinipa nyumbani kwake, na wakati nafanya nikaona Gari za Utalii za kwake Zimepaki ni ana kampuni ndogo ya kitalii.

İkibidi nimuulize hujapata watalii? Mbona gari zimepaki tu? na je ni kwa nini Tanzania tunazidiwa na nchi ambazo hazina hata vivutio vingi vya utalii?

Alinieleza swala la kodi, na tozo mbalimbali za Serikali na swala la huduma mbovu, aliniambia bado huduma zetu ni duni sana sana, Miundo mbinu ni shida sana, Udokozi/ wizi, utapeli na ujanja ujanja wa kampuni za kitalii,

Kubwa kulilo lote lililo nivutia sana ni kuhusu Tour guaide kuwa omba sana watalii/ wageni pesa, aliniambia binafisi alisha pokea malalamiko mengi sana ya wageni kulalamika kuombwa pesa na waongoza watalii na hata Kampuni za kitalii kuwapangia pesa za posho za kuwapa Guide.Alisema wageni wanachukia mno hio tabia ila ni basi tu.

Alisema wageni/ Watalii wanachukizwa sana na kupangiwa Tip/ posho za kuwapa Tour Guide na ndo maana pia watalii huwa hawa opt kurudi tena Tanzania kwa sababu ya haya.

Kwenye hili nilikubaliana naye kwa sababu nina Washikaji ni Ma tour Guide huwa wananipa story za wanavyo waganda watalii na hata kuwapa sababu mbali mbali kama za wao kutunza yatima, na wapo wanao tembea na picha feki za watoto ili watalii wawape pesa.

Hili la Kampuni za Utalii kuwapangia Wageni kiwango cha Tip lipo sana ila sijajua huko Duniani wao wanafanyaje hiyo hili sikutaka kubaliana naye hadi nipate upande wa pili, ila la Tour Guide kuomba pesa kwa Wageni hilo ni kweli kabisa.
 
Mkuu Mimi sio Mtalii ila ni Mnywaji, nachukia sana muhudumu anayelazimisha nimnunulie Pombe au badala anipe chenchi yangu yeye anajikausha nayo kwa kudhani nimelewa sikumbuki.. au mwengine anakwambia kabisa chenchi nanunua pombe yangu.. Aiseeee... Nikienda hiyo Bar ikajirudia mara 3 basi nakata mguu kabisa.!

Muache mtu atoe mwenyewe kwa roho yake, utapata mengi zaidi ya hivyo vya kuomba.
 
Kwa taarifa yako guide hajipangii tip(mboneka).toka mgeni ametoka huko kwao ameshapewa list yote ya malipo kwaajili ya guides au watu wa kupanda milimani!!..labda uniambie tabia ya kuomba vitu vidogo vingine kama viatu,saa au material zingine....

Kuhusu huduma mbovu kiukweli inalingana na bajet ya mgeni mwenyewe..

Wageni wanapenda ku bagein sana!utoe ela ya kifala utegemee kupewa five star service ushaona wapi
 
Madereva na Tour guides wengi hutumia Tabia hiyo na hulka ya kujishusha ati tajiri yao hatoi mshahara mzuri, pia kulalamika shida ati familia sikuwachia posho nyumbani.... Watalii huona ni kero,adha na huchafua siku yao na kitu ambacho hakiwahusu... !!
Taswira nzima ya vivutivo vetu safari nzima hupondeka na kuharibika..!!
 
Kwa taarifa yako guide hajipangii tip(mboneka).toka mgeni ametoka huko kwao ameshapewa list yote ya malipo kwaajili ya guides au watu wa kupanda milimani!!..labda uniambie tabia ya kuomba vitu vidogo vingine kama viatu,saa au material zingine....

Kuhusu huduma mbovu kiukweli inalingana na bajet ya mgeni mwenyewe..

Wageni wanapenda ku bagein sana!utoe ela ya kifala utegemee kupewa five star service ushaona wapi
Hilo la kupangiwa kiasi cha Tip liko sawa? Ndo mfumo wa Dunia nzima?
 
Madereve na Tour guides wengi kutumia Tabia hiyo na hulka ya kujishusha ati tajiri yao hatoi mshahara mzuri, pia kulalamika shida ati familia sikuwachia posho nyumbani.... Watalii huona ni kero,adha na huchafua siku yao na kitu ambacho hakiwahusu... !!
Taswira nzima ya vivutivo vetu hupondeka na kuharika!!
Ya wanalalamika sana, na kuwadanganya hadi kwamba mara wanasomesha yatima, mara wana saidia wajane mara sijui watoto wa kike yaani fixi nyingi hii inachukiza sana watalii
 
Kwa taarifa yako guide hajipangii tip(mboneka).toka mgeni ametoka huko kwao ameshapewa list yote ya malipo kwaajili ya guides au watu wa kupanda milimani!!..labda uniambie tabia ya kuomba vitu vidogo vingine kama viatu,saa au material zingine....

Kuhusu huduma mbovu kiukweli inalingana na bajet ya mgeni mwenyewe..

Wageni wanapenda ku bagein sana!utoe ela ya kifala utegemee kupewa five star service ushaona wapi
Kunagaine kuko Dunia nzima, wao wanacho lalamika ni kuombwa pesa, na kupangia kiwango cha kutoa tip
 
Huyo mama kakupa sababu nyingi za watalii kutotaka kurejea nchini lkn wewe umeamua kwa sababu zako binafsi kuja na hio moja tu! Mbona bar ombaomba kibao lakini bado tunarudi kila siku kunywa, mtu akiombwa pesa ana option ya kutaa au kukubali hawalazimishwi na mtu.

Lakini vipi kuhusu baa kupandisha bei kuliko baa za jirani au duka jirani, wateja watarudi tena kweli? Tatizo kuu ni tozo kubwa sana ingawa hutaki kuliona hilo. Tanzania ni destination ghali kuliko zote east africa, ni ghali tangu visa mpaka fees za hifadhini
Ni bora mgeni aende Kenya au uganda au zambia atamwona simba yule yule na atarudi na change mfukoni kuliko hili balaa la kodi zitakazomkabili pindi atakapoweka mguu wake nchini!

Tumemfanya mtalii ni al shabab, hatakiwi nchini kwetu na silaha uetu kuu against yeye ni kodi kuubwa.
Taarifa ndio hiyo sio sababu ya ombaomba
 
Hilo la kupangiwa kiasi cha Tip liko sawa? Ndo mfumo wa Dunia nzima?
Ofcoz ndio maana kuna TRIP ADVISOR!!wageni wengi hufanya booking ya safari zao kwa AGENT alieopo huko!!hufanya malipo yote huko huko isipokuwa tip ya kuwapa guides ndio huibeba..hapo kwa agent ndio hupewa mfumo wote wa malipo ya guides in details....
Kampuni ambayo ita provide kuanzia hotel na transport huja kulipwa na huyo agent baadae sana!!.muda mwingine agent analala mbele na pesa zako.
 
Huyo mama kakupa sababu nyingi za watalii kutotaka kurejea nchini lkn wewe umeamua kwa sababu zako binafsi kuja na hio moja tu! Mbona bar ombaomba kibao lakini bado tunarudi kila siku kunywa, mtu akiombwa pesa ana option ya kutaa au kukubali hawalazimishwi na mtu.
Lakini vipi kuhusu baa kupandisha bei kuliko baa za jirani au duka jirani, wateja watarudi tena kweli? Tatizo kuu ni tozo kubwa sana ingawa hutaki kuliona hilo. Tanzania ni destination ghali kuliko zote east africa, ni ghali tangu visa mpaka fees za hifadhini
Ni bora mgeni aende Kenya au uganda au zambia atamwona simba yule yule na atarudi na change mfukoni kuliko hili balaa la kodi zitakazomkabili pindi atakapoweka mguu wake nchini!
Tumemfanya mtalii ni al shabab, hatakiwi nchini kwetu na silaha uetu kuu against yeye ni kodi kuubwa.
Taarifa ndio hiyo sio sababu ya ombaomba
Umesoma bandiko zima? Sababu katoa nyingi ikiwemo tozo, rudia kusoma
 
Umesoma bandiko zima? Sababu katoa nyingi ikiwemo tozo, rudia kusoma
Nimesoma lote, na mimi ni mdau ndio nakwambia tozo ndio tatizo mgeni anaangalia destination nafuu ili aweze kwenda na mwakani tena! Tanzania ni ghali sana na sababu ni hiyo ombaomba wamejaa dunia nzima. Tozo kubwa ndio laana ya utalii wetu
 
Nimefanya kazi ya utalii, bro professional tour guide haombi hombii mkuu, kila kitu Kiko kwenye website plus amount ya day unayo mlipa guide wako.ukipendezwa zaidi unatoa zaidi.mataifa yenye njaa njaaa kama Germans,France, Italy na Spain wageni wake huwa niwagumu Sana kwenye tip trust me.taifa kubwa marekani au muingereza ukifanya nae kazi tip mlima.mradi apende service
 
Na Wasije.....yaan nishindwe kwendaa mahal kisa kuna maskin mtu 1 ataniomba hela..haingii akilin
 
Na Wasije.....yaan nishindwe kwendaa mahal kisa kuna maskin mtu 1 ataniomba hela..haingii akilin

Mkuu naona hujakutana na ombaomba wa kulazimisha
Wanakera sana

Sidhani kama huyo Mama kashindwa kudhibiti ila basi tu na uchumi umeyumba na mambo yamebadilika sana
 
Nimefanya kazi ya utalii,bro professional tour guide haombi hombii mkuu,kila kitu Kiko kwenye website plus amount ya day unayo mlipa guide wako.ukipendezwa zaidi unatoa zaidi.mataifa yenye njaa njaaa kama Germans,France, Italy na Spain wageni wake huwa niwagumu Sana kwenye tip trust me.taifa kubwa marekani au muingereza ukifanya nae kazi tip mlima.mradi apende service

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Tip ni lazima? Shida iko hapa je ni lazima tip?
 
Tour Operators nao walipe vizuri I don't condone ambacho wanafanya ila Tour Guides hawana mishahara kabisa na wanalipwa kutokana na kazi.
İshu ni kwamba tour oparater wanawaachia majumu ya kulipa mishaha watalii kupitia tip
 
Back
Top Bottom