Tour in Zanzibar

Kwa ambaye hatujawahi kuja Zanzibar embu tuambie kuna nini cha maana sana hapo Fumba kwa bakhresa

kazimkazi kwa Samia?
Just ni kuenjoy tu kubadilisha mandhari

Pia unaweza kugoogle ukajionea mengi zaidi
 
Kwa bei za hoteli nilishasema kua chumba cha bei ya chini ni Elfu 50 sasa apo itabdi mchukue vyumba viwili ambavyo ni laki moja
Mbona umesema Bei ya chini ni 35k , hiyo 50k inatoka wapi tena mkuu
 
Mzanzibar? Tukuachie familia yetu? Wewe? Famasihara nini?
 
Kwa upande wangu nishatembelea mbuga za wanyama kama

Arusha National Park

Manyara National Park

Mikumi National Park



Inshort kuna furaha yake ya Kutembea sehemu ngeni unaliwaza mwili unaipumzisha akili n.k
Kati ya hizo mbuga 3 ulizotaja ipi nzuri yao na ipi ya pili na ya mwisho.
Elezea uzuri wake na mapungufu yake
 
Kati ya hizo mbuga 3 ulizotaja ipi nzuri yao na ipi ya pili na ya mwisho.
Elezea uzuri wake na mapungufu yake
Duh unge google ndo ungepata details nzuri ila ata mm nasikia serengeti ndo mbuga nzuri japo sijawahi fika
 
Mzanzibar? Tukuachie familia yetu? Wewe? Famasihara nini?
Umdhaniaye ndie kumbe sie

Acha kuamini stori za kuambiwa mm nishakaa bara for almost 9yrs najua unachokimaanisha
 
Brother mimi nipo Zanzibar nina siku kadhaa sasa nimekuja kutafuta maisha. Kwa uzoefu wako, unaweza kunipa muongozo wa wapi naweza kupata kazi/vibarua?
Ni PM tuongee zaidi
 

Kazi nzuri ila kwenye hoteli hizo lodge za 35k sipendekezi sana utaharibu kazi Yako.

Ungejitahidi kupata connection za watu wenye BnB wanakua na nyumba zenye Kila kitu na vyumba viwili au viratu ni Bei nafuu sana hasa Kwa wenye familia.

Pia ungetengeneza route zako ukaweka na makadirio ya gharama. Kwa mtu ambae hajafika ukimwambia anataka nini itamchanganya tu.

Weka mfano day 1 stone town, day 2 kizimkazi day 3 Nungwi au Fumba. Weka gharama za boat na malazi. Kidogo inampa picha mtu ajipange namna Gani.

Shukrani
 
Naunga mkono hoja!
 
Kuhusu gharama mkuu mbona nilishazitoa

Gharama nyingi nimeshaeleza apo juu angalia vizuri tu

Ila Asante sanaa kwa ushauri wako

Mungu akubariki
 
Kuhusu gharama mkuu mbona nilishazitoa

Gharama nyingi nimeshaeleza apo juu angalia vizuri tu

Ila Asante sanaa kwa ushauri wako

Mungu akubariki

Nimekuelewa, umeelezea gharama za boat ambazo zinafahamika.

Nilichoshauri, wengi wanataka kuja na familia zao au kikundi, ni nadra sana mtu anaekuja peke yake ahitaji msaada wa tour japo wapo.

Kwakua wewe unataka kufanya kibiashara lakini uwarahisishie watu wanaotaka kuifaidi Zanzibar, ungetengeneza ratiba ya utalii wako utakavyoenda.

Mwingine atakaa siku Moja anataka aende Prison Island akaone Kobe na azunguke Stone Town . Unaweka makadirio ya hizo gharama.

Kuna wale wenyewe Stone Town walishafika au hawahitaji kupoteza muda, unawashauri waende Jozani au Kizimkazi wakaone Dolphin.

Kuna wale wanataka waende fungu la mchanga n.k

Kwa ufupi tengeneza program zako na makadirio ya gharama ili mtu achague au kujua namna ya kujipanga .

Kuna watu watahamasika baada ya kupata taarifa sahihi kutoka kwako. Na ukifanya vizuri, utakimbia wateja.
 

Hii 35,000 ni hapo stone town?

Hebu Nipe connection mie

Mara kibao nakuja nalala kuanzia 60k-100k ina maana napigwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…