Nani atatuwakilisha vyema bara la Africa katika world cup inayokuja, au ndo mambo yaleyale ya robo fainali sherehe?.Sikuhizi visingizio vya refa naona vinapungua kwaajili mpira upo live kwenye luninga zetu, sasa sijui watatupa kisingizio gani wakichemsha mwakani. Nadhani Ivory Coast wana tim nzuri, nawapa nafasi kubwa ya kuingia semi finals. South Africa..mmh!algeria ni under dog, Nigeria na Cameroon wanabidi wajitahidi kujiandaa zaidi.
Je Tanzania tunajifunza nini, apart kuangalia tu kila miaka nenda rudi wenzetu wakiwa wanashiriki mashindano makubwa?.
Kila siku tutaishia Challenge tuuuu hatuendi popote wala nini, hata African cup of nations jamani?majirani zetu wao wanashiriki kama Msumbiji....sisi twabaki kushangilia wenzetu.