Toyota Altezza Gita (Wagon) Thread: Karibuni tujuzane ubora na udhaifu wa gari hizi

huyo jamaa gari yake ina maajabu gani hadi awe anawabeba?
 
inakuaje ina cc 4000 then horse power ndogo?
 
nataka nichukue hiyo tezza yenye cc 3000 .I guess itakuwa na nguvu balaa
Yes, ile ina nguvu kweli lakini inakiu balaa. Ina engine ya 2JZ. Ila kwa Japan, nafikiri Altezza ya cc3000 ni Gita pekee. Zile saloon ni cc2000.

Ile saloon ya four cylinder yenye engine ya 3S ina nguvu zaidi kuliko ya six cylinder yenye 1G. So unaweza kuchukua hiyo. Hazipishani saana nguvu na ile yenye c 3000, ila yenyewe ulaji wake wa mafuta ni mzuri. Shida yake ni kwamba hiyo engine 3S-FE Beams dual vvti iko kwenye Altezza RS200 pekee. So ikizingua inabidi uitafute hiyo hiyo ya Altezza.
 
modifications gani ukiongezea kwenye altezaa inafanya iwe nzuri/ yenye starehe zaidi
Aise, Altezza kwa upande wa starehe hapana. Suspension zake ni ngumu, zimekaza, na ndani imeshakuwa ya kizamani kidogo kulinganisha ni kina Brevis na Crown. Wengi huwa wanaipiga mziki wa maana, na kuongeza radio ya android, kidogo inapendeza.
 
hiyo yenye engine ya 2JZ inakula kiasi gani kwa km 1?
 
zile zenye uwazi kwenye bonnet ni engine gani ile?
 
powerseats na seat heaters ndo nini mzee?
 
ni altezza gani ina horsepower kubwa?
 
hivi zile zenye antenna kwenye boot ndo hizo Gita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…