Toyota Altezza Gita (wagon) ni moja kati ya magari mazuri na imara kuwahi kutengenezwa na kampuni ya kutengeneza magari ya Toyota kwa kipindi cha miongo kadhaa iliyopita. Gari hili liliingia sokoni mwaka 2001, miaka mitatu baada ya gari la
Altezza (sedan) kupata mafanikio makubwa sokoni tangu lilipoanza kutengezwa mnamo mwaka 1998. Altezza na Altezza Gita ni magari yaliyotengenezwa kupambana na magari ya Ulaya kama
BMW 3 series,
Mercedes C class na
Audi A4, ambayo kiutaalamu huwa yanawekwa kwenye kundi la Entry Level
Compact Executive Salon/Wagon.
Kwa soko ya Ulaya na Marekani Altezza na Altezza Gita ziliuzwa kwa jina la Lexus IS, na Lexus IS SportCross.
View attachment 898986
Kuna matoleo matatu ya Altezza Gita kutokana na engine zake. Kuna
AS200 yenye
cc2000 ambazo ndio nyingi. Hizi zinakuja na engine ya
1G-FE, na
AS300 ambayo ina engine ya
2JZ-GE yenye
cc3000. Hizo engine zote ni
6 cylinder. Pia kuna models chache za Altezza Gita,
RS200 zenye engine ya
3S-GE. Hii ni engine ya 4 cylinder, iliyoundwa kwa ushirikiano kati ya Toyota na Yamaha. Hii ina nguvu (200-210hp) zaidi ya ile 1G-FE, na mara nyingi inakuwa kwenye Altezza salon.
View attachment 898987
The good
- Gari hili lina muonekano mzuri na usiopitwa na wakati kirahisi (ukizingatia lina umri wa zaidi ya miaka 17). Watu wengi wanashawishika kuliita Altezza new model
- Lina features nyingi kutoka kiwandani kulinganisha na magari ya Ulaya ya kipindi hicho, hasa ukipata Limited edition (yenye seats za leather) mfano power seats kwa dereva na abiria, 6 disc CD changer, 6 airbags etc. Ukibahatisha kupata model ya Lexus ndio utafurahi zaidi. Lina mpaka seat heaters.
- Japo ni sports car, ila liko comfortable vya kutosha kwa aina ya gari, hasa kwenye barabara ya lami
- Vile ni rear wheel drive (linasukuma kwa tairi za nyuma) handling inakuwa safi sana, maana tairi za mbele zinabaki na kazi ya kuliongoza gari tuu. Kiukweli linafurahisha kuendesha, hasa kwenye barabara zenye kona.
- Hizi gari ni very reliable, yaani ni kati ya magari ambayo kiukweli hayana urafiki saana na garage. Yanavumilia shida saana. It is very well made.
The bad
- Linakunywa mafuta zaidi ya magari ya Ulaya ya level moja, kama BMW 3 series (E46) na Mercedes C class (W203).
- Kwa kuwa ni sport car, suspension zake ni ngumu kiasi, na rims za size 17 ambazo zinakuja na gari, tairi linakuwa na low profile, hivyo haliko comfortable saana kwenye barabara za vumbi (rough roads).
- Seats za nyuma ni finyu kidogo kwa watu warefu, hasa kama dereva ni mrefu pia.
- Liko chini saana, hasa kwa barabara zetu za mtaani ambazo mara nyingi haziko kwenye hali nzuri. Hii husababisha watu wengi kuligonga sehemu za chini na kwenye bumper kama wakilitumia bila kuliinua. Na ukiliinua linakuwa bayaa, na linapoteza stability.
- Radio yake ya CD 6 huwa inaharibika kirahisi huo mfumo wa kubadilisha CD hasa inapotumiwa na watu wasio wazoefu.
Cha kuzingatia unapolinunua hilo gari likiwa limetumika
- Models zote za tangu 2001 mpaka 2005 hazina tofauti kubwa, sababu gari hilo halikufanyiwa mabadiliko yeyote makubwa ndani ya kipindi hicho, zaidi ya mabadiliko madogo (facelift) mwaka kwa model ya mwaka 2003 ambapo, taa na navigation screen ndio vilibadilishwa na vitu vichache vya ndani.
- Ukinunua likiwa chini ya km 100,000 hakikisha unamuuliza muuzaji kama alibadilisha timing belt, maana huwa zina kawaida ya kukatika baada ya kufikisha km hizo. Na zikikatika zinaweza kuleta madhara makubwa kwenye engine. Kama ni Japan, hakikisha linabadilishwa huko huko.
- Usinunue ambalo lina dalili za kuwa modified saana kama hauna lengo la kulitumia kwenye mashindano na kupiga misele (drifting). Maana hizi gari zilipendwa saana na racer boys, walikuwa wanazitumia kwenye mashindano, hivyo zilikuwa abused saana.
- Manual transmission inafurahisha saana kuendesha. Ina gia sita. Japo kiukweli, hizi nimeziona chache saana. Automatic transmission nazo hazina shida. Kuna za gia nne, na gia tano. Ukiwa na auto, hakikisha unatumia ATF ya Toyoto TIV, kama hauwezi, basi bora usibadilishe kabisa.
- Engine ya 1G inatabia ya kuvuja oil kwenye Valve cover, hasa kama utajaza engine oil kupita kiasi wakati wa kufanya service. Hakikisha oil ya viscosity ya 5W40 au 10W40, na usizidishe lita 4.1. Mafundi wenge huwa wanashauri kuweka lita 5. Ni makosa ina haribu oil seals. Na usitumie oil filter za elfu 5, nunua genuine 😉😉.
- Hizi gari hasa zikiwa na km nyingi, bush za low control arms (lower wishbone) za mbele huwa zinaisha, na kusababisha gari kula tairi upande wa ndani. Usijaribu kufanya wheel alignment ukiona inakula tairi. Hilo sio tatizo la alignment. Tafuta hizo wishbone bushes ubadilishe. Hakikisha unaweka alama kwanza kabla ya kufungua wishbone, maana ukikosea kuzirudisha kwenye alignment tu unaharibu handling na litaboa kuendesha..
Maoni yangu
Hizi ni gari nzuri saana, ukizitunza unaweza kuzitumia kwa muda mrefu saana bila kukuletea shida yeyote. Na idadi yake sio kubwa, hivyo ukiwa nalo linakuwa unique kidogo. Ila kama unaishi sehemu yanye barabara mbovu, halikufai, hata kama wewe ni dereva mzuri. Utachoka kuliendesha.
Karibuni tupeane uzoefu.