Toyota hizi...!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Si kwamba nazikandia hizi gari za kijapan la hasha. Nimewahi kuzimiliki Chaser mayai na balloon GX90. Kila moja imevuma kwa nyakati zake. Zikisifika kwa wepesi mwendo (kuchanganya haraka) kiyoyozi kama Greece land. Zimepita model nyingi.

Tunamalizia enzi za Harrier TAKO LA NYANI zimechuja haraka baada ya nyingi kupiga chini.

TOYOTA crown bado iko juu lakini nayo inaendelea kuchinja watu. Simlaumu mjapani katengeneza kwa matumizi yake na taratibu zake. Huku hatuzingatii hili kabisa

Mwisho tunaishia kulaumu na kusema TOYOTA hizi....!!!
lakini pamoja na Toyota nyingi kuwa na viwango vidogo vya usalama kulinganisha na gari za ulaya bado tatizo ni letu sisi wenyewe.....!

ELIMU JUU YA VYOMBO VYA MOTO hasa gari nyepesi za kijapani ni finyu mno...! tumepoteza damu changa nyingine Kabuku. Damu ya Rchunga... Rip [emoji1019]
 
Pole kwa waliofikwa na hayo. Ukiangalia siku hizi madereva wengi wanajua kukanyaga mafuta na break basi. Sheria na alama za barabarani hawazijui, na wanaozijua baadhi hawazifuati kabisa, achilia mbali kujua uwezo wa gari na namna ya kulihandle barabarani ndio shida kubwa zaidi.
 
Udereva wa mitaani.... Hakuna hata nafasi ya kufundishwa kuhusu uchumi na athari za mwendokasi
 
Apumzike kwa amani.

Gari linatabia kama za baiskeli ukishalizoea huoni cha kukutisha unajikuta umekuwa Expert suddenly matokeo yake ndio hayo.
Tuwe makini na haya madude kuna jamaa yetu mmoja aliizoea sana Toyota Land cruiser ya jeshi fulani hata akawa anafanya THE IMPOSSIBLE matokeo yake sasa hivi anajua aliko yeye mwenyewe.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 😥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…