Toyota hizi...!

Toyota hizi...!

Je speed kubwa na kuto kuwa makini barabarani kwa gari ya mjerumani huwezi kupata ajari??

Funguka zaidi tuweze kujifunza kuhusu hizi gari za mjerumani cc: Mshana Jr
Ukiingia uvunguni hata ukiwa unaendesha volvo lazma ufe tu japo kwa usalama hakuna gari inaikuta volvo kwa rating.
 
Huku mjini anaovateki bila kuangalia anakuwashia taa unampisha,tabia hujenga mazoea wakienda highway malori yanawanyoosha
Tabu iko pale pale, nina shemeji yangu anachezaga rally, yeye ni msoma ramani ila fujo za gari zinaishiaga mjini tu. Akiwa safari unaweza sema mlemavu 😂😂😂 hasa akiwa kabeba watoto. Speed haivuki themanini.

Siku nasafiri nae tulianza safari saa 8 mchana mpaka saa 6 usiku hio ni Moshi-Dar na hapo tumekula boda ya Msata Bagamoyo.
 
unalo sema kweli kaka,mfano huku south africa gari hizi hazitakiwi kabisa toyota za kijapan,wanagari zao ambazo ni sawa zengine zina fanana lakini ukiliona unasema hili gari mfano VITS inaitwa YARIS,unajua ile vits new model ilifanya vibaya lakini iliyopo huku ukiiona unaweza kusema IST jinsi ilivo ngumu.
kiufupi tu ajali zipo sema barabara sio salama na vyombo vyetu.kwa nchi yetu
toyota sauzi zipo kibao acha kupotosha..sema zilizopo zinautofauti kidogo na za huku..zina speed 220 na kuendelea.
 
Utafikiri katumwa[emoji24][emoji24][emoji24]
Hawa madogo wanakimbiza haya magari mpk unashangaa.... Siku nakatiza zangu na speed yangu ya kizee... nikashangaa kaPasso kananipita kama nimesimama. Nikashangaa na kujiuliza hawa madogo huwa wanawaza nini na haya mambio???
 
Hii sehemu kama naifahamu ina barabara moja nzuri sana inavutia kukanyaga wese...
 
Safiri usiku angalau upunguze kutoa hela ya mboga...

Maana kwa huo muda unataka kutumia speed 150kph inakuhusu...
Ajali ya mtu mwingine haiwezi kunifanya niongope kukanyaga mafuta..... Kesho asubuhi na safari ya Mbeya+Tunduma nikitoka Dar saa kumi na mbili asubuhi nataka saa kumi niwe Tunduma.... Nimesha andaa na hela ya faini kabisa ya matrafiki
 
Royal saloon tena bado mbichi kabisaaa ila ndio ishakula kichwa tena
Si kwamba nazikandia hizi gari za kijapan la hasha. Nimewahi kuzimiliki Chaser mayai na balloon GX90. Kila moja imevuma kwa nyakati zake. Zikisifika kwa wepesi mwendo (kuchanganya haraka) kiyoyozi kama Greece land. Zimepita model nyingi.

Tunamalizia enzi za Harrier TAKO LA NYANI zimechuja haraka baada ya nyingi kupiga chini.

TOYOTA crown bado iko juu lakini nayo inaendelea kuchinja watu. Simlaumu mjapani katengeneza kwa matumizi yake na taratibu zake. Huku hatuzingatii hili kabisa

Mwisho tunaishia kulaumu na kusema TOYOTA hizi lakini pamoja na kuwa na viwango vidogo vya usalama kulinganisha na gari za ulaya bado tatizo ni letu sisi wenyewe.

ELIMU JUU YA VYOMBO VYA MOTO hasa gari nyepesi za kijapani tumepoteza damu changa nyingine Kabuku. Damu ya Rchunga... Rip [emoji1019] View attachment 1105974View attachment 1105975View attachment 1105976
 
Wnaita mnyama wenyewe
IMG-20190513-WA0061.jpeg
 
toyota sauzi zipo kibao acha kupotosha..sema zilizopo zinautofauti kidogo na za huku..zina speed 220 na kuendelea.

toyota ya mjapani na toyota ya hapo ni tofauti ndugu.kama umenunua ya japani hapa wanakubebea mpaka mpakani na kukukabizi
 
Huyo wa gari kuwaka moto imekuaje ina maana milango ilijilock au
Kuna mwenzake amekufa baada ya Harrier kuacha njia akiwa kibati na wenzake wawili wamefia eneo linaitwa Mahenge akielekea Mbeya...gari imewaka moto hapohapo ni jirani na Ruaha Mbuyuni...huyo jamaa ni lawyer Mbeya town anaitwa Mwesigwa wametangaza ITV tena lead story leo...hawa vijana huwa hawaelewi la kengele wala mwadhini kwa hiyo ni better kuwatangulizia R.I.P tu.....polisi wanasema ajali imetokea muda si mrefu baada ya jamaa kuandikiwa notification...gari sio bagadu
 
toyota ya mjapani na toyota ya hapo ni tofauti ndugu.kama umenunua ya japani hapa wanakubebea mpaka mpakani na kukukabizi
nachofaham toyota ni brand ya Japan.labda kama unamaana ingine
 
Toyota za Kimarekani mwisho wa kazi speed 220 na hata ugonge jiwe itachubuka tu na kimkunjo kidogo..... hizi gari za mchina inagonga boda Boda inakanika vipande viwiliView attachment 1106081
Tatizo sio No ya SpeedMeter ! Hekima nBusara za Huyo anae kiendesha chombo. Kama were no dereva kuna wakati unakanyaga mafuta unasikia moyo wako unakuambia hapa Mmmhhhhh...... ! Pia gari lenyewe kama were ni msikivu mzuri,gari lina kwambia kabisa hapa too much ! Unatoa mguu kwenye mafuta.... Barabara zetu hizi pia nyembamba, kwa wale tunao endesha magari usiku nafikiri hili watakuwa wanaliona ! Tuwe makini Barabarani, HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE ZAIDI
 
Ilichomfanya hawezi kusahau? [emoji849]

Alipona kwani mkuu?
Hii inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliniambia hii gari iko stable sana ikishapita speed 120 inakamata chini/inatitia,kuna siku alikuwa yuko kwenye 180 kph kufika kwenye kona hakupunguza,ilichomfanya hatakaa asahau,ile gari iliruka nzima nzima ikazunguka juu mara 3 kuja kutua miguu juu kichwa chini,guess what,Toyota Carina wakati huo ndio zilikuwa zinasumbua...
 
Kwakweli hiyo michezo ya kumaliza visahani Mungu anikumbushe nisije jisahau.
R I P!
 
Huyo wa gari kuwaka moto imekuaje ina maana milango ilijilock au
Hapo possibility ni mashine ilipiga mzinga ikiwa kwenye mwendo kasi na immediately ikadaka moto...ukiicheki imepinduka upside down kwa hiyo inaonekana kama walikuwa wamejeruhika ilikuwa vigumu kujitetea...ukiendesha mkoani ukaona vijana wa private wanavyoamka na magari utadhani vichaa
 
Back
Top Bottom