Ukiingia uvunguni hata ukiwa unaendesha volvo lazma ufe tu japo kwa usalama hakuna gari inaikuta volvo kwa rating.Je speed kubwa na kuto kuwa makini barabarani kwa gari ya mjerumani huwezi kupata ajari??
Funguka zaidi tuweze kujifunza kuhusu hizi gari za mjerumani cc: Mshana Jr
Tabu iko pale pale, nina shemeji yangu anachezaga rally, yeye ni msoma ramani ila fujo za gari zinaishiaga mjini tu. Akiwa safari unaweza sema mlemavu 😂😂😂 hasa akiwa kabeba watoto. Speed haivuki themanini.Huku mjini anaovateki bila kuangalia anakuwashia taa unampisha,tabia hujenga mazoea wakienda highway malori yanawanyoosha
Mkuu huo ndio uanaume familia kwanza.Kisahani tatizo kaka ila kama una familia kidogo nidhamu Ipo, sasa hivi sina tofauti na Kobe.
Mkuu, rudia kusoma kwenye aya yangu ya pili.Kwani mjerumani ukipigwa uso kwa uso haudanji ama gari haibonyei. Kifo ni kifo tu
Angalia na Volvo(The Safest Car in the World)
View attachment 1106238View attachment 1106238
Soma hio RED....ultra high strength STEEL
toyota sauzi zipo kibao acha kupotosha..sema zilizopo zinautofauti kidogo na za huku..zina speed 220 na kuendelea.unalo sema kweli kaka,mfano huku south africa gari hizi hazitakiwi kabisa toyota za kijapan,wanagari zao ambazo ni sawa zengine zina fanana lakini ukiliona unasema hili gari mfano VITS inaitwa YARIS,unajua ile vits new model ilifanya vibaya lakini iliyopo huku ukiiona unaweza kusema IST jinsi ilivo ngumu.
kiufupi tu ajali zipo sema barabara sio salama na vyombo vyetu.kwa nchi yetu
Hawa madogo wanakimbiza haya magari mpk unashangaa.... Siku nakatiza zangu na speed yangu ya kizee... nikashangaa kaPasso kananipita kama nimesimama. Nikashangaa na kujiuliza hawa madogo huwa wanawaza nini na haya mambio???Utafikiri katumwa[emoji24][emoji24][emoji24]
Ajali ya mtu mwingine haiwezi kunifanya niongope kukanyaga mafuta..... Kesho asubuhi na safari ya Mbeya+Tunduma nikitoka Dar saa kumi na mbili asubuhi nataka saa kumi niwe Tunduma.... Nimesha andaa na hela ya faini kabisa ya matrafiki
Si kwamba nazikandia hizi gari za kijapan la hasha. Nimewahi kuzimiliki Chaser mayai na balloon GX90. Kila moja imevuma kwa nyakati zake. Zikisifika kwa wepesi mwendo (kuchanganya haraka) kiyoyozi kama Greece land. Zimepita model nyingi.
Tunamalizia enzi za Harrier TAKO LA NYANI zimechuja haraka baada ya nyingi kupiga chini.
TOYOTA crown bado iko juu lakini nayo inaendelea kuchinja watu. Simlaumu mjapani katengeneza kwa matumizi yake na taratibu zake. Huku hatuzingatii hili kabisa
Mwisho tunaishia kulaumu na kusema TOYOTA hizi lakini pamoja na kuwa na viwango vidogo vya usalama kulinganisha na gari za ulaya bado tatizo ni letu sisi wenyewe.
ELIMU JUU YA VYOMBO VYA MOTO hasa gari nyepesi za kijapani tumepoteza damu changa nyingine Kabuku. Damu ya Rchunga... Rip [emoji1019] View attachment 1105974View attachment 1105975View attachment 1105976
Mzuka wa kumaliza kisahani
toyota sauzi zipo kibao acha kupotosha..sema zilizopo zinautofauti kidogo na za huku..zina speed 220 na kuendelea.
Kuna mwenzake amekufa baada ya Harrier kuacha njia akiwa kibati na wenzake wawili wamefia eneo linaitwa Mahenge akielekea Mbeya...gari imewaka moto hapohapo ni jirani na Ruaha Mbuyuni...huyo jamaa ni lawyer Mbeya town anaitwa Mwesigwa wametangaza ITV tena lead story leo...hawa vijana huwa hawaelewi la kengele wala mwadhini kwa hiyo ni better kuwatangulizia R.I.P tu.....polisi wanasema ajali imetokea muda si mrefu baada ya jamaa kuandikiwa notification...gari sio bagadu
nachofaham toyota ni brand ya Japan.labda kama unamaana inginetoyota ya mjapani na toyota ya hapo ni tofauti ndugu.kama umenunua ya japani hapa wanakubebea mpaka mpakani na kukukabizi
Tatizo sio No ya SpeedMeter ! Hekima nBusara za Huyo anae kiendesha chombo. Kama were no dereva kuna wakati unakanyaga mafuta unasikia moyo wako unakuambia hapa Mmmhhhhh...... ! Pia gari lenyewe kama were ni msikivu mzuri,gari lina kwambia kabisa hapa too much ! Unatoa mguu kwenye mafuta.... Barabara zetu hizi pia nyembamba, kwa wale tunao endesha magari usiku nafikiri hili watakuwa wanaliona ! Tuwe makini Barabarani, HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE ZAIDIToyota za Kimarekani mwisho wa kazi speed 220 na hata ugonge jiwe itachubuka tu na kimkunjo kidogo..... hizi gari za mchina inagonga boda Boda inakanika vipande viwiliView attachment 1106081
Hii inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliniambia hii gari iko stable sana ikishapita speed 120 inakamata chini/inatitia,kuna siku alikuwa yuko kwenye 180 kph kufika kwenye kona hakupunguza,ilichomfanya hatakaa asahau,ile gari iliruka nzima nzima ikazunguka juu mara 3 kuja kutua miguu juu kichwa chini,guess what,Toyota Carina wakati huo ndio zilikuwa zinasumbua...
Hapo possibility ni mashine ilipiga mzinga ikiwa kwenye mwendo kasi na immediately ikadaka moto...ukiicheki imepinduka upside down kwa hiyo inaonekana kama walikuwa wamejeruhika ilikuwa vigumu kujitetea...ukiendesha mkoani ukaona vijana wa private wanavyoamka na magari utadhani vichaaHuyo wa gari kuwaka moto imekuaje ina maana milango ilijilock au