Toyota Noah Si (new shape)

Toyota Noah Si (new shape)

geezerlad

Senior Member
Joined
Dec 31, 2017
Posts
182
Reaction score
195
Naomba kufahamu kuhusu Toyota Noah Si (new shape) Ubora wake na changamoto zake kwa aliyewahi itumia hii gari.
 
Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    34.8 KB · Views: 8
  • f.jpg
    f.jpg
    55.2 KB · Views: 11
Naomba kufahamu kuhusu Toyota Noah Si (new shape) Ubora wake na changamoto zake kwa aliyewahi itumia hii gari.
Ni gari nzuri sana japo sio ngumu kama zile za zamani, ila ukitunza body ni gari nzuri sana ina injini ya 3zr ambayo unaipata hata kwenye toyota wish kuanzia 2007 hadi 2013 japo sio zote, ni economy sana kulinganisha na zile noah za nyuma yake pia ni CVT gearbox, kama unaitaka usiiache utakuja kunishukuru baadae
 
  1. Umeshawahi kumiliki gari
  2. Una gari nyingine
  3. Unafahamu machimbo ya spare, garage na mafundi wazuri?
Kama moja ya jibu katika maswali hapo juu ni HAPANA, basi usinunue hii gari!
 
Naomba kufahamu kuhusu Toyota Noah Si (new shape) Ubora wake na changamoto zake kwa aliyewahi itumia hii gari.
Niliwahi panda Noah (2012) Zanzibar, hiyo yenye new shape yenye injini ya 3ZR ambayo ili replace injini ya 1AZ iliyosababisha hizi gari na Voxy kuchukiwa sana. Mmiliki wa ile gari aliisifia sana hasa kwenye fuel consumption na engine performance.
 
1AZ hiyo hiyo inafanya vizuri kwenye rav 4, nadha itategemea. Lakini 3zr -fe ndio successor wa 1AZ , double performance kwa mafuta kidogo
 
1AZ hiyo hiyo inafanya vizuri kwenye rav 4, nadha itategemea. Lakini 3zr -fe ndio successor wa 1AZ , double performance kwa mafuta kidogo
Kwenye Rav 4 kulifungwa injini ya 1AZ-FE, ila Voxy iliwekewa 1AZ-FSE ambayo ni 'Gasoline Direct Injection (GDI). Sasa hii yenye GDI inayohitaji mafuta masafi sana ikawa na changamoto nyingi. Uchafu kdg tu, misfire za kutosha.
 
Back
Top Bottom